Haya ndio Mapinduzi ya Zanzibar, yamerikodiwa live na waitaliano 1964

Nimeipenda hiyo ya mwisho Okello alipo ulizwa swali kajifunzia wapi ujeshi na jibu alilowapa...jamaa anajeri sana na jasiri. Ninasikitika kwa nini historia hizi zimefichwa kwa faida ya nani huku tukilishwa matangopli shuleni

By the way Mohammed Babu anaonekana kabisa alilikuwa njema kuliko hata huyo Aman Karune. Lakini mashule tumekalilishwa kuwa Karume tu!!!!
 
...kaka we una chuki na watanganyika na ni chuki ambayo itaishia kukupakijiba moyoni....hivi ni siri kwamba waafrika na washirazi walifanya mapinduzi? hivi ni siri kwamba umma party ilikuwa na makada wengi ambao walikuwa wamepewa mafunzo cuba kwa ajili ya kuja kuikomboa nchi yao na kuifanya cuba ya afrika masahariki? kwa nini wazanzibar wengi walioupenda usultani wa kiarabu wasingempigania sultani na kuzuia mauaji ya raia wasio na hatia yaliyokuwa yakifanywa na kama unavyodai 'watanganyika'? hivi, kinasaidi abdallah natepe. mohamed babu na wenzao walikuwa ni watanganyika? okello alikuwa mtanganyika? washirazi na waafrika wakiupenda usultani, na wakitendewa haki?....pamoja na hayo, mauaji ya watu ambao hawakuwa na hatia yanasikitisha na hayakustahili...laiti yasingetokea....! lkn wenye kuamini ktk uislam tunasoma ktk qur'an 8;25..."na iogopeni adhabu ya allah (ya hapa duniani) ambayo haitawasibu peke yao wale waliodhulumu nafsi zao miongoni mwenu; na jueni ya kuwa allah ni mkali wa kuadhibu..".....ukoloni ni ukoloni..na dhambi zake ni zile zile..!..mungu awarehem wale wote ambao walidhulumiwa nafsi zao ktk matukio na harakati za kuung'oa ukoloni na dhulma zake ktk kila kona ya afrika na palestina ,......
 


Yaah! hakika ni uchambuzi mzuri, inawezekana ni CINEMA, je na hawa JOHN OKELO, ABEDI AMANI KARUME na MOHAMED BABU, PIA NI CENEMA. Je tunahoja za kuwakana hao. Wasi wasi ndio Akili. Sipingi uchambuzi huu (OBSERVATIONS). Ila tusiwe washabiki, kama ni changa la Macho, tulijadili kwa Maslahi ya Vizazi vijavyo.
 

uloyasema hapa ni kweli tupu 100%.

hata leo znaizbar hatuoni raha kutawaliwa na tanganyika na hili tunalitizamia njia ya kulimaliza pia.

Lakin iinakupasa ujuwe kwamba kuanzia mwaka 650 AD warabu tayari wamefika zanzibar. Na vitabu vipo ziloandika juu ya hilo

Hakuna mtu leo anayethubu kusema znzn ni ya wafrika. Mimi binafsi ninaamini kwamba hakuna mtanganyika alokuwa na sababu ya kuja znz katik amiaka ya 1800s, isipokuwa wale walioletwa.

watu walisafiri sababu ya shida za maisha na huko tanganyika kulikuwa kuko poa sana, wanyama na mazao yalikuwa yanawatosha wenyeji wa huko siku hizo, yaani yata watu kusini hawakuwa na sababu ya kwenda kaskazini

kwa mtazamo huo mwarabu alipokuwa zanzibar alikuwa yupo nyubani kwao kabisa.
 
...kaka historia inatufundisha kuwa miongoni mwa wakoloni waliokutana mwaka 1884 huko berlin ujerumani ili kugawana afrika sultan wa oman alikuwa mmojawapo....!yeye alipewa viswa vya zanzibar na kilomita kumi za mraba kutoka pwani kwenda bara..! ktk pwani yote ya afrika mashariki..! ..ni mkoloni alikuwa...!suala la kutokuwepo muafrika ktk zanzibar ni upotoshaji mwingine wa historia ambao sasa unafanywa zaidi na washabiki wa usultani wa kiarabu ktk zanzibar..!na labda nikuulize..nani alitangulia kufika zanzibar kati ya mashiraz wa uajemi na waarabu wa kioman? vp waarabu wa kiyemen? unajua ni kwa nini pamoja na zanzibar kuwa chini ya sultan ambae anatoka nchi ambayo ni waislam wa dhehb la ibaadh, lkn wengi wa watu wake toka siku hizo ni ordhodox muslims kama walivyo waumini wengi wa bara?......tuache hayo..mi ni mzanzibar pia..! lkn ni ukoloni upi wa bara ktk zanzibar? naam..! kuna matatizo na kero ktk muungano wetu..lakini ukoloni kwa tafsiri halisi ya ukoloni ni upi? weka chuki ya uafrika pembeni..weka mapenzi yaliyokithiri ya uarabu pembeni...karibu tujadiliane..sisi ni ndugu..kama si kiimani, alhamdullillah, huwezi jua...wazee wetu walikuwa si haba ...lol..labda babu zetu ni ndugu..karibu..!
 
