Haya ndio Mapinduzi ya Zanzibar, yamerikodiwa live na waitaliano 1964

propaganda za siasa za Tanzania zimeadvance,mngetumia huu muda na akili kuwaletea maendeleo watanzania tungekuwa mbali
 

Kaka hujakosea chochote hapa tuko kwa kuelimishana,hapa najaribu kuelezaea uhalisia kuhusu zanzibar na enzi zake ninavyouona mimi na sio jengine,nitakurejesha nyuma kidogo tu zanzibar ilipoungana na tanganyika zanzibar ilkuwa na watu takriban laki tatu(300,000),sasa tafuta jibu Dr Livingstone alipotangaza kuondoshwa kwa utumwa katika miaka ya 1800s, je zanzibar ilikuwa na watu wangapi?

jibu la haraka labda kulikuwa na wazanzibari 20,000 hiyo ukifanya thathmini kuwa zanzibar hivi sasa kuna watu millioni moja na nusu(1,500,000),amini usiamini hakuna mzanzibari aliewahi kuwa mtumwa,walikuwepo wazanzibar waliokuwa wanamiliki watumwa walikuwa wanafanaya biashara ya kuuza watumwa akina Tiptip na wenzake.

Wakati huo wa utumwa kama polulation ya zanzibar ilkuwa kidogo hivyo haiwezekani kuwa wazanzibar walikua watumwa la si hivyo wazanzibar wote waliuwa watumwa,Watumwa alikuwa wanaletwa zanzibar kuuzwa kama bidhaa nyengine yoyote ile,wanauzwa wanapakiwa kwenye jahazi wanasafirishwa wanakosafirishwa,mfano kama gari zinavyouzwa Dubai lakini hakuna kiwanda cha gari Dubai,ofcouse is a shame history lakini thats how happened

Kumbuka kaka History imeandikwa na watu kuna walioiposha na kuna waliosema ukweli,kuhusu history ya zanzibar kuna watu wanavutia kwenye uarabu na kuna watu wanavutia kweye uafrika mimi najaribu kuwa "neutral" najaribu kuvutia uzanzibari, karne hii tulionayo ya "information technology "history unaweza kuiandika mwenyewe ingia kwenye google utapata kila kitu
 
Mkuu kinachosumbua hapa ni ubaguzi wa waarabu dhidi ya weusi!


Ubaguzi upi huo wa Waarabu dhidi ya hao watu unaodai yakuwa ni "Weusi"!?

Kwani wewe hujui huko mabara/Tanganyika mpaka kesho, hao watu unaodai yakuwa ni "weusi" wanachinjana na kuuwana kwa kugombania ng'ombe na migomba!?...sasa kuna Mwarabu pale!?

Mpaka kesho hujui yakuwa jamaa zenu Wahaya na wengineo wanavyowadharau na kuwabeza Waswahili yakuwa ni wapuuzi,wavivu na hawajasoma!?

Sina haja ya kutaja mengi kuhusu Wachaga dhidi ya Wagogo na mengineyo mengi mno!?

Pale Zanzibar/Unguja yoote,tangia enzi ya Sultan watu woote walikua na maingiliano na tolerance ya hali ya juu kuliko hata hiyo Tanganyika,Amerika na sehemu nyingi mno za dunia!

Kumbuka tangia wakti huo wa Sultan hapohapo Zanzibar Waswahili/Wazanzibary wa matabaka tafauti walikua wakioleana na Wazanzibary wengine waliokua na asili ya ki-Persia,Bengalis,Arabs,Chinese,Indians/Pakistanis,Goans na wengineo.

Sasa hapo Tanganyika,kwa matabaka na ubaguzi ulokubuhu mpaka kesho...hivi unafikiri kuna mtu gani leo hii anaweza kutoka Kilwa na kuthubutu kupeleka posa yake Marangu!?

Niambie kuna Mgogo gani kutoka Mpwapwa leo hii anaweza kuthubutu kukubaliwa posa yake kwenye family ya Wahaya wa Ngara au Kamachumu!?

Hivi vitu hata kama vipo,itakua ni nadra mno...I mean rare cases/coincidences tu!

