Haya makundi ya Bongo Fleva yalitupa raha sana sisi Wahenga

Sure,
 
Bon cruz waloimba Jamaa (Wanamwita kaka poa huyu jamaa, wanamwita mambo safi huyu jamaa, wanamwita mtoto wa watu huyu jamaa, sijui si riziki au ni laana huyu jamaa twakuomba tusamehe maulana)
Na Dolphin pose walikuwa wakijiita machalii wawili heat song yao Ni rafiki tu.
 
Kuna kundi walikuwepo Suma Lee na marehemu CPwaa linaitwa Pack Lane.

2Berry wale wapemba wa Chakechake
 
Msondo show zao nlikuwa naenda sana

Ova
Ilianza ikiwa NUTA Jazz band ikakaja kuwa JUWATA Jazz band (Msondo ngoma ukiwa ni mtindo wao) baadaye ikivyokuwa bendi huru kutoka Jumuiya ya Wafanyakazi ndipo ikwa bendi ya Msondo.
 
Waliokuwa consistent na focused walifanikiwa, hata kidogo upatacho ukiwa na malengo unasonga mbele.
Ukiachilia waliokwenda overseas kwa hapa bongo mifano ya Sugu, AY, Mwana FA, Professor J na Lady JD unaweza kuona maana halisi ya kuwa focused, uwezo wa kuwekeza au kutumia brand-name kupenya kwenye siasa ni mifano iliyo wazi. Wapo waliochanganyikiwa na fame na vipesa kidogo walivyokuwa wakipata wakazama kwenye maisha ya parting through and through, drugs, ulevi uliopindukia na vurugu nyingine nyingi sasa watu sampuli hizo imagine wangepata pesa kama wapatazo Bongo flavors wa sasa nadhani wengi wao tungeshazika.
 
Wale wajaruo VP ," mpenzi ungejua moyoni mwangu jinsi ninavyokuthamini"
 
ahaaaa naukumbuka huu wimbo 🙏
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…