Pre GE2025 Haya Maridhiano yanamjenga Rais Samia au yanambomoa kuelekea 2025?

Pre GE2025 Haya Maridhiano yanamjenga Rais Samia au yanambomoa kuelekea 2025?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Ni kweli kabisa.
1. Watanzania wanalia na tatizo la umeme, yeye yupo busy na maridhiano.

2. Watanzania wanalia na mfumuko wa bei, yeye yupo busy na maridhiano.

3. Watanzania wanalia na hali ngumu ya Maisha, yeye yupo busy na maridhiano.

Mama, Watanzania hawatashiba maridhiano. Watanzania wanataka hali bora ya Maisha.

RIP, JPM, BABA YETU MPENDWA.
 
Inawezekana; lakini 2025 akifikisha kura halali 35% amshukuru sana Mungu.

Opposition wana uhakika wa kura za wanachama wao, ccm kuna wanachama wengi wasiofurahishwa na yanayoendelea. Waite wahafidhina au jina lolote, sioni kama wanaweza kumpigia kura.
Yan CCM hata wakisimamisha mbwa atapata zaidi ya kura 35%

Sent from my 220333QAG using JamiiForums mobile app
 
Wanajukwaa kumekua na Siasa mpya ndani ya Nchi yetu iliyopewa jina "Maridhiano" umekua ngumu kutofautisha vyama vya upinzani na chama tawala kwasababu ya Viongozi wao kuwa machawa wa Rais nazungumza hili kwa uhalisia uliopo sasa. Lakini nina mashaka ndani ya hii Siasa mapya inayoitwa Maridhiano. Je, inamjenga Rais au inabomoa Taasisi ya Urais na Rais mwenyewe Kisiasa kuelekea uchaguzi Mkuu wa 2025?

Hoja zangu ni hizi:

1. Rais amesahau kujishughulisha na hali ngumu ya Maisha kwa Wananchi na kupanda kwa gharama za maisha kwa ujumla.

2. Wale wapinzani wanaomsifia leo ndiyo hao kesho watasimama jukwaani na kupigia kelele hali ya Maisha yalivyo sasa.

3. Kuwakumbatia wapinzani ni sawa na kumkumbatia nyuki kwa maono ya kupata asali kiganjani.

Mimi nahisi Kama CCM wametafuta namna ya kumtoa Samia katika Siasa za ushindani ili iwe rahisi kwao kumuwekea kauzibe ugombea 2025.Mama Sasa anasifiwa anaupiga mwingi lakini wengi wanaomsifia ni Viongozi wa vyama vya Upinzani ambao kiidadi hawafiki hata 10 lakini rest ya Watanzania wenye sifa ya kupiga kura takribani M15-20wanalia na hali ngumu ya Maisha na upandaji wa Bei ya vitu kila uchwao na vilio kwasasa vimeongezeka zaidi na kuvuka mipaka.

Hadi uko ndani ya chama tawala hali siyo shwari.Wengi wanatamka hadharani hawamuelewi hata kidogo Bora hata JPM kila kitu ndani ya Nchi akishkiki Bei za vyakula,mzunguko wa biashara TRA wamekua kero na Watu wengi kwasasa wanafunga biashara kutokana na mlolongo wa Kodi zisizo na kichwa Wala miguu,kwa kifupi gharama za Maisha hazikamatiki Nchi inaendelea kukopa kwa kasi ya ajabu, umeme umekua kero Kubwa.

RASILIMALI za Nchi zinaliwa na kundi dogo la watu ndani ya Nchi Mama hata ajali yeye Yuko bize na Wapinzani na Sasa hili limekwenda mbali zaidi mbele za kamera za waandishi wanaomsifia Ila nyuma ya kamera wanatoa Siri na udhaifu mkubwa kuwahi kutokea wa serikali yetu tangu Uhuru katika awamu hii.

Ni Nani atanusuru huu mkatiko? Au Mama ameamua liwalo na liwe yeye 2025 hana haja Tena ya kugombea? Ukitizama kwa makini Mama maejichimbia kaburi lake mwenyewe Kisiasa kwani hao wanaomzunguka ndani ya chama ndiyo wanaofanikisha mipango yote ya kuhakikisha kwamba 2025 hagombei tena.

