Haya ndio maumivu au uchungu wa kifo unaompata mtu anayekufa 'Sakaratul-Mauti'

Haya ndio maumivu au uchungu wa kifo unaompata mtu anayekufa 'Sakaratul-Mauti'

Sio lazima kumtii Mungu kama moyo wako hautaki. Huo ni unafiki.

Mungu Mkuu sio mhitaji iweje ahitaji, atake, anapenda Watu wamtii ikiwa hawataki?

Hiyo unayoitaja ni sheria za miungu ambayo haina lolote.

Ninachokueleza ni kuwa, Mungu Mkuu Muumba WA hiyo miungu unayoitaja sheria zao hataki umtii wala umpende. Angetaka hivyo wala wewe usingeandika hii Porojo yako hapa, kwani Watu wote na viumbe wote automatically wangemtii na kumpenda.

Lakini yeye ndio hataki na hapendi, hiyo kutaka na kupenda ameachia miungu, na viumbe waliowaumba wao ndio wataamua watake au wasitake, wapende au wasipende.
Mwanaadamu sio kiumbe pekee wa MUNGU, yeye kaumba viumbe vingi kabla ya huyu mwanaadamu, na vipo viumbe vinamtii hadi sasa ikiwemo mwanaadamu mwenyewe, ispokuwa wachache walio potoka
 
Hakunaga Elimu ya Imani.
Unachoelezea wewe sio Elimu ya Imani. Bali unaelezea Elimu ya Dini Kwa jinsi Watu wanavyoamini.
Hakunaga Elimu ya Imani.

Imani inahusu Nafsi, hakujawahi kuwa na Elimu ya Nafsi kwenye huu Ulimwengu.

Kutunga Visasili(Myths) na kuigeuza kuwa kweli ndio ninapopingana na watu wenye Akili ndogo.
Ni Sawa na Mimi zile Stori zangu za kubuni hasa Visasili watokee Watu kama wewe wazisadiki waamini ni Elimu ya Imani. Ndicho unachokifanya
Kwetu sisi Wailsamu Imani ni kuwa na yakini juu ya kuwepo kwamba muumba ni mmoja tu kwa dhati na sifa zake. Nguzo nyingine za imani zinajengwa juu ya imani ya Mungu mmoja wa kweli, imani juu ya maisha baada ya kifo, imani juu ya Malaika wa Mungu, vitabu vyake na kudra na tafsiri ya vitendo ya imani hii ni: Sala, Zakah, Saumu na Hija.
 
Elim ya anga imekupitia kushoto sana. Mars Jupiter Satan vunus zinaonekana kwa macho bila hata msaada wa viona mbali
Elimu ya Imani imekupitia mgongoni bora mimi imepita kushoto hiyo elimu ya anga
 
Kwetu sisi Wailsamu Imani ni kuwa na yakini juu ya kuwepo kwamba muumba ni mmoja tu kwa dhati na sifa zake. Nguzo nyingine za imani zinajengwa juu ya imani ya Mungu mmoja wa kweli, imani juu ya maisha baada ya kifo, imani juu ya Malaika wa Mungu, vitabu vyake na kudra na tafsiri ya vitendo ya imani hii ni: Sala, Zakah, Saumu na Hija.

Sio kosa na wala hamtendi dhambi Kwa hiyo mungu mnayemuamini.

Kwa mujibu wa Waislam na Quran, mungu wenu anaitwa Nani? Na lini alijitambulisha kuwa Mimi jina langu ni hili?

Hapo ndipo utajua kuwa kuna miungu na Mungu Mkuu
 
Kama wewe umeshindwa kutoa proof za porojo zako mie ambae sijawahi kufa au kushuhudia mtu aliyekufa akafufuka nitapata wapi proof
Kanuni ya kupinga jambo lazima wewe mpingaji uthibitishe ukweli wake wa jambo hilo. Huwezi kupinga bila hoja na kuuleta ukweli wako hapa, kufanya hivyo ni sawa na bure
 
Sio kosa na wala hamtendi dhambi Kwa hiyo mungu mnayemuamini.

Kwa mujibu wa Waislam na Quran, mungu wenu anaitwa Nani? Na lini alijitambulisha kuwa Mimi jina langu ni hili?

