Uchaguzi 2020 Haya ni mambo 10 niliyoona kwa CCM Vs CHADEMA mpaka sasa kuelekea kipute cha kampeni rasmi

Uchaguzi 2020 Haya ni mambo 10 niliyoona kwa CCM Vs CHADEMA mpaka sasa kuelekea kipute cha kampeni rasmi

Nikwambie ukweli ktk uchaguz ambao ccm hawakujipanga ni huu, pia ktk uchaguz ambao chadema wamejipanga ni huu, ccm hawakujipanga kwasababu hawakutegemea kama upepo ungebadili iv, ukweli ni kwamba ccm walipanga sana kutumia vyombo vya dola kupata ushindi, na mbinu iliyokuwa inategemewa kwa asilimia zote ni hiyo, Ila lissu baada ya kuja Lissu upepo umebadilika hawaelewi wafanye nini, wanashindwa kujibu hoja zinazowahusu, wanakimbilia kumtetea msajili ovyo kabisa, kiukweli Lissu kawashika pabaya sana, had mmeanza kula maindi ya kuchoma bilakupenda
Upepo gani mbona mimi naona wala amna chochote zaidi ya kupiga piga projo huku mitandaoni

Sent from my SM-A015F using JamiiForums mobile app
 
Kwa nyongeza, iwapo CHADEMA, chama ambacho viongozi wake, wanachama na wafuasi wanaamini Lissu ni mtaji mkubwa au turufu ya kuingia Ikulu, wanapaswa kutambua yafuatayo:
1) Lissu siyo mwanasiasa wala mwanaharakati kwa hoja zake na matendo. Ili awe "presidential material" yabidi apigwe msasa. Hoja zake hadi sasa ni kama za kuwasilisha mahakamani.
2) Wagombea wa CHADEMA wajipange vilivyo kujibu tuhuma dhidi ya M/Kiti wao kuhusu matumizi mabaya ya fedha za chama, rushwa ya ngono, na ulevi wake wa kupindukia.
3) Kususia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa athari zake zitaonekana wakati wa kampeni, ikizingatiwa chama kina upungufu wa fedha kuendesha kampeni.
4) Kitendo cha CHADEMA, Chama Kikuu cha Upinzani, kuwaengua Wabunge wengine wa vyama vya upinzani, kwenye Baraza la Mawaziri kivuli, athari zake zitajitokeza katika Uchaguzi Mkuu huu.
5) Hama hama ya Madiwani na Wabunge kwenda vyama vingine vya siasa, hasa CCM, na kudaiwa wamenunuliwa, pia madhara yake yatajitokeza kwenye mchakato wa Uchaguzi Mkuu.
6) Matumizi ya lugha isiyo staha, hasa ikilenga kumdharilisha na kumtukana Rais, inaweza kuwa "pendeka" kwa wafuasi lakini si kwa jamii ya WaTz ambao kwao heshima ni kitu cha bure.

1. Hoja yako ya kwanza nakubaliana nayo. TL anatakiwa afafanue mabadiliko atakayoyaleta. Niliona akizungumzia suala la kupeleka madaraka ya maamuzi chini zaidi mpaka ktk ngazi za halmashauri, wilaya, na majimbo.

2. Kama Mbowe ni mlevi au mzinzi hilo atajibu mwenyewe. Wapiga kura watawapima wagombea, hawatampima mwenyekiti wa chama anachotokea mgombea.

3. Wasimamizi wa uchaguzi waliengua 90%+ ya wagombea wa upinzani ktk uchaguzi wa serikali za mitaa. Kwa mfano, wagombea 61 wa ACT ktk jimbo la Kigoma Kusini wote walienguliwa kwa madai kuwa hawakuwa raia wa Tanzania. Kitendo hicho naamini kimeleta machungu sana huko mitaani, na wapiga kura wanaweza kuiadhibu CCM.

4. Yako majimbo kadhaa ktk uchaguzi uliopita, jumla ya kura walizopigiwa wagombea wa upinzani zilizidi kura alizopigiwa mwana-ccm, ambaye alikuwa mshindi ktk eneo hilo. Upo uwezekano wa vyama vya upinzani kuumizana vyenyewe kwa vyenyewe.

5. wabunge wengi waliounga mkono juhudi wamepigwa chini ktk kura za maoni za CCM. Maana yake ni kwamba wana-CCM hawakupendezwa na hama-hama. Wapinzani nao hawakupendezwa na hama-hama. Sasa hii hama-hama ilimfurahisha nani? Nani alikuwa akisuka mipango hiyo?