RED Xs


Kwanza sio kweli kwamba washirazi walifanya mapinduzi, washirazi ijapokuwa wanajisema wao ndio wenyeji wa znz lakini kabila lao linatokea Persia, irani ya siku hizi katika mji uitwao Shiraz. Hassan Bin Ali alikuja na watoto wake 7 wakaanzisha Zenj Empire ya kwanza, znz hapukuwa na maisha rasmi, wao wakapafanya ndio kituo chao kuchukuwa maji na mapuumziko kidogo kidogo ndio pakawa na life.

Kwahivo mshiraji na mwarabu sio watu mabli sana, wao hawakushiriki katika mapinduzi

Mapinduzi yalifanywa na watanganyijka, na ikiwa kwa ukweli huu unananihisi mimi ninakuchukieni basi ndio ninakuchukieni kwa kuivamia nchi yetu na kutuulia jamaa zetu kiholela.

wewe utafurahi kama sisi wazanzibar tutakuja tabora au iringa au popote huko tanganyika na kukuuweni kiholela? Jee kwa hilo utatupenda sisi wazanzibari?? be honest pleae!!!!!!
 

Mkuu minashindwa kuelewa nikigezo gani kilicho pelekea karume (asie msomi) kukabidhiwa nchi badala ya Babu alie msomi? Ikiwa hata ngeli ya ugoko tu alikua hana? Kumbe hili tatizo la nchi kuongozwa na vilaza halikuanza leo
 
Kitoabu

Mkuu minashindwa kuelewa nikigezo gani kilicho pelekea karume (asie msomi) kukabidhiwa nchi badala ya Babu alie msomi? Ikiwa hata ngeli ya ugoko tu alikua hana? Kumbe hili tatizo la nchi kuongozwa na vilaza halikuanza leo

Kiongozi hapa umekuja na hoja muruwa kabisa....

Lakini kumbuka Umma party sio waliofanya mapinduzi, Babu na Salim ahmed salim hata iwe vipi na wao walionekana ni waarabu katika macho ya ASP

Labda Abdullah Kassim hanga aliekuwa Prime Minister wa SMZ angepewa nafasi ya karume. Kassim Hanga alikuwa msomi mzuri sana pia. lakini badala yake alikufa katika mazingira ya kiajabu na kaburi lake halijulikani lipo wapi. wengi ndani ya ASP wanasema alifungwa mawe na kutumbukwiza chumbe.

Aboud Jumbe alikuwa msomi pia na alisoma pampja na nyerere huko makerere. Pia yeye alikuwa na uzoefu katika uongozi ndani ya serikali halali ya zannzibar alikuwa asifa mkubwa katika wizara ya elimu bado nyaraka zipo za mishahara yake. Jumbe akapewa uwaziri ndani ya SMZ hatimae raisi wapili baada kuuwawa kwa karume

mshahara wa jumbe siku za sultan


au hata mzee mwinyi alikuwa na yeye yumo ndani ya ASP msomi na alikuwa akifanya kazi na Mzee Jumbe huko huko wizara ya elimu ya sultan na yeye akaonekana hafai kwasabau ni msomi, akapewa uraisi baadae.

msharaha wa mwinyi siku za sultan


Jumbe na Mwinyi walikuwa ni wale walioitwa wazanizbara, kwahivo walikuwa na sifa ya kupewa uraisi wa serkali ya mapinduzi ya zanzibar in 1964, badala ya karume. Lakini waloyaunda mapinduzi hawakuta msomi kuwa Raisi wa znz siku hizo.

Kusema ukweli siasa ya znz baada ya mapinduzi ni chafu zaidi ya biashara ya utumwa wanayosingiziwa waarabu znz
 


Wickama,

Nashukuru mno kwa mwaliko ndugu yangu. Nami nimo hapa nachungulia kiduchu.

Tafadhalini ndugu zanguni khasa kwa wale msoyajua mambo/maafa ya Zanzibar kwa utuvu...tupunguzeni japo kiduchu jazba na ile mentality ya kuegemea mno kwenye upuuzi wa Youtube,Google na Wikipedia.

