Haya ndo majibu ya Alikiba na Harmonize kwa Diamond Platinumz baada ya kupata mwaliko wake...

Haya ndo majibu ya Alikiba na Harmonize kwa Diamond Platinumz baada ya kupata mwaliko wake...

Kuomba msamaha ni kukiri kosa sio kujisahaulisha na kutaka mambo yaende tu kwa kuwa umeamua wewe, ni rahisi mtenda kusahau lakini mtendwa anaumia daima.
HV Mond kamkosea nn Kiba,mnasahau kipindi Mondi anatoka Bob Junior na Kiba walimtimua sharobaro records wakizani ndo itakuwa anguko lake,mungu kamfikisha mpaka hapa alipo Kiba kajaribu kuvuruga events nyingi sana za Mondi ila Mondi yupo kimya tu show nyingi za Mondi Kiba nae alikuwa anaandaa zake the same date ili kuipunguza makali show za Mondi ila Mondi huwezi kumkuta mtandaoni au kwa interview akilia lia na hiki ndo kinanifanya nimkubali huyu kijana maaana tit for tat is a fair game no kulalamikaling
 
Hakuna kitu kama hicho. Hivi unaweza kuniambiaje, mtu ametoa nyimbo zaidi ya nne kwa vipindi tofauti na kila wimbo unapotoka unapata views za kutosha.

Ila wakati watu wengi wanapoanza kuuangalia ghafla views zinasimama kwa siku nzima na views zikianza kusoma zinapungua kwanza ndipo zinaendelea na mwisho wa siku wimbo haufikishi views nyingi.

Sasa hapo mchawi wa alikiba anakuwaje alikiba mwenyewe?
Kwa akili zako hizo Mondi si angekuwa anaongoza Afrika kwa views kama anauwezo wa kupunguza views za Kiba,kuna muda fikiri kabla ya kuchangia hoja maana unazid jishushia hadhi
 
Kuna kitu kibaya Diamond "anaweza takuwa" amemfanyia Kiba ndio maana kila wakati anataka wayamalize, kama ni hivyo bora aombe msamaha yaishe maana kosa halina muda wa kuisha bila kuondoa tofauti, kama anaona muda umepita kosa limepita atakuwa anajidanganya.
Ww acha kupiga ramli , kitu gani kibaya alichofanyiwa , huyo jamaa yenu kiba ni hopelessy , kwann hasiweke wazi iko kitu?
 
Nikweli
Unachotakiwa kujua ni kwamba Mondi ameanza kujifanya anataka kumaloza bifu na kiba, mara baada ya kuvurugana na clouds ambako saiv ali ndiye msanii wao. So mond anamtaka kiba kwa ajili ya kuishusha clouds na amegundua harmo pia anaweza chukuliwa na hao clouds ndio maana anajifanya kuwasogeza karibu harmo na kiba.

Ila anachosahau ni kwamba anawafanyia au amewahi kuwafanyia vitu vibaya kiba na harmo directly. So ni mnafiki tu, hakuna cha kumaliza bifu wala nini.
Vitu gani vibaya ? Mbona hamvisemi ?
 
Saa chache baada ya msanii, Naseeb Abdul maarufu Diamond Platnumz kuwaalika Harmonize na Ali Kiba katika tamasha la Wasafi, wawili hao wameibuka na kumjibu.

Wakati Ali Kiba akimtaka Diamond kutomfuatilia akitumia neno “unikome”, Harmonize amesema hataki kuongea kuhusu jambo hilo.

Leo mchana Jumatano Oktoba 30, 2019 Diamond wakati akizungumzia tamasha hilo litakalofanyika Novemba 9, 2019 jijini Dar es Salaam alisema ana imani Harmonize atashiriki na kwamba amepeleka mwaliko kwa uongozi wa Ali Kiba, ili msanii huyo naye ashiriki tamasha hilo.

"Wenzetu (wasanii) Nigeria ndio maana wanaendelea kwenye muziki kwani kunapokuwa na matamasha kama haya wanaweka tofauti zao pembeni, kumkuta jukwaa moja Wizkid na Davido ambao walikuwa na bifu kwao ni jambo la kawaida.”

