..
Kimbinu Chadema wanahitaji timu bora kumzunguka Lissu wakiwemo waandamizi wa serikali zilizopita akiwemo Nyalandu ili kumshape Lissu kama Mgombea Urais lakini pia mipango ya kusaidia kampeni Majimboni ambako hali si nzuri...
Kwa nyongeza, iwapo CHADEMA, chama ambacho viongozi wake, wanachama na wafuasi wanaamini Lissu ni mtaji mkubwa au turufu ya kuingia Ikulu, wanapaswa kutambua yafuatayo:
1) Lissu siyo mwanasiasa wala mwanaharakati kwa hoja zake na matendo. Ili awe "presidential material" yabidi apigwe msasa. Hoja zake hadi sasa ni kama za kuwasilisha mahakamani.
2) Wagombea wa CHADEMA wajipange vilivyo kujibu tuhuma dhidi ya M/Kiti wao kuhusu matumizi mabaya ya fedha za chama, rushwa ya ngono, na ulevi wake wa kupindukia.
3) Kususia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa athari zake zitaonekana wakati wa kampeni, ikizingatiwa chama kina upungufu wa fedha kuendesha kampeni.
4) Kitendo cha CHADEMA, Chama Kikuu cha Upinzani, kuwaengua Wabunge wengine wa vyama vya upinzani, kwenye Baraza la Mawaziri kivuli, athari zake zitajitokeza katika Uchaguzi Mkuu huu.
5) Hama hama ya Madiwani na Wabunge kwenda vyama vingine vya siasa, hasa CCM, na kudaiwa wamenunuliwa, pia madhara yake yatajitokeza kwenye mchakato wa Uchaguzi Mkuu.
6) Matumizi ya lugha isiyo staha, hasa ikilenga kumdharilisha na kumtukana Rais, inaweza kuwa "pendeka" kwa wafuasi lakini si kwa jamii ya WaTz ambao kwao heshima ni kitu cha bure.