Natumai wenzangu ni wasomi mlobobea kunishinda,sasa yawaje tena tunaumizana vichwa kwa kutumia vigezo/vielelezo vya kitoto!?

Insha Allah,kila nikipata fursa takua napita hapa jamvini kukuamkueni wenzangu.

Ahsanta.
 

Hizo propaganda ndio tulizosomeshwa shuleni kuwa warabu waliwanyansa na kuwafanya watumwa watu weusi lakini hiyo sio kesi ya zanizbar,watumwa walikuwa wanaletwa zanzibar kuuzwa tna waliokuwa wakikamata watumwa ni waafrika wenyewe kutoka na tafauti zao za makabila,hakuna mzanzibari aliyewahi kuwa mtumwa,wazanzibar ni watu waliochamnganya damu na wakabila mbali mbali ya afrika na nje ya afrika

Katika afrika mashariki na kati zanzibar ndio likuwa nchi yenye wafrika wasomi kuliko nchi yoyote katika ukanda huu wa Afrika,mafano angali hao akina babu,Hanga na wengineo,watu weusi wa zanzibar walikuwa wanamiliki ardhi walikuwa wamechanganya damu na famili za kisultani,kwaupi hao wanaotwa masultani walikuwa ni machotara wakiarabu waliochanganyika na wamanyema

kama hayo unayoyasema kuhusu utawala Jemshid ni kweli mbona akina karume wameishi mpaka wakuwa maraisi,moja katika mahojiano na mke wa Karume aliwahi kusema kuwa karume alikuwa anapinga mapinduzi,sasa jiulize kwanini Karume alikuwa anapinga mapinduzi kama utawala wa jemshid ulikuwa wa kinayama?Uongo huo haufanyi kazi tena katika karne hii ya "Information technology" kila kitu kiko wazi

Hayo uliyoyasema kuhusu udhalimu wa utawala wa Jemshid kuwatesa na kuwakamata watu ndio tunayoyaona sasa kati ya utawala wa CCM na wapinzani je serikali ya CCM nayo ipinduliwe wanachama wa CCM wauliwe kama kuku!!!!? au unataka kuniambia wapinzania hawakatwi na kuteswa na utawala tuliona sasa!!!? tafakari

Kuuwa ni dhambi,kuuwa watu walikuwa hawana hatia ni kufuru na dhambiMapinduzi ya zanzibar yalikuwa ni "Genocide"
 

mimi tangu nipo darasa la kwanza hadi for 6, walikuwa wakinipa propaganda hizo hizo waarabu wabaya, walikuwa wakituuwa wakituchinja ..kwanza kama watoto wengine niliwaamini baaade nikaanza kuona kumbe wanatuulia hot air tu hawana la kusomesha

Kama waarabu walikuwa wabaya na madhalimu nimeweka katika makala moja humu mishahara ya Malim aboud Jumbe na Maalim Ali Hassan Mwinyi. Hawa na wengine kama hawa walikuwa na nafasi kubwa tu serikalini.

Lakini kuna watu bado wanatumia siasa za divide and rule zanzibar

Ukimuona mwana CCM anapanda kiriri na kuanza kutukana waarabu ujuwe anatafuta mkono uende kinywani tu, ni njaa tu zinazowasumbuwa hawa.

walipoambiwa wasome walikataa sasa wanasema waarabu hawakuwasomesha waafrika, lakini maajabu zaidi hao yanaosema ni wamkuu ambao siku zao za skuli serikali ilikuwa ya mapinduzi, ukiwauliza kwanini nyinyi hamukusoma jawabu ni kwamba tulikwenda kuvua vibua au kupanda minazi.
 
Nina swali kabla sijaenda mbele zaidi: Waitaliano walishiriki katika mapinduzi ya Zanzibar?

Makala Jr,

hakuna dalili ya dhairi kwamba wataliana walishiriki, lakini behind the scenes sijui, ingawaje nijuwalo ni kwamba wataliana walikuwa ni interest kubwa huko tanganyika kwa kupitia kanisa lao

isipokuwa kuna swala zima hapa inapaswa tujiulize kwanini na wao washiriki katika kuyarikodi mapinduzi au mauwaji ya 1964 huko znz, ingawaje kwa hili hatuwezi kusema walishiriki moja kwa moja
 
Nina Swali kidogo kwako Bin Faza, mimi ni Kijana kama ujuavyo tunajifunza historia nyingine shuleni hafu tunakuja kujifunza wenyewe Historia nyingine, unadhani kwa nini Karume aliuwawa?
 

Haaaa haaa! Haya mafundisho kwamba Mtanganyika aliua Wazanzibari ni ya Gaidi Sheikh Ilunga! Kama mwanaume mbona kaikimbia nchi?
 


Chabuso.