Kwa kifupi hizi stereotypes/prejudices ni udhaifu tu wa kila mwanadamu,lakini kinachogomba zaidi ni ile degree ya yayo inapotamalaki!

Kwa hivyo, hiyo issue ati yakuwa Waarabu ndo wao tu peke yao,wamefanza au wanafanza mambo/udhalim exceptional nakhis haina mwelekeo wenye kukubalika ki-Historia wala kitaaluma.
 

Bila shaka matatizo yalikuwepo,tafauti zilikuwepo,kwani huu wakati tulio nao hatuna tafauti miongoni mwetu,Kulikuwa hakuna ubaguzi kama wanavyoueleza hawa watu wa mapinduzi,wazanzibari wengi hawakuwapeleka watoto wao shule kwa imani kuwa kufanya hivyo ni kinyume cha uislam,cha kujiuliza Hao akina Karume,Hassan Nassor Moyo,Aboud Jumbe Mwinyi,Ali hassan Mwinyi wao walisoma wakati gani?mpaka kufikia kuwa na nyazifa kubwa kubwa kwenye serikali ya sultan
 


Chabuso,

Haina neno ndugu yangu. Natanguliza shukran zangu za dhati

Nakusoma kwa utuvu,pia nafuatilia bayana zako kwa utuvu.

Hiyo khabar ya wingi wa watu/sensa hapo Zanzibar...kuna khabar za kuthibitisha zaidi yakuwa Zanzibar wakti ilipokua himaya kubwa zaidi centuries nyingi zilizopita pia ndo ilipokua na watu wengi/population kubwa zaidi.

Population ya Zanzibar ilianza kuporomoka zaidi pale ile himaya ya Sultan ilipoanza kudhofu kwa fitna za Wazungu khasa Waingereza.

Nafikiri hatuna haja ya kuleta malumbano mengi,nami nakubaliana nawe yakuwa tumo hapa kujifunza soote kwa pamoja.

Naomba kukuuliza suali kiduchu,kama hutojali...je wewe watokea ndugu yangu Unguja/Zanzibar!?

Mimi nina watu/Wazanzibary nilowahi kuwaona kwa macho yangu binafsi ambao waliwahi kuwa Watumwa pale Unguja enzi za Sultan!?

Majina yao ninayo kibindoni mpaka kesho,na mpaka makaburi yao walipozikwa pale Unguja nayajua!

Labda tukubaliane yakuwa,tuna tafsiri tafauti yakuwa Mzanzibary khasa ni nani,na je Utumwa nao khasa ni nini!?

Au matendo gani/yepi yenye kuhalalisha mtu a-qualify kuitwa Mtumwa!?

Nafikiri hizi ni hoja zenye kuhitaji uchambuzi wa kina na unyambulisho wa kitaaluma!?

Ahsanta.
 
Hivi kama kweli mapinduzi yameleta uhuru kwa waz'br mbona hawapo huru kujiamulia mambo yao na kila kitu wanapangiwa kutoka dodoma?ni wazi wakoloni weusi hutumia silaha ya kutubagua kwa rangi zetu ili waitawale zanzbr,ukoloni wao hauna nafasi tena kwani wazbr wamesha jielewa,zanzbr kwanza.
 
gombesugu

Mimi nina watu/Wazanzibary nilowahi kuwaona kwa macho yangu binafsi ambao waliwahi kuwa Watumwa pale Unguja enzi za Sultan!?

Mkuu

hii yako ya leo kali kidogo, tumewasikia watanganyika wakimapaka matapo sulatan wa zanzibar kwa kila aina lakini hii nadhani unastahiki nobel prize mzee

inavojulikana kimataifa ni kwamba utumwa ulifutwa zanzibar rasmi katika 1886 -1896

sasa hao watumwa unawajuwa wewe waliokuwa zanzibar enzi za sultan iyupi tabidi tukuulize vyema yafuatayo

1. wewe umewahi kufika zanzibar, au uliogopa kwenda huko usije ukafanywa mtumwa?

2. Sultani gani na wamwaka gani huyo alokuwa ndani ya utawala wake kuna watumwa unaowajuwa wewe kw amajina namakubiri yao?

