Haya majenereta yanaweza kutoa na kupeleka maji umbali gani?

Haya majenereta yanaweza kutoa na kupeleka maji umbali gani?

Kimla

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2008
Posts
3,810
Reaction score
6,599
Jamani nimeambatanisha picha za maelezo ya generator mbili za kuvuta na kusukuma maji .Naomba mtaalamu aniambie generator hizi Kila Moja inaweza kuvuta maki kutoka vhanzo kwa umbali Gani na kutupa majo Kwa umbali Gani?na kiwango cha maji yakusukumwa kwa dakika ni kiasi gani?

IMG_20240313_155056.jpg

IMG_20240313_155741.jpg
 
Hizo ni water pumps mkuu, zinazo endeshwa na Engines,

Picha ya kwanza pump yake inaweza:-
1.kuvuta maji kutoka chanzo kwa umbali usiozidi mita 7
2. kutupa maji Kwa umbali
Usiozidi mita 20
3.kiwango cha maji yakusukumwa kwa dakika ni lita 1,000 kwa dakika moja
 
Inapeleka umbali mrefu,hata kilomita 1
Hints:
Modeli ya injini=GX200
Kiwango cha juu ya pawa =4.8Kw ~ 6.4-6.5Hp
Midomo ya uingizaji maji na utoaji maji =80mm = 3inch
Kiwango cha juu cha utoaji maji =60m³/h (lita 1000 kwa lisaa) hapa ni kama maji yatarushwa hapo hapo na umbali wa chanzo cha maji(kutoka kwenye mdomo wa uvutaji mpaka maji yalipo itakua 0-2m.
Uwezo wa pump kubeba maji =20m(hapa maana yake ni kimo cha ujumla kutoka maji yalipo na eneo la juu zaidi ambapo mpira wako utapita(mfano kichuguu kilivyo,uchore mstari katikati kama una kigawa nusu kwa nusu kutoka chini kwenda juu-kimo hichi ndo hiyo 20m na mpira wako ndo uwe kichuguu kilivyo,chanzo cha maji ndo mwanzo wa mstari chini)
Kwa mzunguko wa injini wa 3600/dakika unaweza kutoa ubora na usahihi wa 53% ya uwezo wa mashine(engine na sio pump-hilo li housing lenye impeller).
Net Positive Sunction Head(NPSH)=kimo cha kipimo kizuri cha presha inayojijenga kutoka kwenye njia ya unyonyaji wa maji kuingia katika pump-centrifuge kuzuia cavitation(maji yako kua mvuke).
Inaweza vuta maji kutoka kimo cha 7m(chanzo cha maji mpaka mdomo wa pump).

Jibu:

Hizi centrifuge pump zinauwezo wa kupeleka maji mbali sana kama utafanya haya,
1.Umbali kutoka chanzo cha maji ukiwa <3m(urefu kwenda juu)-kimo.
2.Kimo cha ujumla kikiwa hicho hicho 3m ama kushuka chini
3.Eneo linalopelekewa maji likiwa ni la chini kuliko pump ilipo-hapa utapata advantage ya gravity
4.Delivery pipe ikiwa ni kubwa-hapa itapunguza msuguano na pressure ndani ya mpira wako,ie ukifunga hiyo pipe ya 3" kwenda juu-say 4" etc
5.Impeller yako iwe in 100% perfect condition
6.Seal zote za kwente Impeller ziwe nzima
7.Mpira wako wa kuingizia maji kwenye pump usi ingize hewa kwa aina yoyote ile.

Hapa 1km+ yatafika

Note:Kila kimoja nlicho eleza hapo juu kikipungua basi na umbali utapungua kwa mrandano.

Thanks in Advance

Taifa moja,Nguvu moja
 
Back
Top Bottom