“Kwa nini tung’ang’anie bifu hata sehemu ambayo ni ya kutengeneza pesa na kutuleta Watanzania pamoja,” amesema Diamond katika mkutano wake huo na waandishi wa habari.

Baada ya Diamond kueleza hayo, Mwananchi lilimtafuta Ali Kiba kujua kama ataweza kushiriki katika tamasha hilo na msanii huyo alisema hawezi kulizungumzia hili.

Baada ya muda Ali Kiba alimjibu Diamond kupitia ukurasa wa mtandao wake wa kijamii wa Instagram, “usiniletee mambo ya darasa la pili unaniibia penseli halafu unanisaidia kutafuta unikome.”

“Mwanaume huwa anaongea mara moja tu sasa ukitaka nikuweke uchi watu wajue unayonifanyia hata kwenye hilo tamasha hatokuja mtu sasa tuishie hapo nakutakia tamasha njema.”

Wakati Ali Kiba akieleza hayo, Harmonize alipoulizwa na Mwananchi amesema, “achana na hayo mambo ya Diamond, tuongee mambo mengine.”
View attachment 1249233
Msio
 
Hivi unaposema kiba hategemei mziki na diamond anategemea mziki maana yake nini. Diamond ana biashara kama radio, tv na matangazo kibao. Niamboe kiba anategemea nini
Tv na radio sio za naseeb yeye kuna share tuu anayopata ila sio biashara yaake inamaana mwenye hio biashara akiaamua Leo hio kumuondoa anamtoa so usisifie vitu usivyovijua
 
A
Ali kiba ana akili za kimasikini na atabak msanii wa kilocal wanavosemaga ana dharau kumbe kweli
ACha kuongea ujingaa wewe unajua kiba na we ni sawa ?endelea kusubir awe masikin bongo bhana ukiwa msanii usipojianika ww na mali zako kwenye media ww ni masikin...mutukomeee hatutakii shoboo mjifunze kubalance shoboo manake huku kwenye media mnatafuta wema machoni pa wanadamu wakati upande wa pili upuuz yaan mond anajua kucheza na akili za wajinga wenzakee
 
Kma a, kama kuna kitu kibaya mondi alimfanyia Kiba lazima kitakuwa kina muumiza, hao kina Tale ni wapiga zumari tu bila mondi hakuna wao, wamuache atafute kile anacho hitaji wasimpangie uadui au urafiki, mondi ni mtu mzima hao mameneja washukuru kuajira nae waache kimbelembele.
Hicho kitu kibaya ni kipi asichosema?! Sana sana kuna wakati alipoulizwa kuhusu bifu lao alitaja sababu za kijinga kabisa... suala la kufutiana sauti kwenye wimbo!!

Hakuna lolote zaidi ya mambo ya kipumbavu! Si ajabu hapo kaenda kwa mganda wa kienyeji kaambiwa nyota yako imechukuliwa na mpinzani wako! Sasa kama sio upumbavu tuite nini!

Muziki duniani kote umebadilika! Muziki duniani kote siku hizi watu wanatoa ngoma back to back kwa sababu ule upuuzi wa zamani kwamba eti ngoma mzuri inaishi, hivi sasa huo upuuzi hauna nafasi!!

Huo upuuzi hauna nafasi kwa sababu siku hizi media za kusikiliza ngoma zipo nyingi, na matokeo yake, ngoma ikitoka kwa siku unaweza kuisikia hata mara mia na ushee... ukipanda daladala utaisikia, ukipanda UBA utaisikia, kwa Dar kila uchochoro utakaopita, utaisikia kwa njia mbali mbali! Matokeo yake, ngoma hata ikiwa kali vipi, baada ya muda mfupi itachosha tu kutokana na kuisikia mara kwa mara!

Kutokana na hilo, ili watu wasipotee, ndo hapo linapokuja suala la back to back! Sio zama za akina Marijani Rajabu hizi kwamba mtu ukisikia ngoma yake leo, unaweza usiisikie tena wiki mzima au hata mwezi kwa sababu huna kokote kwa kuisikia zaidi ya Radio Tanzania, na matokeo, kila unapoisikia ngoma kwako inakuwa mpya!

