Haya ndio maumivu au uchungu wa kifo unaompata mtu anayekufa 'Sakaratul-Mauti'

Wewe umewahi kufanya hivyo vitu na ukashuhudia au ume-hadithiwa na kukaririshwa maandishi tu?
Brother unajua wanasema ogopa vitu viwili moja MUNGU mbili teknolojia, sasa teknolojia inaongea ukweli km zifanyavyo CCTV camera hakuna CCTV camera inayosema UONGO, sasa wewe ugunduzi wa kifo umetumia teknolojia gani? Uliwaita majini wakuonyeshe?
 
Hiyo hadithi ni Uongo mtupu.

Mtu anapoanza Kufa ubongo unapoteza uwezo wake wa kufanya kazi. Hayo maumivu utayasikiaje?
Fikiria kwanza michakato iliyopitika hadi kupatikana huo ubongo, fikiria huyo mtu ametokea wapi? miezi 9 katika tumbo. Kabla ya hapo alikua wapi? miaka mingapi katika korodani? kabla ya hapo alikua wapi? alikua ni chakula na nafaka? au alikua wapi? nani kamleta hapa? je huyo aliyemtoa huko alikotoka hadi akamfisha anashindwa vipi kumrejesha? na kumpitisha katika hatua hizi za sakaratul-mauti? Ikiwa tu mwanaadamu mwenzako anaweza kukupa sindano ya usingizi na akakufanya atakavyo iweje MUNGU ashindwe kukupitisha atakapo?
 
Brother unajua wanasema ogopa vitu viwili moja MUNGU mbili teknolojia, sasa teknolojia inaongea ukweli km zifanyavyo CCTV camera hakuna CCTV camera inayosema UONGO, sasa wewe ugunduzi wa kifo umetumia teknolojia gani? Uliwaita majini wakuonyeshe?
Mimi nimekuuliza wewe swali? umewahi kushuhudia hiyo sayari ya MARS jibu ni ndio au hapana.
 
Hizi ni soga tu kama nyingine. Ukifa ndio bye bye hakuna cha maumivu wala moto wala mbingu. Story yako ndio inakuwa imefika ukomoni.
Mwenye kukanusha maisha baada ya kifo ni mpingaj wa MUNGU, Kukataa imani ya Akhera ni kukataa aina yoyote ya uwajibikaji. Watu kama hao hawaamini malipo au adhabu kwa matendo. Hapa hapa ulimwenguni tu, ukivunja sheria za jamii uanchukulia hatua. Iweje kuvunja sheria za aliyekuumba akuache hivihivi?
 
Mimi nimekuuliza wewe swali? umewahi kushuhudia hiyo sayari ya MARS jibu ni ndio au hapana.
Kwa kutumia teknolojia ndio inaweza kuonekana kupitia viona mbali hilo lipo wazi sasa wewe umeona wapi ulimwengu wa kifo kwamba mtu akitaka kufa anakua hivi na hivi na hivi umetumia vipimo gani au ni suala la Imani sio suala la kuonekana kwa macho yaani ni kiinimacho?
 
Kumbe kama hujawahi kuiyona hiyo MARS ila unaamini kwa kutumia teknolojia, basi nami ninaamini matukio hayo ya kifo kwa kupitia matamko ya Mwenyezi MUNGU ambaye amezileta hizo teknolojia duniani.
 

Kwa nini nifikirie nilipotoka?
Ukisema nifikirie nilipotoka ni endless question na haliwezi kuwa na jibu. Maana swali hilo halina jibu Kwa sababu litazaa swali jingine huyo aliyeniumba yeye alitoka wapi?
Kwa hiyo Hilo swali Kwa Watu wenye fikra Pana hawezi kuuliza swali ambalo ni endless, haliishi. Na kama watajiuliza basi watahitimisha kuwa Hakuna Mungu.

Kwa kukusaidia tuu, Mimi na wewe tulizaliwa Baada ya kuumbwa katika Matumbo ya Mama zetu. Hatukuwahi ku-exit popote pale.

Ni kama vile utengeneze Computer yenyewe uwezo wa kujichakata kiteknolojia Kwa namna ya reasoning, alafu ijiulize iltoka wapi. Jibu ni kuwa ilitengenezwa, ilikuwa wazo la mtu Fulani.