6. CCM sasa wamekuwa vinara wa kutukana viongozi wa upinzani. Matusi anayotukanwa Mbowe, Lissu, Zitto,.. huwezi kabisa kuyalinganisha na "matusi" anayotukanwa Jpm. Na kwa bahati mbaya au nzuri wanaokamatwa na Polisi kwa makosa ya kutukana ni wapinzani peke yao, CCM wao wanapeta tu. Je, wananchi wanapendezwa na hali hiyo? Je, hali hiyo itawa-influence jinsi wananchi watakavyopiga kura?
 
Kwani Chadema hawatukani?

Haoa mtandaoni tu ni kielelezo cha watu fulan humu kushindwa kujibu hoja na walicho nacho to offer ni matusi.

CCM safari hii nadhani wamejipanga vizuri zaidi kukilo miaka yote.

Ndo maana wamewaachia tu uwanja kwa sasa.

..kwa hiyo unakubaliana na hoja yangu kwamba ccm nao ni mafundi wa kutukana?

..Je, wana-ccm wanapotukana viongozi wa cdm huwa wanachukuliwa hatua na vyombo vya dola au polisi?

..ccm safari hii wamejipanga kwa ubabe, vitisho, hujuma, lakini kwa upande wa hoja siamini kama wamejipanga.
 
Hakuna mahali popote nimekubaliana na wewe kwamba CCM ni mafundi wa kutukana.

Wananchi wa Tanzania na ambao ndo wapiga kura wa nchi hii wamegundua mambo mawili matatu kuhusu Tundu Lissu na upinzani kwa ujumla.

1. Kususa kuhudhuria vikao vya Bunge- jambo hili litawafelisha sana wapinzani na wananchi wapo tayari kuwapigia kura wagombea ambao wapo tayari kuwatumikia majimboni na kwenye serikali za mitaa.

2. Wapinzani hawana umoja na sasa wamekataa kuwashirikisha Lazaro Nyalandu na Bernard Membe kwa kutumia reference ya Lowasa.

Mkakati wa CCM ni uleule wa wavuruge na wakuchanganye.

4. Tundu Lissu amekuta tu kutoa hekaheka na kuwapelekesha CCM lakini hawezi kushinda uchaguzi wa mwaka huu.

Nakubali Tundu Lissu ni kiongozi hodari mpanga hoja lakini amekosa mambo makuu matatu, hoja za haja, mbinu ya kuwasilisha hoja zake hizo na pia amekosa maandalizi.

CCM hawajajipanga kwa ubabe, vitisho na hujuma bali ni uzoefu ambao unasahau, sasa hivi wanawaangalia tu.

CCM is the machinery and is not the machine.

Mashine waweza kuwa nayo ya kusaga nafaka tu na ikakutosha.
 
Mbona mzee unapenda ushabiki kwenye mambo ambayo hayaitaji ushabiki wapi niliwahi kusema me Ni mwanachama wa CCM? au wapi nimeonesha me Ni mwanachama wa CCM

Mbona unalia lia mkuu kwani kuwa mwanachama wa ccm ni dhambi????jiamini vyote ni vyama isikuogopeshe hiyo misemo ya lumumba sijui matanga
 
Hakuna mahali popote nimekubaliana na wewe kwamba CCM ni mafundi wa kutukana.

Wananchi wa Tanzania na ambao ndo wapiga kura wa nchi hii wamegundua mambo mawili matatu kuhusu Tundu Lissu na upinzani kwa ujumla.

1. Kususa kuhudhuria vikao vya Bunge- jambo hili litawafelish asana wapinzani na wananchi wapo tayari kuwapigia kura wagombea ambao wapo tayari kuwatumikia majimboni na kwenye serikali za mitaa.

2. Wapinzani hawana umoja na sasa wamekataa kuwashirikisha Lazaro nyalandu na Bernard Membe.

Mkakati wa CCM ni uleule wa wavuruge na wakuchanganye.

4. Tundu Lissu amekuta tu kutoa hekaheka na kuwapelekesha CCM lakini hawezi kushinda uchaguzi wa mwaka huu.

Nakubali Tundu Lissu ni kiongozi hodari mpanga hoja lakini amekosa mambo makuu matatu, hoja za haja, mbinu ya kuwasilisha hoja zake hizo na pia amekosa maandalizi.

CCM hawajajipanga kwa ubabe, vitisho na hujuma bali ni uzoefu ambao unasahau, sasa hivi wanawaangalia tu.

CCM is the machinery na sio machine.

Mashine waweza kuwa nayo ya kusaga nafaka tu na ikakutosha.

