Haya ndiyo mambo ya ajabu niliyowahi kuona na kushuhudia kwa macho yangu, sitoyasahau katika maisha yangu

Ninaposema kuwa nimeshuhudia nakuona kwa macho yangu siyo kwamba nimekuja kutunga story ili niwafurahishe hapana

Tena humu Kuna watu wameona mazito kuliko haya ninayoyazungumza kiufupi tu Mimi sinywi pombe wala sivuti bangi
[emoji3][emoji3]uliyakomesha
 
Sitasahau nilipolala makabulini kisa kutafuta utajili usiku akaja Simba Kwa macho yangu namuona Simba usiku WA manane tena makabulini nikajikaza kiume baada ya mda akaja mtu na gari mpya Huku kafungulia nyimbo ya Rose mhando nibebe na ni usiku nimelala makabulini ghafla akapotea Yani usiku huo niliuona kama nimelala mwaka makabulini utafutaji huu Acha Tu mauza uza kibao
 
(8) NILIMSHITUKIA BINTI MMOJA ALIYEKUA ANAJIPAKA DAWA ZA KIENYEJI KABLA YAKUFANYA MAPENZI.

Hii nilikutana nayo kijiji kimoja kilichopo mlandizi kinaitwa kwa DOSA kipo karibu na kambi ya ruvu jkt.

Kama Kuna kamanda alipiga kozi pale bila Shaka atakua anapajua vizuri tu, maana eneo lile makuruta tulikuwa tunapenda sana kwenda huko kulikua Kuna kila kitu unachokitaka.

Sana sana makuruta na serviceman walikua wanakwenda kufuata wanawake na wasichana wa pale huwa hawana hiyana hasa anapokujua we ni kamanda.

Naam, nilikua napiga kozi pale ya jkt katika pita pita zetu huko mashambani nilikutana na binti mmoja mzuri alinipa baada yakumtongoza aliniambia anaishi kwa DOSA.

Nilisubiri nikipata pass hata ya siku kazaa ndiyo nitakwenda kukutana na huyo binti mitaa ya kwao kwa dosa.

Aliniambia anaishi yeye na mdogo wake wazazi wamesafiri kwa hiyo hata nikienda kwao hakuna shida.

Hiyo ilinipa kigugumizi kidogo kwenda kwa binti Tena kwao, lakini kwa kuwa kichwa chini kilisha simama Cha juu hakifanyi kazi na ukiangalia sina pesa yakumpeleka gest maana posho ya jkt ilikua ndogo inakidhi mahitaji yangu madogo madogo.

Nakumbuka siku hiyo nilipata pass ya siku mbili, niliona huu ndiyo muda wa kwenda kukutana na binti wakwa DOSA

Mishale ya saa mbili usiku Yule binti alinipokea nyumbani kwao na alinipeka moja kwa moja mpaka chumbani kwake

Kwa mazingira ya pale nilivyoyasoma niliona ana uhuru sana maana anaishi na mdogo wake aliyekuwa anasoma darasa la nne.

Nilikaribishwa ndani Yule binti alinipelekea maji yakuoga, kamanda nilibadili nguo zangu chapu nikawahi kuoga bafu lilikua lipo nje halafu mazingira ya kijijini ni kiza .

Sasa nilipomaliza kuoga niliona nisiende ndani moja kwa moja nilianza kukagua mazingira ya nyumba kwa usalama zaidi huku muda huo Yule binti nilimuacha chumbani kwake.

Kipindi nakagua nyumba kwa usalama nyuma ya nyumba ili likitokea lolote nijue kamanda najidhatiti vipi au naweza nikakimbilia wapi ili kuokoa uhai wangu.

Kipindi nipo nje nilipita kwenye lile dirisha la binti alilokuwemo ndani ama kile chumba chake alichonikaribisha.

Nilishitushwa na minong'ono iliyokua ikitokea chumbani kwa Yule binti, nikajiuliza mbona anaongea peke yake.

Kwa binafsi nilihisi au Kuna Jambo binti alipanga na mtu muda mrefu watengeneze fumanizi.

Nilisogea mpaka dirishani nikasogeza pazia kwa utaratibu kabisa ambapo ni ngumu hata yeye kuniona maana nyumba ilikua haina umeme na Yule binti alikua amewasha chemli mwanga hafifu kwa kupitia dirishani niliweza kuona nakujua binti alikua anazungumza Nini

Nilimuona binti alishika kibuyu kidogo akiwa uchi wa mnyama na alikua akinuia kwenye like kibuyu Kisha anaweka kilicho ndani ya kibuyu juu ya kiganja chake baada ya hapo anapakaa sehemu zake za siri hicho alichokitoa ndani yakibuyu.

Alifanya hivyo kwa kurudia nakunong'ona Mara tatu ila sikufanikiwa kusikia alichokua ananuia katika kile kibuyu.

Nilipoona vile ilinibidi niende ndani katika hicho chumba alichopo binti,

Nilitaka kuingia bila ya hodi lakini binti alikua amejifungia kwa ndani mpaka nilipogonga ndyo alifungua akiwa amejifunga kanga moja tu.

Nilivyoingia ndani Cha kwanza nilitazama kibuyu lakini sikukiona Hapo ndipo nilipopata wasiwasi nilijiuliza alikua anapaka Nini huyu sikupata majibu.

Nililala na huyo binti, sikusubutu kumgusa kabisa mpaka asubuhi na yeye alishangaa sana mpaka akaniuliza upo sawa nilimwambia ndiyo.

Saa kumi na moja asubuhi nilibeba begi langu, nilimpa Yule binti elfu tano nikapotea , nilikata na mawasiliano mpaka Sasa sijui anaendeleaje.
 
[emoji16][emoji16]
 
Aisee, wewe noma...
 
mbn wengine tunatembea usiku mnene tena njia za makaburin lakini hatuwaoni hao majini na walozi, au wana watokea watu special.

Hao wavunja nazi na wanao oga mabarabarani nitaamini wapo lakini uchawi na majini hivyo vitu havipo.
Akili hauna
 
Hii iliwahi kututokea tulipokuwa wanafunzi wa shule Moja ya day huko Morogoro. Ni kweli paka zilikuwa nyingi, zinapiga kelele na kulia usiku kama watoto. Pia zilikuwa zinatembea kwenye bati kwa vishindo vikubwa kama vya Binadamu. Siku Moja tukakubaliana tuwaue kwani tulipanga wanafunzi 4 wavulana watupu kwenye hiyo nyumba.

Jamaa Mmoja akalipiga na kuliua paka Moja. Hahaaaa, Mzee J baba mwenye nyumba akawa mkali kwanini tumeua paka wake. Akatuwashia moto kweli Jumamosi Ile. Ile nyumba ilikuwa na mauza uza mengi sana. Mungu katulinda na kutusaidia sana na kimsingi ndipo nilipopataga pia jini mahaba pale. Haya masuala ya kiroho sema sana ila omba yasikukute.
 
mpaka sasa bado una jini mahaba?
 
Duh, kweli mkuu hii dunia inatisha sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…