Uchaguzi 2020 Haya ni mambo 10 niliyoona kwa CCM Vs CHADEMA mpaka sasa kuelekea kipute cha kampeni rasmi

Upepo gani mbona mimi naona wala amna chochote zaidi ya kupiga piga projo huku mitandaoni

Sent from my SM-A015F using JamiiForums mobile app
 

1. Hoja yako ya kwanza nakubaliana nayo. TL anatakiwa afafanue mabadiliko atakayoyaleta. Niliona akizungumzia suala la kupeleka madaraka ya maamuzi chini zaidi mpaka ktk ngazi za halmashauri, wilaya, na majimbo.

2. Kama Mbowe ni mlevi au mzinzi hilo atajibu mwenyewe. Wapiga kura watawapima wagombea, hawatampima mwenyekiti wa chama anachotokea mgombea.

3. Wasimamizi wa uchaguzi waliengua 90%+ ya wagombea wa upinzani ktk uchaguzi wa serikali za mitaa. Kwa mfano, wagombea 61 wa ACT ktk jimbo la Kigoma Kusini wote walienguliwa kwa madai kuwa hawakuwa raia wa Tanzania. Kitendo hicho naamini kimeleta machungu sana huko mitaani, na wapiga kura wanaweza kuiadhibu CCM.

4. Yako majimbo kadhaa ktk uchaguzi uliopita, jumla ya kura walizopigiwa wagombea wa upinzani zilizidi kura alizopigiwa mwana-ccm, ambaye alikuwa mshindi ktk eneo hilo. Upo uwezekano wa vyama vya upinzani kuumizana vyenyewe kwa vyenyewe.

5. wabunge wengi waliounga mkono juhudi wamepigwa chini ktk kura za maoni za CCM. Maana yake ni kwamba wana-CCM hawakupendezwa na hama-hama. Wapinzani nao hawakupendezwa na hama-hama. Sasa hii hama-hama ilimfurahisha nani? Nani alikuwa akisuka mipango hiyo?

6. CCM sasa wamekuwa vinara wa kutukana viongozi wa upinzani. Matusi anayotukanwa Mbowe, Lissu, Zitto,.. huwezi kabisa kuyalinganisha na "matusi" anayotukanwa Jpm. Na kwa bahati mbaya au nzuri wanaokamatwa na Polisi kwa makosa ya kutukana ni wapinzani peke yao, CCM wao wanapeta tu. Je, wananchi wanapendezwa na hali hiyo? Je, hali hiyo itawa-influence jinsi wananchi watakavyopiga kura?
 
Kwani Chadema hawatukani?

Haoa mtandaoni tu ni kielelezo cha watu fulan humu kushindwa kujibu hoja na walicho nacho to offer ni matusi.

CCM safari hii nadhani wamejipanga vizuri zaidi kukilo miaka yote.

Ndo maana wamewaachia tu uwanja kwa sasa.

..kwa hiyo unakubaliana na hoja yangu kwamba ccm nao ni mafundi wa kutukana?

..Je, wana-ccm wanapotukana viongozi wa cdm huwa wanachukuliwa hatua na vyombo vya dola au polisi?

..ccm safari hii wamejipanga kwa ubabe, vitisho, hujuma, lakini kwa upande wa hoja siamini kama wamejipanga.
 

Hakuna mahali popote nimekubaliana na wewe kwamba CCM ni mafundi wa kutukana.

Wananchi wa Tanzania na ambao ndo wapiga kura wa nchi hii wamegundua mambo mawili matatu kuhusu Tundu Lissu na upinzani kwa ujumla.

1. Kususa kuhudhuria vikao vya Bunge- jambo hili litawafelisha sana wapinzani na wananchi wapo tayari kuwapigia kura wagombea ambao wapo tayari kuwatumikia majimboni na kwenye serikali za mitaa.

2. Wapinzani hawana umoja na sasa wamekataa kuwashirikisha Lazaro Nyalandu na Bernard Membe kwa kutumia reference ya Lowasa.

Mkakati wa CCM ni uleule wa wavuruge na wakuchanganye.

4. Tundu Lissu amekuta tu kutoa hekaheka na kuwapelekesha CCM lakini hawezi kushinda uchaguzi wa mwaka huu.

Nakubali Tundu Lissu ni kiongozi hodari mpanga hoja lakini amekosa mambo makuu matatu, hoja za haja, mbinu ya kuwasilisha hoja zake hizo na pia amekosa maandalizi.

CCM hawajajipanga kwa ubabe, vitisho na hujuma bali ni uzoefu ambao unasahau, sasa hivi wanawaangalia tu.

CCM is the machinery and is not the machine.

Mashine waweza kuwa nayo ya kusaga nafaka tu na ikakutosha.
 
