Haya ndio maboresho ya Mtaala wa Elimu yanayoenda kufanyika Tanzania katika jitihada za kuboresha Elimu

hiyo hata marekani hakuna, secondary na high school no lazima,
 
lugha inabaki kama ilivyo sasa. nguvu inramuliwa iwepo kwenye ubora wa walimu na elimu. ila lugha ni kama sasa, govt kiswahili shule za msingi. ila naona kingereza kimepewa kipaumbele
 
Nimeona hapo et Coding..

Nimecheka sana Usiku huu, nani huyo wa kufundisha coding shule ipo Nyanchanyoko ndani ndani huko?

Alafu unakuta alieweka hilo wazo hata kuandika line moja iliyonyooka ya HTML hawezi..

Tuwe serious kidogo mipango mingiii utekelezaji sasa..
 
😂😂
Mkuu Huenda tukafika maana nasikia kwa Olevel na Advance wanaanza mwakani
 
Hamna kitu hapo kwanza kitu kinachodumaza elimu ya nchi hi iwe Haina thamani ni kukumbatia kiswahili

Na sijui Kwa Nini serikali inalazimisha kiswahili ndio iwe lugha ya kufundishia shule ya msingi

Hizo fani zilizowekwa hapo ni upuzi mtupu
Ufundi ambao ulitakiwa ufundishwe shule za msingi na secondary ni

Computer science
Electronics
Electrical
Graphics

Kijana akimaliza shule akiwa na ujuzi wa hivyo vitu Wala hapato taabu mtaani
 
😂😂
Mkuu Huenda tukafika maana nasikia kwa Olevel na Advance wanaanza mwakani
Sio rahisi.. huko Chuoni tu.. na kuna Comp Lab ila wahitimu wengi wanamaliza weupe.. leo hii Sekondari ya Mbagala Charambee ifundishe coding.. waalim wenyewe hawa hawa au wataajir kila shule Mtaalam wa Programming? Ni hectic
 
Wadau wa elimu wameshirikishwa katika maamuzi hayo?What we are seeing is the continued destruction of the education system na kuendelea kuingiza katika mitaala maudhui ambayo hayalengi kuboresha ufahamu wa msingi wa mwanafunzi,bali vitu hewa kama sanaa na michezo.

Sababu zinazotolewa za kupunguza madarasa Std.VIII to Std VII na sasa VI ni very flimsy.Mbona wenzetu Kenya na Uganda hawajapunguza,tuseme sisi ndio wajanja zaidi,I don't think think so.

Ukweli ni huu,upo mpango wa NWO wa kuzalisha wajinga kwa kuharibu elimu,ili waendelee kututawala na kuiba rasilimali zetu,na hili ndilo linaloendelea.Ukweli huu unaonekana kwa wahitimu wetu wa shule za msingi,sekendari na vyuo.Literally hawajui kitu,kwa kuwa mfumo wa kufundishia umeharibiwa kabisa,and there are no efforts at all being made to reverse the situation.Instead the destruction continues,as if the destruction that has already been done is not enough.Very sad indeed.

Why has this been possible,hivi sisi wenyewe hatuoni kinachoendelea?Ukweli ni huu,our state machinery is heavily infiltrated by the NWO Cabal,kwa hiyo hao mamluki ndio wanao amua kila kitu.Simply put it our government is "captured."
 
Sio rahisi.. huko Chuoni tu.. na kuna Comp Lab ila wahitimu wengi wanamaliza weupe.. leo hii Sekondari ya Mbagala Charambee ifundishe coding.. waalim wenyewe hawa hawa au wataajir kila shule Mtaalam wa Programming? Ni hectic
😂😂
kuna wakati huwa wanapanga hizi sera kufurahisha ila tuwape muda tuone..
Maana kwa Secondary wanaanza mwakani
 
Na umesikia implementation inaanza mwakani 2024 kwa Wanaoingia Form one
 
😂😂
kuna wakati huwa wanapanga hizi sera kufurahisha ila tuwape muda tuone..
Maana kwa Secondary wanaanza mwakani
Tuombe uhai..

Tatizo hawakusanyi ushauri kwa Wadau wanaojielewa. Waanzishe online poll pale system ichuje maoni bora na ambayo yapo rated.

