Haya ndiyo matumizi ya Tsh 600B za uchaguzi!!! Tusishangae vijana kuchoma nchi

Haya ndiyo matumizi ya Tsh 600B za uchaguzi!!! Tusishangae vijana kuchoma nchi

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
9,780
Reaction score
15,488
Wakati vijana wanamaliza vyuo na mikopo, nchi nayo inakopa sio kwa kuwasaidia vijana wetu bali inakopo na kutumia pesa kununua ma range rover , VX na chaguzi kama hizi. Serikali imetumia Tsh Billion 600 kwenye huu uchaguzi ambao tumeona waziwazi kura zinaibiwa, kura hata hazijahesabiwa, vurugu tupu na aibu kwa nchi. Tulishauri hapa chaguzi zisogezwe mbele hata kwa mwaka ili tutengeneze katiba mpya twende kwenye chaguzi vizuri kama nchi mmoja. Sasa Tanzania vijana wamepata sugu, mgawanyiko kwenye jamii ya Tanzania ni mkubwa sana, watu wametekwa bila sababu za maana, vijana wameuliwa bila sababu na mali zimeteketezwa.

ICC inafanya uchunguzi na watafungua kesi mahaka za kimataifa na vyombo vyetu vya usalama vitahusika. Unyanyasaji mkubwa na kubambika kesi za ajabu mtu anapewa kesi ya ugaidi kwa kuchochea maandamano wakati alikuwa jela chini ya ulinzi, hakuna chochote cha ujumbe wa kuandamana wala nini ilimradi haungi mkono wizi anafunguliwa kesi.

Kama kweli unapenda Tanzania pigania haki tulisema na tunasema tena bila HAKI hizi vurugu zitakuwa trela tu mlipuko mkubwa utatokea tena muda si mrefu. Huku Jeshini kuna mgawanyiko kati ya vijana na wazee ni muda tu mambo yatakuwa mabaya. Bado visasi kwa ndugu na jamaa wa machawa na viongozi hawa vijana watawajua tu. Lakini pesa yote hiyo billion 600 imetumika kwa nini? Yale magari VX ya wagombea sasa watajibinafisisha!!

Bila kubadilika na kujitambua tutakuwa ZIMBWABWE
 
Kama kweli unapenda Tanzania pigania haki tulisema na tunasema tena bila HAKI hizi vurugu zitakuwa trela tu mlipuko mkubwa utatokea tena muda si mrefu. Huku Jeshini kuna mgawanyiko kati ya vijana na wazee ni muda tu mambo yatakuwa mabaya.
Sisiemu imekuwa kichwa cha mwendawazimu, kila mtu asaivi anajifunzia kunyoa.

Wataelewa haya hali ikiwa TOO LATE.
 
Nchi ikianza kuwekewa vikwazo na nchi zingine hapo ndio akili zitakaa sawa
 
Rangi tunaanza kuziona, hakuna mtalii atakuja bongo utalii unarudi kenya
 
Back
Top Bottom