3. Jee unaouthibitisho ya kuwa watu hao walikuwa watumwa?

4. Jee hujichanganyi katika kumbambanuwa baina ya watumwa na watumishi? maana hapa zanzibar wapo hadi leo hii watumishi wa majumbani kutoka tanganyika, wakulima wa mashamba na watumishi wa aina nyengine lakini sio watumwa ni watumishi.
 
Ikiwa wewe huna asili ya kiarabu au ya kishiraz,lazima utakuwa una Asili ya Tanganyika,kama ww ni mwafrika mweusi.
Na pia jiulize,waarabu walikuwako Tanganyika,miaka mingi kabla hata utawala wa waarabu Zanzibar,mbona waarabu hawa wa Tanganyika,hawajauliwa,hawajateswa,hawajanyanyaswa,mpaka leo wapoTanganyika,na tena idadi ya Waarabu waliopo Tanganyika,wenye asili ya Oman,ni mara kumi na zaidi waliopo Pemba na Unguja.
Pale panapsemwa kuna historia kubwa baina ya Oman na Tanganyika,ufahamu kuna sehemu,Tanganyika ukifika utakuta waarabu ni wengi kuliko hata wenyeji kwa miaka hiyo nampaka sasa,Jiulize sasa kwa nini waarabu hawa Wa Tanganyika,ambao ni wengi kuliko wa Zanzibar,waishi kwa Amani.Lakini Watanganyika hao hao wanaodaiwa kuwauwa waarabu wa Zanzibar,hawakuwauwa,waarabu wa Tanganyika,na wapo waarabu waliokimbilia Tanganyika Toka Zanzibar,akiwemo huyo Sultani wa Zanzibar,kwa nini hakupata madhara yoyote alipokimbilia Tanganyika,kabla ya kwenda Ungereza.
 

Naongea na mwenye mbwa siongei na mbwa.

Kwani kufungwa kwa uzi wetu leo ndiyo siku ya kwanza mbona kawaida uzi zetu kufungwa, wewe umeonya nani humu JF zaidi ya mnafiki tu kauzu wewe.
 
Kikwajuni one


kwanza kabisa ujuwe mimi sikubali kulizimishwa katika ubaguzi, mimi nikiwa muarabu, muhindi,mchina, mswahili hapa zanzibar ninajihisi ni mzanzibari halisi.

lakini kukujibu swala lako tu ni kwamba waarbu walioko tanganyika labda ni wengi kama unavodai lakini huko hawakufanya serikali. walikuwa na mado wanabakisha kuwa raia wa kawaida tu.

Waarabu waliokuwepo zanizbar walifanya serikali ndio hiyo munayopenda kuiita serikali ya sultan. kwahivo akina nyerere na watanganyika wenzake wakitumiliwa na wazungu walitaka kufanya kile kiitwacho ethnic cleansing ili waarabu wasije wakatawa tena huko.ndio maana wakakimbilia kufany amuungano mara tu baada ya mapinduzi ili kuhakikisha sultan harejei tena

nadhani nimekujibu
 

Wewe acha unafiki hebu hapa jisome mwenyewe mabwana zako hawapo sijui utawaita kina nani.
Mnafiki ni chakula ya mamba, wewe kila siku na ulikuwa unatumia hizi hizi video kama ushahidi wa kumtetea bwana wenu Okello leo eti unasema ya kughushi.

Cc.. gombesugu, Boko haram,
 


Bin Faza,

Salaam.

Mimi nimezaliwa Unguja,tena ni Stone Town/Baghani...na nikifia pale Unguja abadan sitazikiwa Kwerekwe!...na wala sina asili/sitokei ng'ambo,je una jingine!?

Nafikiri ushanifahamu uzuri kama kweli wewe ni Muunguja!?

Unaponambia ati nitofautishe baina ya Mtumwa na House Boy...mie najua uzuri tafauti iliyopo,sijui wewe mwenzangu!?

Ndo maana,kwenye ile post/s yangu kwa ndugu yetu Chabuso, pia nikanena yakuwa wakti mwingine yatulazim kuangalia majambo kwa utuvu wa kina na kitaaluma.

Kwa mtazamo wako wewe Sheikh Bin Faza,Mzanzibary khasa ni nani!?

