Haya ndio maumivu au uchungu wa kifo unaompata mtu anayekufa 'Sakaratul-Mauti'

Haya ndio maumivu au uchungu wa kifo unaompata mtu anayekufa 'Sakaratul-Mauti'

Hapa ndipo dini hukosea, Yaani mtu badala ufunze watu kutenda yaliyo mema ili kumtafuta Mungu... ila ninyi hutengeneza story kutisha watu na kufanya Mungu aonekane katili
 
Nyie wa You only live once mnachekesha sana, may my children not turn into such fools

images (2).jpeg
 
MUNGU hataki umpende wala hana shida ya upendo wako, yeye ndiye anata akupende kwa wewe kutii amri zake. Sifa ya kupenda ni sifa ya Mwenye kumiliki nasio chenye kumilikiwa. Kwa hivyo ili MUNGU akupende lazima uwe mtiifu na mwenye heshima kwake, kisha yeye atakupa upendo wake. Kamwe ni ngumu kumpenda mtu jeuri, ila ni rahisi sana kumpenda mtu anaye kuheshimu na kukutii.

Sio lazima kumtii Mungu kama moyo wako hautaki. Huo ni unafiki.

Mungu Mkuu sio mhitaji iweje ahitaji, atake, anapenda Watu wamtii ikiwa hawataki?

Hiyo unayoitaja ni sheria za miungu ambayo haina lolote.

Ninachokueleza ni kuwa, Mungu Mkuu Muumba WA hiyo miungu unayoitaja sheria zao hataki umtii wala umpende. Angetaka hivyo wala wewe usingeandika hii Porojo yako hapa, kwani Watu wote na viumbe wote automatically wangemtii na kumpenda.

Lakini yeye ndio hataki na hapendi, hiyo kutaka na kupenda ameachia miungu, na viumbe waliowaumba wao ndio wataamua watake au wasitake, wapende au wasipende.
 

1 Corinthians 2:14 NIV

The person without the Spirit does not accept the things that come from the Spirit of God but considers them foolishness, and cannot understand them because they are discerned only through the Spirit.

 
Limewasumbua nyinyi tu. Wengine halijawasumbua. Kwa nini useme kwa niaba ya dini nyingine wakati hauamini hizo dini wala haziamini mungu wako?
Kwa watu wengi wa kidini, imani ya uhai baada ya kifo inategemea mafundisho katika maandiko au mapokeo yao. Maandiko matakatifu katika Ukristo, Uyahudi na Uislamu yanazungumza juu ya maisha ya baada ya kifo - kwa hivyo kwa wafuasi wa imani hizi maisha baada ya kifo yameahidiwa na Mungu.
 
Kumbe MARS inaonekana kwa kutumia vyombo lakini hadi uwe na elimu ya anga, vipi unakanusha maisha baada ya kifo ilihali huna elimu ya IMANI. Umepata wapi hiyo nguvu? Yaani MARS huwezi kuiyona bila kutumia vyombo maalumu, lakini pia inabidi upite class kujifunza. Ujasiri wa kukanusha maisha baada ya kifo unaupata wapi ilihali hujapita Class la IMANI

Hakunaga Elimu ya Imani.
Unachoelezea wewe sio Elimu ya Imani. Bali unaelezea Elimu ya Dini Kwa jinsi Watu wanavyoamini.
Hakunaga Elimu ya Imani.

Imani inahusu Nafsi, hakujawahi kuwa na Elimu ya Nafsi kwenye huu Ulimwengu.

Kutunga Visasili(Myths) na kuigeuza kuwa kweli ndio ninapopingana na watu wenye Akili ndogo.
Ni Sawa na Mimi zile Stori zangu za kubuni hasa Visasili watokee Watu kama wewe wazisadiki waamini ni Elimu ya Imani. Ndicho unachokifanya
 