Mbona mzee unapenda ushabiki kwenye mambo ambayo hayaitaji ushabiki wapi niliwahi kusema me Ni mwanachama wa CCM? au wapi nimeonesha me Ni mwanachama wa CCM

Mbona unalia lia mkuu kwani kuwa mwanachama wa ccm ni dhambi????jiamini vyote ni vyama isikuogopeshe hiyo misemo ya lumumba sijui matanga
 

..kwa hiyo wenye siasa za matusi ni wapinzani tu?

..ccm wao hawatukani viongozi wa vyama vya upinzani?

..nakubaliana na wewe kwamba ccm wana mbinu, wana resources, na wana vyombo vya dola.

..Mwalimu Nyerere alipata kusema maneno, " moyo kabla ya silaha." Wapinzani wana MOYO wa kuleta mageuzi nchini.
 

tuache maneno mengi, twende kwa wananchi wenyewe tuone wanasemaje! hwa ni wananchi wakitoa maoni kuhusu mbowe
baba hakuna mtu anawataka msilazimishe
 

Mkuu kwa mfano JPM angesema atoke CCM badala ya mzee Lowasa wakati ule na ajiunge Upinzani unadhani angepita?

Wadhani Dr Slaa angeondoka Chadema kama JPM angejiunga nao?
 
Mbona unalia lia mkuu kwani kuwa mwanachama wa ccm ni dhambi????jiamini vyote ni vyama isikuogopeshe hiyo misemo ya lumumba sijui matanga
Nitakubali vipi wakati me si mpenzi wa hivi vyama Kuna sehemu au Kuna taratibu zozote zilizowekwa humu jamvini kwamba ili kujiunga jamiiforum lazima uwe mshabiki au mwanachama wa CCM au wa Wapinzani?
 
Nitakubali vipi wakati me si mpenzi wa hivi vyama Kuna sehemu au Kuna taratibu zozote zilizowekwa humu jamvini kwamba ili kujiunga jamiiforum lazima uwe mshabiki au mwanachama wa CCM au wa Wapinzani?

Kulia lia kunakujengea udhaifu wa kushambuliwa kikubwa wewe unajua si mwanachama wa chama chochote hivyo endelea kutoa mawazo yako bila kujari watu wanakupeleka chama gani kikubwa wewe ujijue
 
Mkuu kwa mfano JPM angesema atoke CCM badala ya mzee Lowasa wakati ule na ajiunge Upinzani unadhani angepita?

Wadhani Dr Slaa angeondoka Chadema kama JPM angejiunga nao?

..mjadala wa Lowassa ni mgumu sana. wakati wa kampeni alikuwa mgonjwa mahututi. lakini kura alizopata ni nyingi kulinganisha na aina ya kampeni aliyofanya.

..Dr.Slaa aliwahi kusema kuwa akiwa raisi atamsweka Jpm jela. Cdm hawakumtendea haki Dr.Slaa kwa kumnyima nafasi ya kugombea Uraisi.
 

Sio kila mmoja ni mhanga kama unavyo dai,wengine kwa miaka hii 5 ya JPM tumepiga hela kwa kujiajiri tumeenda shambani tumelima kwa Kilimo cha biashara wewe endelea kulalamika jf
 
si mlikua mnasema lowasa mabadiliko , saaahv mmefanya makosa tusubirie ujao tena mseme mmefanya makosa, SKU mkiweza kujenga hoja zenye mashiko kwa watanzania ndo mtaskilizwa, , , yaani mkipata zaidi ya 20% huu uchaguzi njoo tena kwenye huu uzi
THIS TIME WAPINZANI BILA KUJALI WAKO MADARAKANI AU LA NITAJIUNGA NAO BUT ITOSHE KUSEMA WANA WAGOMBEA WAZURI SANA NA HAIJAWI TOKEA TANGU MFUMON WA VYAMA VINGI ,ZAMANI WAGOMBEA WENGI WALIKUA MAMLUKI SAA WAPO WAGOMBEA WANAOJUA MAHANA YA TZ mwafaaa mtiti wa mwaka huu balaa
 
Sio kila mmoja ni mhanga kama unavyo dai,wengine kwa miaka hii 5 ya JPM tumepiga hela kwa kujiajiri tumeenda shambani tumelima kwa Kilimo cha biashara wewe endelea kulalamika jf
We kula kulala ujui hata bei ya mazao, ungekuwa mkulima ungeelewa labda Kama ulikuwa unalima bange
 
Wamejifunza,uzuri wamebakia pure wapinzani,wale dhaifu mfumo umewachuja wameenda unga juhudi
 

True thus awajarudia makosa again,
 
Liweke gazeti lako in terms of numbers. Maada ya takwimu inaelezewa vyema kwa namba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…