Na mtu yupi khasa ana-qualify kuitwa Mtumwa tangia zama hizo pale Unguja!?

Lakini penye nilijualo tazungumza japo kiduchu.

Nakufuatilia bayana zako leo takriban wiki kadhaa. Wallahi,wafanza uzuri mno kutufumbua macho wenzio.

Nafikiri unachoharibu kiduchu,ni vile unapojaribu kila mara kuonyesha yakuwa wale Waarabu/ma-Sultan walikua ni kama vile Malaika wakti wa utawala wao pale Zanzibar!?

Usinifanze nikashindwa kukutafautisha na hao jamaa zako wa ki-bara/Watanganyika humu Jf...maana na wao wanawaona Wazungu kama vile ni nusu Miungu na kuwaabudu mno huku wakichukia Waarabu bila ya sababu zozote za msingi!?


Ahsanta
kwa kunisikiza.
 
Wazanzibar wengi wanaamini kama Zanzibar katika afrika mashariki ndio ilikuwa kitovu cha biashara pekke yake.
Wakati kuna miji mingi ilikuwa kitovu cha biashara,
By the begining of the second millenium CE,THE SWAHILI towns conducted a thriving trade that linked the Africans in the interior with trade partners throughout the Indian Ocean.From c .1200 to 1500 ,the town of KILWA on Tanzania's southern coast ,was perhaps the wealthiest and most powerful of these towns,presiding over what some scholars consider the golden age of Swahili civilization.
 
In the early 14th century ,Ibn Batuta ,a Berber traveller from North Africa,visited Kilwa and proclaimed it one of the best cities in the world.Islam was practised on Swahili coast as early as the eighth or ninth century CE
 
Na wale weusi waliouawa, wakiwamo kina mama wajawazito waliotobolewa matumbo ili familia ya kisultani ione mtoto anavyokaa tumboni mbona hamuwagusi? Kina mama weusi waliobakwa vipi? Weusi waliohasiwa wakiwa njiani kupelekwa utumwani hawakuwa binadamu? Wanaume waliolawitiwa hawakuwa binadamu? Mnapoamua kujadili ubaya wa Mapinduzi ya mwaka 1964, jitahidi pia kujadili uonevu usio kifani waliofanyiwa weusi. Hapo mtakuwa mme-balance equation!!!
 

Kama waliouwa waarabu ni waTanganyika,basi hizo chuki zingeishia huko,zingefika mpaka huku,ila naweza kufikiria,japo sina uhakika,walioletwa Zanzibar kufanya mapinduzi,itakuwa ni wafanyakazi Wa Mashamba ya mkonge,waliokuwa wakiitwa manamba,ambao si Wa Tanganyika,ni watu kutoka Malawi,Rwanda na Burundi,walikuwako Tanga kwenye mashamba ya mkonge.Na watu hao ndio hao unaowaona huko Zanzibar mkiwaitwa wa Zanzibara,ambao pia wapo wamalawi,waburundi,wa Rwanda wamebakia huku Tanganyika.
Amini na nakufahamisha watu wa asili hasa wa Tanganyika,hawezi kufanya unyama huo,kama ingekuwa ni wao,wangewauwa pia waarabu wa huku,kwa sababu hata hao wananchi wa kiarabu wa Zanzibar waliouliwa hawakuwa watawala ni wananchi wa kawaida tu.
Hebu fanya uje Tanganyika,uone waarabu na wenyeji wa huku wanavyoishi kushinda hata ndugu wa tumbo moja.
 
 
Ritz huyu jamaa asikusumbue ana ugonjwa wa yule mjinga mwenzake Yericko unaitwa "amnesia" hasa kipindi hiki cha baridi ndio unawasumbua sana!
 
Yericko Yohana Msambila a.k.a "Yericko Nyerere".

Nakuona upo hapo chini...

Tafadhali nakusihi nenda ukanijibu yale masuali yangu nilikuoachia tangia jana kwenye ile thread yako.

Kama huna uwezo wa kujibu masuali ya Wanajamvi wenzio kwa kina,basi si uzuri kufungua thread/s na kujaza server/s humu Jf!?

Ahsanta sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…