Wakae chini na kusuka mikakati kwa phases.. hiyo ni transformation kubwa sana inahitaji muda na kugawa vitu kwa phases mbalimbali..

Najua mpk wanakuj kuimplement Computer language inakuwa sio marketable tena unakuta AI inagonga code fulll kbs ni ww kuingiza proposal yako na AI inakuchapia code..

Sasa hao wanafunzi unawafundisha coding then haina matumizi ki reality.. muda na tech vinasogea havisubiri mtu.
 
Hii elimu ya ufundi itakuwa nadharia? Nafikiria baadhi ya ufundi waliouandika hapo bila vitendo ni bure.
 
Katika vitu ambavyo watunga sera Bado hajatupeleka mbele ni kubaki kutumia lugha ya kufundishia kuwa ni kiswahili, badala ya English
I concur with you! Huu wa kutokuweka bayana lugha ya kufundishia ni upumbavu bado hatotatua tatizo kabisa! Yani bado wana ng’ang’ana na kiswahili lakini ukienda kwenye uhalisia kabisa lugha ya kingereza ndio inatumika mahali pote rasmi kuanzia mashuleni hadi vyuoni bila kusahau kwenye kutoa huduma na pia kwenye usaili!

Huu mtaala ni bure kabisa kama bado lugha ya kufundishia itabaki kiswahili halafu wanafunzi wakifika juu wanaanza kuteswa na kingereza…Huu ni upumbavu tuu…
 
lugha inabaki kama ilivyo sasa. nguvu inramuliwa iwepo kwenye ubora wa walimu na elimu. ila lugha ni kama sasa, govt kiswahili shule za msingi. ila naona kingereza kimepewa kipaumbele
Ni vyema tuchague moja ni lugha gani ya kufundishia na yenye manufaa? Yani kiswahili hiki kinampeleka wapi mwanao? Kina manufaa makubwa zaidi ya kingereza kama tutaendelea kukitumia kufundishia? Kiswahili kina matumizi makubwa kwenye maisha yetu kuliko kingereza? Lugha yetu rasmi kwenye shughuli za serikali kitaifa na kimataifa ni ipi? Na kwanini ni lugha hiyo? Lugha ambayo inatumika kwenye kila shuguli hata tukichangamana na wengine kwanini isiwe lugha ya kufundishia hiyo?
 
Hii nchi ina watunga sera mazuzu na wapumbavu,kwenye huo mtaala Kuna mambo ya kijinga na upumbavu.Nitabainisha machache.

Mosi,Lugha bila kupepesa macho kiingereza kinapaswa kuwa Lugha ya kufundushia kuanzia shule ya msingi,sio kama ilivyo wekwa hapo.

Pili,Dini unafundisha masomo ya dini,mashuleni ili ugundue nini hasa,huu upumbavu wa kuanza kulishana itikadi utakuja kuleta shida uko mbele.

Tatu,Historia ya Tanzania hili SoMo litajaa siasa za hovyo za nchi hii za kusifu viongozi kama miungu watu.
 
Mkuu kiingereza ndio msingi wa maarifa mengi na hii ni kutokana na kuwa na Literatures nyingi,jambo ambalo watu wengi hawafaham ni kwamba kukua kwa Lugha huenda sambamba na kukua kwa mawazo (fikra) kwa sababu fikra mpya au mawazo mapya lazima yapate misamiati ya kukamata hayo mawazo na hapo ndipo Kiswahili kinapo feli,mfano neno Ethics na Moral,katika Kiswahili hupewa maana Sawa kitu ambacho sio Sawa,lakini Kiswahili phone hawalioni hili kama tatizo.
 
Ovyo sana! Kwa maandalizi gani waliyofanya? Hizo elimu za ufundi zinahitaji nyezo, waalimu (wabobezi) wa hizo taaluma.
Tuna walimu wangapi wenye uwezo wa kutosha shule zote?
Hapo sijaelewa kwa kweli!
Hili taifa kila jambo ni siasa mpaka kwenye mambo ya msingi kama elimu,afya nk.shule za kata tu zina miundombinu mibaya na hovyo,sasa mambo ya karakana za kisasa yatawezekana kweli ?

Somo la historia ya Tanzania ilikuwa utashi wa mtu mmoja,lakini watu wamefanya agenda ya watu wote,yaani siasa kwa kila jambo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…