Haya magari ya hivi karibuni yenye namba A yanamilikiwa na akina nani?

Weka picha acha majingu hatukuelewi. Subiri miezi mitatu ununue G wagon na Lc 300 Porche, Y63, fortuner 2024 zilizo zama kwenye maji dubai uache chuki
 
yaani mimi mwenyewe nashangaa sasa huo u secret service unatoka wapi? Sababu hwavai unifrom au n vp? Sema mwisho wasiku kila mtu anaweza akaleta storii yake kuchangamsha genge.
Ndio ukweli.
Utakuta mtu anafahamiana na informer, anakuja kusema ni TISS yule. Kazi ya informer inaishia kutoa taarifa tu, hajui lolote kuhusu TISS. Na ma informer ndio wanatafuta sifa ssna kutambulika. TISS huwezi mgundua kwa mwonekano wala maongezi. Ni kitu inafundishwa kabisa chuoni
 
Sasa asipokupa si utamchukulia poa mkuu?

Lazima akupe, na wengine wakipigiwa simu ya kazini anaweka loud speaker ili mjue siyo mwenzenu.
Ni informer hao. Sio TISS.
Chuoni kitu cha kwanza kukutambulisha kama umeiva ni kuweza kutunza siri na kutojulikana.

Huwa kuna wahitimu wanaenda kufanya field kwenye kambi za jeshi. Wakikamatwa nanasurubiwa hasa ila hawatoi siri, mwishoe wanapelekwa polisi na huko wanaomba kuongea na ndugu zao kutoa taarifa,.................
 
Ujinga wa nchi yetu, polisi hatakiwi kuogopa kuwashika. Awashike wajieleze kuwa wao ni Tiss.

Ila kuna hii ya kufanya update ya toyota LC nayo unaweza shtuka hii namba A ukichukua kadi gari ya zamani bodi mpya.
Nchi haina ujinga.
Wananchi ndio wenye ujinga.
 
Wenye kutumia namba feki hapa bongo ni polisi. Kikosi maalum.

Gari rasmi za kiofisi za TISS zina namba og
Gari za matukio ndio hupewa namba feki
Nafikiri neno feki sio sahihi bali special numbers
Ila kama nchi kama nchi ndio wameamua iwe hivyo sawa
Ila naona ni kama kuji exposed kirahisi kwa mtu yeyote
Hata criminals wakiona namba tofauti mbele ya nyumba zao mbona wanakimbia kabisa
 
Nafikiri neno feki sio sahihi bali special numbers
Ila kama nchi kama nchi ndio wameamua iwe hivyo sawa
Ila naona ni kama kuji exposed kirahisi kwa mtu yeyote
Hata criminals wakiona namba tofauti mbele ya nyumba zao mbona wanakimbia kabisa
Kuna Fake kwa maana nyingi huwa haziko kwenye system yoyote hapa tz.
Halafu kuna special numbers ambazo ziko kwenye system ila zinatumiwa kimakosa.
 
Mhhh!
 
Ni magari ya viongozi au wafanya biashara
 
Usikariri mambo TISS ya Enzi za Nyerere na sasa hivi Kuna utofauti mkubwa sana katika Swala la maadili ya utumishi Hadi uzalendo

Kuna mess up zilifanyika katika recruitment hasa kuchomekana ndugu na hii inapelekea watu walioko kwenye hiyo idara kutokuwa waadilifu na kutoa Siri...matukio mangapi ya ikulu yanavujishwa na watumishi hao hao wa TISS wasio na maadili? Kwani polisi ushenzi wanaofanya chuoni hawajaenda huko CCP? Tena walikuwa wanakaa miezi 9 now imekuwa 12 lakini Bado wanaongoza Kwa ushenzi sembuse hao TISS wenye short course

TISS kibao wapo wanaotoa Siri na hii ni kutokuwa na vijana au watu wasiojielewa ambapo imetokana na kuchomekana ndugu kwenye taasisi nyeti

Sent from my Infinix X652C using JamiiForums mobile app
 
Nadharia iko kama unavyosema.
Ukijua tofauti ya hawa watu Case officer, sources , Bridge Agent, na Floater utaelewa nilichosema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…