..kwa hiyo wenye siasa za matusi ni wapinzani tu?

..ccm wao hawatukani viongozi wa vyama vya upinzani?

..nakubaliana na wewe kwamba ccm wana mbinu, wana resources, na wana vyombo vya dola.

..Mwalimu Nyerere alipata kusema maneno, " moyo kabla ya silaha." Wapinzani wana MOYO wa kuleta mageuzi nchini.
 
Nikwambie ukweli ktk uchaguz ambao ccm hawakujipanga ni huu, pia ktk uchaguz ambao chadema wamejipanga ni huu, ccm hawakujipanga kwasababu hawakutegemea kama upepo ungebadili iv, ukweli ni kwamba ccm walipanga sana kutumia vyombo vya dola kupata ushindi, na mbinu iliyokuwa inategemewa kwa asilimia zote ni hiyo, Ila lissu baada ya kuja Lissu upepo umebadilika hawaelewi wafanye nini, wanashindwa kujibu hoja zinazowahusu, wanakimbilia kumtetea msajili ovyo kabisa, kiukweli Lissu kawashika pabaya sana, had mmeanza kula maindi ya kuchoma bilakupenda

tuache maneno mengi, twende kwa wananchi wenyewe tuone wanasemaje! hwa ni wananchi wakitoa maoni kuhusu mbowe

baba hakuna mtu anawataka msilazimishe
 
..kwa hiyo wenye siasa za matusi ni wapinzani tu?

..ccm wao hawatukani viongozi wa vyama vya upinzani?

..nakubaliana na wewe kwamba ccm wana mbinu, wana resources, na wana vyombo vya dola.

..Mwalimu Nyerere alipata kusema maneno, " moyo kabla ya silaha." Wapinzani wana MOYO wa kuleta mageuzi nchini.

Mkuu kwa mfano JPM angesema atoke CCM badala ya mzee Lowasa wakati ule na ajiunge Upinzani unadhani angepita?

Wadhani Dr Slaa angeondoka Chadema kama JPM angejiunga nao?
 
Mbona unalia lia mkuu kwani kuwa mwanachama wa ccm ni dhambi????jiamini vyote ni vyama isikuogopeshe hiyo misemo ya lumumba sijui matanga
Nitakubali vipi wakati me si mpenzi wa hivi vyama Kuna sehemu au Kuna taratibu zozote zilizowekwa humu jamvini kwamba ili kujiunga jamiiforum lazima uwe mshabiki au mwanachama wa CCM au wa Wapinzani?
 
Nitakubali vipi wakati me si mpenzi wa hivi vyama Kuna sehemu au Kuna taratibu zozote zilizowekwa humu jamvini kwamba ili kujiunga jamiiforum lazima uwe mshabiki au mwanachama wa CCM au wa Wapinzani?

Kulia lia kunakujengea udhaifu wa kushambuliwa kikubwa wewe unajua si mwanachama wa chama chochote hivyo endelea kutoa mawazo yako bila kujari watu wanakupeleka chama gani kikubwa wewe ujijue
 
Mkuu kwa mfano JPM angesema atoke CCM badala ya mzee Lowasa wakati ule na ajiunge Upinzani unadhani angepita?

Wadhani Dr Slaa angeondoka Chadema kama JPM angejiunga nao?

..mjadala wa Lowassa ni mgumu sana. wakati wa kampeni alikuwa mgonjwa mahututi. lakini kura alizopata ni nyingi kulinganisha na aina ya kampeni aliyofanya.

..Dr.Slaa aliwahi kusema kuwa akiwa raisi atamsweka Jpm jela. Cdm hawakumtendea haki Dr.Slaa kwa kumnyima nafasi ya kugombea Uraisi.
 