Salaam. Nimeisoma bayana yako kwa utuvu mwingi.

Lakini kwa mtazamo wangu nakhis umechanganya khabar/History nyingi kwa pamoja!?

Kwanini sisi tusijikite mno tu kuanzia pale 1961 onwards!? Nakhis hii itarakhisisha hoja/mazungumzo yetu na kufanza iwe wepesi kufahamiana kwa utuvu baina yetu wanajamvi!?

Nimeshtushwa kiduchu pale uliponena yakuwa ati hakuna Mzanzibary alowahi kuwa mtumwa!?...hii History Sheikh wangu unaianzia tangia mwaka/karne ipi!?

Kama Waarabu waliwahi kufanzana watumwa baina ya makabila ya wao kwa wao,sasa kipi tena ati ndo kiwazuie pale walipofika Unguja/Zanzibar ndio ati waache/wasitishe zile dasturi zao za kinyama na umaluuni!?

Huu unyama na udhalimu umefanzwa na makabila/jumuia takriban zoote duniani na mpaka kesho haya majambo yanaendela kwingi mno duniani.

Tunajua yakuwa hata Wazungu nao walianza kufanziana utumwa na udhalimu mwingi mno baina yao hata kabla hawajaanza kufikiria kufika/kuja Afrika.

Pia tuna mifano ya India,China,Mongols na mpaka hivi karibuni ki-Historia vituko vya Oliver cromwell kwa Ma-Irish!?

Waafrika nao hawakuwa nyuma asilan katika kufanziana utumwa na udhalimu uso mipaka kabla hata yakuwa influenced na hao Waarabu au Wazungu. Tutazame pia kiundani unyama,utumwa na uharamia ulo kubuhu alokua akifanza Kabaka,MwanaMutapa na Chaka Zulu dhidi ya watu weusi wenzao kwa miaka mingi mno,tena wala sio centuries nyingi zilizopita!?

Angalia wale freed Slaves nao ule uharamia,unyama na utumwa waliowafanyia watu weusi/Waafrika wenzao pale Liberia - The freed land!? Inasemekana na ushahidi mwingi wa kina upo,yakuwa mambo walofanza wale Afrikan Amerikans (waliojikhis light/fair skinned) dhidi ya ndugu zao natives Afrikans...hayakuwahi kufanzwa hata na hao manguli wa utumwa na udhalim Wazungu!?

Tukumbuke hivi vituko na unyama huo ndo mpaka kesho bado unaendela na umeacha makovu makubwa katika History ya pale Liberia maskini!

Labda nakuunga mkono tu pale uliposema yakuwa History ya Tanganyika/Tanzania,imepindishwa mno kiasi ya kwamba wasomi/Watanzania wengi wamekua mapunguani wa maarifa.

Nina maana yakuwa Ilm/History;imejazwa chuki ,hasama,fitna,uzandik falsifications and fraudulently claims...ili kuwapendezesha Wazungu(the so called Orientalists) na propagandas zao.
Hii inawasaidia mno Wazungu ati waonekane wao walikua ni "wavumbuzi" na "Missionaries" tu,na walikua wastaarabu na watu wazuri mno kwa watu weusi/Waafrika na wao ndo walokataza biashara ya Utumwa na kuhama makwao kwa ajili tu ya kuja Afrika kuleta maendeleo!?

Wakti huohuo imeenezwa/inaenezwa chuki nyingi mno dhidi ya Waarabu na myths nyingi mno zinasomeshwa kwenye ma-Skuli/Shule zetu na huku Serikali ikifumbia macho kwa miaka mingi mno.

Nafikiri matokeo yake ndo utaona hata hapa Jf,unajadilina na mwanajamvi mwenzio kiundani tena huku wewe ukidhani ni msomi/mtaalamu mahiri...lakini inapokuja kwenye History ya nchi yetu au hata Afrika,utagundua udhaifu na chuki nyingi mno with loads of colonial connotations...kiasi hata waeza kujiuliza hivi kweli nazungumza na Mtanzania/Mwafrika mwenzangu hapa au maluuni fulani tu wa Kizungu!?

Niwie radhi ndugu yangu,kama kuna lolote labda unakhis sijui/nimekosea au nimenena nawe hukupendezwa nalo!?

Ahsanta sana.
 

Mkuu kinachosumbua hapa ni ubaguzi wa waarabu dhidi ya weusi!
 
Haaaa haaa! Haya mafundisho kwamba Mtanganyika aliua Wazanzibari ni ya Gaidi Sheikh Ilunga! Kama mwanaume mbona kaikimbia nchi?

Huna hoja wala una jipya jenga hoja za mapinduzi ya zanzibar kama unazo siyo kuleta viroja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…