Sasa Kiba na akili zake za kizamani anaamini akitoa ngoma moja, mwaka mzima ita-trend tu! Ikiwa tofauti, ndo pale wajinga hukimbilia kwa waganga wa kienyeji na kuambiwa wamerogwa kumbe mchawi wao ni ujinga wao wenyewe!!!
 
Mpaka Kiba amesimama tena kwenye muziki alihangaika sana nisikiavyo hasa visomo vya Mombasa kwa Joho vimemsaidia sana. Diamond na mama yake walishaizika nyota yake. Kiba hana hamu kabisa.

Diamond hawezi kumchezea Hamo, Chitoholi si mchezo. Aliweza kuwazima walee wa mwanzo sasa atulie.
Angalieni mashabiki wa Kiba hawa! Na ndo tatizo lingine la Kiba ndo hili... ana akili sawa na mashabiki wake!! Mtu hata ngoma hadi mashabiki wake walalamike sana ndo anatoa lakini bado ana wafuasi kibao halafu mnaamini anarogwa!!!!

Ngoja nikuulize: Tangia Kiba umfahamu ameshawahi kutoa ngoma na watu wasiipokee/! Au amerogwa asiwe anaenda studio kutoa ngoma?!
 
Kiboko ya diamond ni harmonize, kwa sababu wote ni wachawi wakubwa na harmonize kamzidi diamond, diamond kamzidi ali kiba, wote wanga hawa
Hapa umenena, hata Dully Sykes siku anahojiwa na Salama Jabiri kwenye Mkasi alisema kiaina hawa watoto wageni kwenye game wachawi ki norma.
 
ac
Saa chache baada ya msanii, Naseeb Abdul maarufu Diamond Platnumz kuwaalika Harmonize na Ali Kiba katika tamasha la Wasafi, wawili hao wameibuka na kumjibu.

Wakati Ali Kiba akimtaka Diamond kutomfuatilia akitumia neno “unikome”, Harmonize amesema hataki kuongea kuhusu jambo hilo.

Leo mchana Jumatano Oktoba 30, 2019 Diamond wakati akizungumzia tamasha hilo litakalofanyika Novemba 9, 2019 jijini Dar es Salaam alisema ana imani Harmonize atashiriki na kwamba amepeleka mwaliko kwa uongozi wa Ali Kiba, ili msanii huyo naye ashiriki tamasha hilo.

"Wenzetu (wasanii) Nigeria ndio maana wanaendelea kwenye muziki kwani kunapokuwa na matamasha kama haya wanaweka tofauti zao pembeni, kumkuta jukwaa moja Wizkid na Davido ambao walikuwa na bifu kwao ni jambo la kawaida.”

“Kwa nini tung’ang’anie bifu hata sehemu ambayo ni ya kutengeneza pesa na kutuleta Watanzania pamoja,” amesema Diamond katika mkutano wake huo na waandishi wa habari.

Baada ya Diamond kueleza hayo, Mwananchi lilimtafuta Ali Kiba kujua kama ataweza kushiriki katika tamasha hilo na msanii huyo alisema hawezi kulizungumzia hili.

Baada ya muda Ali Kiba alimjibu Diamond kupitia ukurasa wa mtandao wake wa kijamii wa Instagram, “usiniletee mambo ya darasa la pili unaniibia penseli halafu unanisaidia kutafuta unikome.”

“Mwanaume huwa anaongea mara moja tu sasa ukitaka nikuweke uchi watu wajue unayonifanyia hata kwenye hilo tamasha hatokuja mtu sasa tuishie hapo nakutakia tamasha njema.”

Wakati Ali Kiba akieleza hayo, Harmonize alipoulizwa na Mwananchi amesema, “achana na hayo mambo ya Diamond, tuongee mambo mengine.”
View attachment 1249233
ACHEN UFA.....L KIBA HAWEZ JIBU HIVYO.
 
Acha ushabiki maandazi
Dogo uliza uambiwe mi hii bongo fleva naijua nje ndani visa na mikasa ya wasanii navijua km vyote hujui chochote kuhusu huu muziki km umeanza kushabikia muziki siku nyingi itakuwa 2005 na huyo diamond utakuwa umemjua kwenye jisachi au kamwambie so you know nothing
 
Back
Top Bottom