Haya maisha yanapotea kwa kasi. Kuna wakati yatabaki kwenye vitabu vya simulizi tuu

Childhood memories.. Watoto wetu watayasoma haya kama simulizi za kufikirika😭😭😭
Village life.jpeg
 
Tupostie na mitishamba maana wazee wanaondoka na maarifa yao. Yuliobakia hata kichwa kikiuma tunakimbilia panadol
 
Nitakuja na mada yake kamili
 
Maisha ya kijijini.. Mandhari za kuvutia sana.. Changamoto kiduchu.. Wote mnafamiana.. Hakuna gesti za wageni au ni chache na hizo chache hazina shorttime na hazina vibao vya vyumba vimejaa😀
Hata Dar es salaam nakumbuka mwaka 1980 ilikuwa ukienda mjini unakutana na watu karibu wote unawajua.

Huyu unasoma naye shule. Huyu unaenda naye kanisani. Huyu umecheza naye mpira.

Wachache sana wanakuwa watu huwajui kabisa.

Leo vurugumechi hata nani mkazi nani mpazi hujui.
 
Yaani leo hii Upanga inaonekana kubwa sana watu hawajuani
Miaka ya 80s/90s hakuna nisiowajua tulioishi miaka ile kuanzia mwanzo wa Upanga maeneo ya Fire, Watoto wa Mzee Masasi, kina Mtulia famiy Umoja wa vijana miaka ile kuna uwanja wa mpira, na kwenda karibia na mpaka SeaView kina biotto , Polisi selander bridge nyuma kuna maflat kibao, na kurudi upande maeneo ya Zanaki wa kina Obesi na Kipingu wa Vijana basketball,
Huko kote tumetembea wakati watoto na mpira wa kufuma na nyloni kutafuta mechi.

Mtaa wa Mazengo kina Pemba family kina Terrorist na Chuche, ukienda mwisho wa Mindu kina Galinoma family
Ukirudi huku Mathradas kina Natepe na Mazyuni, Scaba Scuba

Watoto na vijana wote maeneo ya Muhimbili na Tambaza family na Duche family na kina Aby Spartan familiy, yaani nilikuwa nawajua Upanga nzima, Uwanja wa skauti, yaani tulikuwa tunazurura sio mchezo
Mkikutana na watesi wenu ngumi zinaanza kesho mnakutana tena mnacheza mpira Don Bosco.
Kwa ujumla Upnga yote tulikuwa tunajuana
Leo hii watu hawajuani kabisa , watoto wanafungiwa ndani kucheza games na watu wapya wanakuja na kuondoka sio kama zamani wanakaa kukulia eneo moja.

Leo hii hata Ilala watu hawajuani, watu wote wapya, na sio wanaishi kijamii kujuana na nyumba zote siku hizi Ilala zina mageti makubwa, sio zile enzi za timu ya Bom na Ashanti, zile mechi za uwanja wa shule ya Uhuru zilikuwa ni noma
 
Nakuelewa sana mkuu.

Umenitajia watu sijawasikia siku nyingi sana hapo.

Nimerudi likizo Upanga pale maskani nakuta hamna watu kabisa, kina watoto wadogo wanatoka kwenye mageti wakiniangalia eti wananiona mimi ndiye mgeni.

Wakati sie tuko pale tangu enzi za Museveni na Okello wanatukanana.

The real Yoweri Museveni and Tito Okello.
 
Back
Top Bottom