Tuangalie viwango vya Dunia vya Jiji kisha tufananishe na Tanga. Tutumie definition ya Wikipedia
View attachment 1626225
Hapo wikipedia wametaja sifa ya jiji kwamba ina extensive system ya
1. Housing
2.transportation
3. Sanitation
4. Utilities
5. Land use
6. Communication
Pia wameongelea uchumi usiohusisha kilimo na watu wengi kukaa kwenye eneo dogo la ardhi.
1. Tuanze na Housing, Tanga kuna makazi ambayo yamepangiliwa, nyumba nyingi mjini zina namba na hazijajengwa ovyo ovyo, zimepangiliwa kwenye mitaa na hata ukiangalia ramani ya Tanga mwenyewe unaelewa hili ni jiji limepangika, makampuni yana nyumba za wafanyakazi, mashule yana nyumba za walimu etc.
2. Transportation
Usafiri pia Tanga si shida kuna usafiri wa maji, barabara, wa ndege na hata reli, tuna connect na mombasa, pemba na zanzibar, wilaya na mikoa tofauti, na barabara za lami ukitoa ya pangani.
3. Sanitation
Mkuu tanga mjini pale jiji zima lipo connected na underground waste system, ukijenga nyumba una connect tu mifereji hio ya maji machafu huna haja ya kuchimba choo, na ni mifereji mikubwa ambayo mtu anaweza dumbukia, i doubt kama kuna mkoa Tanzania wenye system kama Hii,
Pia maji masafi Tanga ni nadra kukatika mjini, na ni masafi kweli unaweza kunywa bila kuchemsha.
Hospitali zipo, na Tanga ni moja kati ya majiji safi Tanzania.
4.communication, Tanga kuna mitandao yote tena 4g, tuna Broadband na Wifi zamani sana, Nipo mdogo city centre yote ipo covered na Wifi, una uwezo ukawa na Tablet ya wifi isiyoingia line na ukawa always connected.
5.land use
Hii inahusiana sana na maneno kutengwa kwa purpose fulani, ukienda Gofu, katikati ya kange na pongwe ama barabara ya pangani utakuta maeneo maalum ya Viwanda, hayaingiliani na makazi, ukienda maeneo ya forodhani utakuta la Casa, chichi, nyumbani hotel etc huko ni night club na starehe nyengine, ukienda barabara za namba ni makazi ya watu etc. Hii inaitofautisha Tanga na majiji mengine ambayo haijulikani wapi bar wapi makazi wapi shule etc.
6. Utilities
Huduma mbalimbali za uma kama maji, umeme, afya, shule, etc vyote vinapatikana kwa wingi na ufanisi Tanga.