Kama Mungu anatupenda kweli angepambana na shetani yeye mwenyewe kuliko kutuachia msala sisi. alafu yeye akaenda kujificha
Hata pesa huiamuru ikifuate ni lazima uitafute, hata chakula hukiamuru kiingie tumboni ni lazima ukitafute na ukitafune ndio kiingie. MUNGU ahajakufanya wewe kama jiwe, kwasababu amekupa akili sasa lazima akupe kwa hatua za baadae. Hata mwanao utaanza kumlinda akiwa mdogo lakini akishapevuka utamuacha. Hizo ni kanuni ndogo za uwendeshaji wa mambo
 
Ukiachana na Imani kifo si mchezo nmeshuhudia vifo vingi ndo kitu pekee kinachofanya niamini kuna vitu vipo hatuvijui
SAKARATUL MAUTI naweza kusema ni pale ambapo brain inaanza kua deprived na oxygen hivo mtu anapata neurological deficits anaanza kuona watu wanaomtisha na ni kweli utaona mtu anaogopa anajificha
Kutoa haja si lazima ila ni common sababu bladder na njia ya nyuma ukiwa unakata roho kunakua hakuna innervation ya sphincter muscles zinazoshikilia
Ila kama marehem ataempty bladder punde kabla ajakata roho ni uncommon kujiokojolea
ALLAHU AALAM
Karibu sana
 
Unabishana na wansayansi ukiwa Kimara🤣🤣🤣🤣
Ndio mkuu, ndio maana tuko wazi kwasababu kinachokea hapa kinafahamika kinaga ubaga kuliko wewe uliyejificha ambaye huna uhakika wa hicho unachokitetea. Karibu Kimara Korogwe
 
Acha fix wewe. Huyo alikuumba wewe ulimuona wapi? Wadangaje wajinga wenzako mimi nishushe nimefika.
Uthibitisho wa kuwepo kwa Mungu Kila mtu huhisi ndani yake kwamba ana Bwana na Muumba, na anahisi kwamba anamhitaji. Muda wako wa kumuhitaji ukifika utamtafuta Boss
 
Mkuu, katika ulimwengu huu wa kawaida kila kitu kina cause and Effect, “nje” ya ulimwengu wa asili, Mungu hawezi kuthibitishwa wala kukanushwa na sayansi pekee. Ninyi mmekua mkitegemea sana Sayansi bila kujua wapi sayansi imetokea.

Ninyi mnakubali kuwa Hakuna uthibitisho wa kudumu wa kisayansi wa kuwako kwa Mungu. Kwa hiyo, katika suala la mtazamo wa ulimwengu unaotegemea tu ushahidi wa kisayansi, ikiwa Mungu yuko au la haijulikani.

Sisi Waislamu tunaamini kwamba Mungu ndiye muumba wa vitu vyote, na kwamba Mungu ni muweza wa yote na mjuzi wa yote. Mungu hana uzao, hana rangi, hana jinsia, hana mwili, na haathiriwi na sifa za maisha ya mwanadamu wala mazingira yake.
Ni dini mpya ya scientism, inaamini kuwa sayansi ina majibu ya kila kitu.
 
MUNGU hataki umpende wala hana shida ya upendo wako, yeye ndiye anata akupende kwa wewe kutii amri zake. Sifa ya kupenda ni sifa ya Mwenye kumiliki nasio chenye kumilikiwa. Kwa hivyo ili MUNGU akupende lazima uwe mtiifu na mwenye heshima kwake, kisha yeye atakupa upendo wake. Kamwe ni ngumu kumpenda mtu jeuri, ila ni rahisi sana kumpenda mtu anaye kuheshimu na kukutii.
Mwambie Mungu wako aende Yemen Sudan afugan Satan na Somalia Kuna watu Ni wanyenyekevu kwake na Wana mtii yeye na Sheria zake
 
Hapa ndipo dini hukosea, Yaani mtu badala ufunze watu kutenda yaliyo mema ili kumtafuta Mungu... ila ninyi hutengeneza story kutisha watu na kufanya Mungu aonekane katili
Ni kama vilevile majeshi hupiga mazoezi makali, kwa ajili ya kutishia watu na kutishia nchi jirani badala ya kuhimiza amani kwa watu wake.
Kila jambo lina hekima zake Boss. Hata mwanao anapokengeuka lazima umkumbushe kwamba kuna kesho.
 
Back
Top Bottom