Mtu anapotaka Kufa Ubongo haufanyi Kazi vizuri Ila mwili ndio unahangaika labda Kwa kukosa hewa, damu, mshtuko, ubongo na moyo kujeruhiwa Kwa kiwango kisichowezekana kupona.

Mtu anapoumwa na Kupata maumivu Makali Ile ni ugonjwa au majeraha ambayo hayahusiani na kifo.
Wapo wanaoumia Sana lakini hawafi , na wapo wanaokufa bila maumivu aidha wakiwa wamelala au wakiwa wanacheka.
 
Kumbe kama hujawahi kuiyona hiyo MARS ila unaamini kwa kutumia teknolojia, basi nami ninaamini matukio hayo ya kifo kwa kupitia matamko ya Mwenyezi MUNGU ambaye amezileta hizo teknolojia duniani.

Mars inaonekana Kwa Kutumia vyombo.
Kasome Elimu ya anga.
Suala la sayansi sio ishu ya kuamini Bali ni ishu ya uthibitisho,

Huwezi sema unaamini Mars Ipo Wakati kitu kipo.
 
Kitu ambacho unatakiwa kujua Mtoa mada ni kuwa,
Vitisho havijawahi kuwafanya wanadamu wakawa na Upendo na Mungu.

Ili Watu wampende Mungu unapaswa uelezee mambo Mema na mazuri ya Mungu na sio kuwatisha kuwa sijui watachomolewa Roho zao vibaya.
Kwani Nani anajali huyo Mungu akichomoa hizo Roho iwe vibaya au vizuri? Who Care?
Kwani atapara nini akifanya hivyo?

Upendo haulazimishwi, kama Watu hawamtaki Mungu huwezi walazimisha, au huyo Mungu hawezi kuwalazisha na kuwapa adhabu kisa Watu hawampendi.

Huo ni ukatili na ushenzi.

Mungu ninayemjua Hana Sifa hizo za kijingajinga.
 
Mkuu, katika ulimwengu huu wa kawaida kila kitu kina cause and Effect, “nje” ya ulimwengu wa asili, Mungu hawezi kuthibitishwa wala kukanushwa na sayansi pekee. Ninyi mmekua mkitegemea sana Sayansi bila kujua wapi sayansi imetokea.

Ninyi mnakubali kuwa Hakuna uthibitisho wa kudumu wa kisayansi wa kuwako kwa Mungu. Kwa hiyo, katika suala la mtazamo wa ulimwengu unaotegemea tu ushahidi wa kisayansi, ikiwa Mungu yuko au la haijulikani.

Sisi Waislamu tunaamini kwamba Mungu ndiye muumba wa vitu vyote, na kwamba Mungu ni muweza wa yote na mjuzi wa yote. Mungu hana uzao, hana rangi, hana jinsia, hana mwili, na haathiriwi na sifa za maisha ya mwanadamu wala mazingira yake.
 
Mars inaonekana Kwa Kutumia vyombo.
Kasome Elimu ya anga.
Suala la sayansi sio ishu ya kuamini Bali ni ishu ya uthibitisho,

Huwezi sema unaamini Mars Ipo Wakati kitu kipo.
Kumbe MARS inaonekana kwa kutumia vyombo lakini hadi uwe na elimu ya anga, vipi unakanusha maisha baada ya kifo ilihali huna elimu ya IMANI. Umepata wapi hiyo nguvu? Yaani MARS huwezi kuiyona bila kutumia vyombo maalumu, lakini pia inabidi upite class kujifunza. Ujasiri wa kukanusha maisha baada ya kifo unaupata wapi ilihali hujapita Class la IMANI
 
MUNGU hataki umpende wala hana shida ya upendo wako, yeye ndiye anata akupende kwa wewe kutii amri zake. Sifa ya kupenda ni sifa ya Mwenye kumiliki nasio chenye kumilikiwa. Kwa hivyo ili MUNGU akupende lazima uwe mtiifu na mwenye heshima kwake, kisha yeye atakupa upendo wake. Kamwe ni ngumu kumpenda mtu jeuri, ila ni rahisi sana kumpenda mtu anaye kuheshimu na kukutii.
 
Urongo mtupu. Wewe uliwahi kufa ukashuhudia haya yote kisha ukarudi kuja kuandika? Au ni hekaya tu hizi?
 
Mars inaonekana bila hata vyombo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…