Mama anamalizwa kijasusi na hii slogan ya Maridhiano Bora angebaki njia kuu a deal na mfumuko wa Bei unaoendela Nchini biashara nyingi zinafungwa hali Ni tete Sana. Mwisho namuombea kwa Mwenyezi Mungu amuepushie hiki kikombe, Mungu Ibariki Tanzania.
Mkuu umeandika sana, Hongera. Maridhiano huwa hayana faida wala hasara kwa pande zote mbili. Kama wanandugu "WATANZANIA" wa chuki miongoni mwao na wakakubaliana wawe na "MARIDHIANO" basi tambua kuwa NURU imepatikana kwa wote. Kwa mtazamo wangu wewe nakuona huna haiba ya "maridhiano" hata ukikosana na ndugu zako hujutii na hauoni umuhimu wa maridhiano.
Tanzania sio ya kwanza, hata South Africa alikuwa na maridhiano.
Mkuu sioni sababu za kumjadiri Rais, umepotoka sana, Mungu akusamehe bure.
 
Mkuu umeandika sana, Hongera. Maridhiano huwa hayana faida wala hasara kwa pande zote mbili. Kama wanandugu "WATANZANIA" wa chuki miongoni mwao na wakakubaliana wawe na "MARIDHIANO" basi tambua kuwa NURU imepatikana kwa wote. Kwa mtazamo wangu wewe nakuona huna haiba ya "maridhiano" hata ukikosana na ndugu zako hujutii na hauoni umuhimu wa maridhiano.
Tanzania sio ya kwanza, hata South Africa alikuwa na maridhiano.
Mkuu sioni sababu za kumjadiri Rais, umepotoka sana, Mungu akusamehe bure.
 
Inawezekana; lakini 2025 akifikisha kura halali 35% amshukuru sana Mungu.

Opposition wana uhakika wa kura za wanachama wao, ccm kuna wanachama wengi wasiofurahishwa na yanayoendelea. Waite wahafidhina au jina lolote, sioni kama wanaweza kumpigia kura.
Nani kasema Rais anachaguliwa kwa kura zako? Ingekua kura zinaamuliwa na wananchi basi CCM ingeng'olewa 2010 na 2015 ingezikwa rasmi.

Samia akiamua kugombea hata asipopiga kampeni watamjazia masanduku business as usual.
 
Ni kweli kabisa.
1. Watanzania wanalia na tatizo la umeme, yeye yupo busy na maridhiano.

2. Watanzania wanalia na mfumuko wa bei, yeye yupo busy na maridhiano.

3. Watanzania wanalia na hali ngumu ya Maisha, yeye yupo busy na maridhiano.

Mama, Watanzania hawatashiba maridhiano. Watanzania wanataka hali bora ya Maisha.

RIP, JPM, BABA YETU MPENDWA.
Bado kuna mtu mwenye vihoja vya kishamba kama huyu?
 
Samia akiamua kugombea hata asipopiga kampeni watamjazia masanduku business as usual.
Hizo za kujazwa kwenye masanduku si kura halali. Nilichoandika ni kwamba akipata kura halali 35% amshukuru Mungu.
 
Hizo za kujazwa kwenye masanduku si kura halali. Nilichoandika ni kwamba akipata kura halali 35% amshukuru Mungu.
Ni lini CCM ilishinda kwa kura zote halali? JPM Ile 2015 hakufika hta 45% ila amekua Rais ndio sembuse Samia.
 
Ni lini CCM ilishinda kwa kura zote halali? JPM Ile 2015 hakufika hta 45% ila amekua Rais ndio sembuse Samia.
Sijui nitumie lugha gani! Sisemi kwamba 2025 mgombea wa ccm hatatangazwa mshindi, ninachosema ni kwamba pamoja na kutangazwa mshindi, hawezi kupata zaidi ya 35% ya kura halali.

Labda nitakuwa nimeeleweka.
 
Back
Top Bottom