Haya mabehewa TRC Wamezitolea ufafanuzi wa Kitaalamu kabisa

Haya mabehewa TRC Wamezitolea ufafanuzi wa Kitaalamu kabisa

Ukiangalia haya ni kama yale ambayo huwa yanauzwa kupatana.com au zoomtanzania. Sijui lakini. Au kikuu.com Naamini ukiwa mzoefu wa ku tafuta tafuta vitu kwenye mtandao utayakuta used hapa bongo au nchi za wenzetu.

Haya mabehewa utaambiwa hayajawahi pata ajali na pia aliyekuwa anayatumia ni mwanamke tena bibi kizee.

Vichwa vyake kwenye matangazo utaona wameandika havijawahi shushwa engine. Limetembea kms chache yu 47,000 haijawahi gongwa. Unamwaga tu oil ,jino moja Msamvu hii hapa.

Jamaa wanasema hayo ya kizamani ni maalumu kwa ajili ya safari za mbali. Usiulize mbali wapi. Halafu yale ya kisasa yatakuwa yanapiga routes za hapa hapa town. Mbagala ,gongo lamboto, mwenge,Tegeta na Mabibo.

View attachment 2425959
Hayo kwa Mujibu wa TRC Ni Mabehewa ya safari ndefu yaani Kigoma na Mwanza 😆😆
 
TRC hebu acheni kuwatania watanzania, hivi mnafikiri ni mambumbu kiasi kwamba hawajui hata kutumia google search?
 
Kuna Watu hawana Aibu Serikalini, utadhani hizo Pesa za Kodi ni za Baba zao, pumbavu zao!
 
Ikiwa hizo bedford/leyland model ni kwa ajili ya masafa marefu (kigoma, mwanza) mbona yameletwa mapema sana kabla hata hiyo sgr hajafika huko?
Wee mtoto huna adabu? Acha kuuliza uliza maswali sehemu wakubwa wamekaa.
 
Ikiwa hizo bedford/leyland model ni kwa ajili ya masafa marefu (kigoma, mwanza) mbona yameletwa mapema sana kabla hata hiyo sgr hajafika huko?
Mkuu hawa watu ni mbumbumbu kweli kweli. Unaleta mabehewa wakati reli bado kabisa? Wana akili kweli hawa watu?
 
Mkuu hawa watu ni mbumbumbu kweli kweli. Unaleta mabehewa wakati reli bado kabisa? Wana akili kweli hawa watu?
hata wao wanajua ni waongo wameshakula. Disaini hiyo ya mabehewa siyo ya masafa marefu ni kwa ajili ya masafa mafupi ya mjini. Miaka ya kati ya 2000 nilikuwa Brussells, nilikuta underground train zina mabehewa ya design hiyo.

Kwa mtindo huu, hata ndege wanazodai wameshalipia si ajabu tukaletewa zilizotumika qatar airways, Turkish airline au emirates
 
Wee mtoto huna adabu? Acha kuuliza uliza maswali sehemu wakubwa wamekaa.
sasa wazee mnapokula muwe mnajifunza kusema hata uongo ulionyooka. behewa za design hiyo ulaya hutumika mjini tu. ni za masafa mafupi ya mjini si safari ndefu.
 
Oya kiufupi keshalizwa mtu kama tunataka kuendana na mabadilikobya kitekinolojia hizo sio behewa za kisasa walizotudanganya kipindi kile
 
Back
Top Bottom