Hapo ndipo utajua kuwa kuna miungu na Mungu Mkuu
Rejea kwenye mada Mkuu, huko unakoelekea utachanganyikiwa zaidi, turudi kwenye mada hii nyepesi maisha ya baada ya kufa, na mambo yanayotokea wakati wa kufa ndio mzizi wa mada.
 
Na wanasayansi ndio waliunda dunia na sayari zote pia
.
20230324_092143.jpg
 
Jina lingine huitwa ''Ulevi wa kifo'' haya ni 'maumivu ya kifo' au mafuriko ya mauti. Hakika Kila nafsi itataabika wakati wa mauti yake. Kwetu sisi waislamu tunazo dalili ambazo humpata mtu siku 40 kabla ya kufa kwake.

Nafsi zetu ipo siku zitalipwa adhabu ya udhalili kwa sababu zilikuwa zikisema uwongo juu ya Mwenyezi Mungu, na kuzifanyia kiburi Ishara zake.

Sakaratul Mauti ni Uchungu wa kifo, ni magumu ya pekee ambayo mtu anayekufa hupata kabla ya kifo chake na wakati nafsi inatoka kwenye mwili wake. Ni ngumu sana mwanaadamu kupata nafasi ya kutoa Wosia kwa jamaa zake akiwa katika kipindi hiki.

Ulevi wa mauti' ni hali maalum inayoambatana na ukali na ina athari kubwa katika nafsi na mwili wa mwanadamu, na miongoni mwa athari zake ni kutokea hali mbaya ya usingizi na ulevi kwa mtu anayekufa, na hali hii inamshinda, kubadilika. ufahamu wake na akili yake, hivyo kwamba mtu anayekufa katika hali hiyo anakuwa kama mlevi, na ndiyo sababu ikasemwa kwamba 'Kifo ni kichaa''. Siku zote anayekufa lazima ajisaidie haja kubwa na ndogo.

Na ulevi wa mauti kwa mtu anayekufa huwa ni mkali sana, yaani ukali wake unaoushinda na kuubadilisha ufahamu wake na akili yake ni kama ulevi kutokana na kinywaji.

Viwango vya ukali wa kifo

Ulevi wa kifo ni moja ya hali ngumu sana ambayo mtu hupitia mwisho wa maisha yake ya dunia wakati anakufa na roho inapotoka kwenye mwili wake, kifo na ukali wake, lakini wakati wa kufa kwake ni mwanzo wa faraja yake, na kuokoka kwake na matatizo ya dunia, hivyo anajikuta katika hatua nyingine ya maisha.

Ukali wa kifo “Kwa Muumini ni kama harufu nzuri anayoisikia, kisha analala usingizi kwa sababu ya wema wake, na uchovu wake wote na maumivu huondolewa kwake, na kwa mtu mwenye kiburi aliyepuuza matakwa ya MUNGU ni kama kuumwa kwa nafsi. Michomo ya nyoka na n'ge, ukali wake huwa ni mbaya zaidi.

Katika Hospitali nyingi kumeshuhudiwa watu wakitapa na kuhangaika wakati wa kukata roho, mwingine roho inatoka akiparamia ukuta kwa machungu.

Maumivu ya kifo ni kama chujio kwa watu wengi, ni lazima kila mwanaadamu kupitia hatua hizi, hata wanyama hupitia hatua hizi wakati wa kuchinjwa kwao, hupaparuka na kwenda hovyo. Uchungu wa kifo wakati mwingine umefananishwa na machungu anayopata mbuzi akichunwa ngozi yake akiwa mzima.

“Mauti ni msafishaji, huwachuja Waumini na dhambi zao, na ni uchungu wa mwisho unaowasibu, ni fidia ya dhambi iliyobakia.” Kwa ajili yao, na Atawatakasa walioamini na matendo yao mema. , ili iwe ni raha au faraja ya mwisho itakayowafuata, na iwe ni malipo mema ya mwisho watakayopata.

Uchungu wa mauti na ukali wake ni lazima kwa kila nafsi, na ni makali sana kwa watu wasiomjua MUNGU, na inaweza kuwa kali kwa baadhi ya waumini ili wanyanyue safu zao na kuwaondolea madhambi yao, kwa kuwa inaweza kuwa nyepesi. kwa wengi wao:

View attachment 2700348
Mna shida nyiieee.....sisi wenzenu kuishi ni Kristo,kufa faida,tunakufa km tumelala tunangojea ufufuo!!!!
 
Back
Top Bottom