Ishu sio kujipanga.Kwa miaka hii mitano kila mtz ni mhanga wa kuumizwa na awamu hii ya hovyo kuliko zote tangu ukoloni,watu watapiga kura za hasira kura za kisasi,maana wanajua kama mgombea wa ccm akirudi tena atawaumiza sana again miaka 5 kwa maumivu na mateso makali walilimia meno watalimia kucha sababu ya uzoefu wa mateso waliyopata.Ugumu wa maisha uliotokana na kuwasosmesha watu namba ili wawe masikini ili waweze kutawaliwa umelata chuki kubwa sana watu kuichukia awamu hii.
Hayo makubwa wanayojidaia ayajasaidia kuboresha maisha yao zaidi ya ngojera na propaganda makubwa yamefanyika Dar,Dodoma NA Chato pekee na hayagusi maisha ya watu bali ni kuleta sifa na lengo kuacha legacy tu ya kukumbukwa kawamba jengo hili lilijengwa na fulani lakini hayajaangazia kuinua maisha ya watz.Maendeleo ya vitu pasipo watu uleta umasikin mkubwa sana ktk nchi na umasikini uleta kuchukiwa kwa serikali iliyopo.Ukiachilia DAR,CHATO na DODOMA ni mikoa gani mingine ya nchi wanaweza simama kifua mbele wametendewa haki na awamu hii?
Makundi yote kijamii yameumizwa na hii ni kampeni tosha kwa upinzani mfano wasiojulikana,wafanyafakazi kunyimwa haki zao,wakulima kuzulumiwa mazao yao,wahitimu kukosa ajira sababu ya sera mbovu za kuwakomaoa matajiri eti wawe masikini utadhani wao ndo wagawa riziki.
Tegemeo la ccm in vitu vitatu tu SGR,bwawa ambavyo havina matumaini ya kukamilika lini,na ndege ambavo bado havijagusa maisha ya mtu watu watu shibe kwanza hivo vingine ni ziada hapa ccm hawana hoja.

Sio kila mmoja ni mhanga kama unavyo dai,wengine kwa miaka hii 5 ya JPM tumepiga hela kwa kujiajiri tumeenda shambani tumelima kwa Kilimo cha biashara wewe endelea kulalamika jf
 
si mlikua mnasema lowasa mabadiliko , saaahv mmefanya makosa tusubirie ujao tena mseme mmefanya makosa, SKU mkiweza kujenga hoja zenye mashiko kwa watanzania ndo mtaskilizwa, , , yaani mkipata zaidi ya 20% huu uchaguzi njoo tena kwenye huu uzi
THIS TIME WAPINZANI BILA KUJALI WAKO MADARAKANI AU LA NITAJIUNGA NAO BUT ITOSHE KUSEMA WANA WAGOMBEA WAZURI SANA NA HAIJAWI TOKEA TANGU MFUMON WA VYAMA VINGI ,ZAMANI WAGOMBEA WENGI WALIKUA MAMLUKI SAA WAPO WAGOMBEA WANAOJUA MAHANA YA TZ mwafaaa mtiti wa mwaka huu balaa
 
Sio kila mmoja ni mhanga kama unavyo dai,wengine kwa miaka hii 5 ya JPM tumepiga hela kwa kujiajiri tumeenda shambani tumelima kwa Kilimo cha biashara wewe endelea kulalamika jf
We kula kulala ujui hata bei ya mazao, ungekuwa mkulima ungeelewa labda Kama ulikuwa unalima bange
 
THIS TIME WAPINZANI BILA KUJALI WAKO MADARAKANI AU LA NITAJIUNGA NAO BUT ITOSHE KUSEMA WANA WAGOMBEA WAZURI SANA NA HAIJAWI TOKEA TANGU MFUMON WA VYAMA VINGI ,ZAMANI WAGOMBEA WENGI WALIKUA MAMLUKI SAA WAPO WAGOMBEA WANAOJUA MAHANA YA TZ mwafaaa mtiti wa mwaka huu balaa
Wamejifunza,uzuri wamebakia pure wapinzani,wale dhaifu mfumo umewachuja wameenda unga juhudi
 
..mjadala wa Lowassa ni mgumu sana. wakati wa kampeni alikuwa mgonjwa mahututi. lakini kura alizopata ni nyingi kulinganisha na aina ya kampeni aliyofanya.

..Dr.Slaa aliwahi kusema kuwa akiwa raisi atamsweka Jpm jela. Cdm hawakumtendea haki Dr.Slaa kwa kumnyima nafasi ya kugombea Uraisi.

True thus awajarudia makosa again,
 
Hivi huyo magufuli takwimu gani zinambeba?

Hali ya kiuchumi Kwa wananchi ikoje? Kwa wakulima wa mbaaazi, korosho, tumbaku takwimu zikoje?

Suala la ajira kwa vijana kafanya nini? Ameua uwekezaji na sekta binafsi kaishia kufanya maelfu ya vijana kuwa jobless na watu kupoteza ajira

Ameua watu, kubambikia watu makesi, kuonea watu mpaka hata watoto wadigo wanajua

Ameharibu biashara kupelekea watu kufunga biashara zao na wengine kufirisiwa na mabenki?

Huyo magufuli kafanya ya nini zaidi ya haya? Njia ni nyeupe sana kwa Tundu Lissu mwaka huu.
Liweke gazeti lako in terms of numbers. Maada ya takwimu inaelezewa vyema kwa namba.
 
Back
Top Bottom