Haya sasa twende kwenye klabu bingwa ya Africa tukimtegemea Phiri, Bocco na Kyombo kutuvusha. Nadhani wachezaji na mashabiki wamefurahi sasa.

Mo dewj atuachie timu yetu ama aweke 20b... tumechoka, huwezi kuchukua ubingwa kwa mshambuliaji kama Bocco... mo ondoka.
 
Wanao jaribu kutuaminisha kwamba "mzungu" ni bonge la striker kuliko kyombo waende wakanye kabisa! Ni mzuri kwao huko uzunguni na sio hapa! Ona wabrazil wa singida wanavyomiliki mpira aaf mwangalie na mzungu wenu anavojikanyaga ndo mtutolee utopolo wenu!
 
Kwahyo kwavle anaondoka ndio umeleta thread ya kumsifu

Wakati yupo mlikuwa mnamkosoa hajui mpira kama unabisha em weka uzi humu ulioandika ukimsifia kuwa anajua na ataifaa SIMBA SC.
 
Wewe ni mpiga dili hapo kwenye club?
Wakati mwingine mfiche upumbavu kocha Zoran angekufikisha wapi kila mchezaji hamtaki?

Hamtaki Chama,hamtaki Phiri hamtaki Kapombe hataki kila mtu ila anamtaka Dejan na kuna wapumbavu mnamuunga mkono?
Nyie utopolo kwa nini mnaingilia sana mambo ya Simba?
 
Acha uchawi kijana!
 
Wacha uchongsnishi bro haulipi, Simba SC walikosea kumpa kandarasi huyo Dejan kiufupi hana quality za kuwazidi hao uliowataja, hata nawapongeza Simba SC kwa uamuzi wa kuachana nae maana hakuwa na madhara yoyote kwa timu pinzani. Alafu nikukumbushe Simba ya 1993 ilikuwa Chino ya kocha Kibadeni na ilifika nusu fainali michuano ya CAF, Je Kibadeni alikuwa mzungu? Hebu tujenge utamaduni wa kupenda vya kwetu, Tuache kuwa watumwa wa ngozi nyeupe. By the way Mimi Ni Young African sc, Ila kwenye ukweli nasema kwa maendeleo ya mpira.
 
Mbona timu mlimpokonya Mkwasa mkaenda kuwatafuta kina Kaze na Nabi?? Vya kwenu hamvipendi??
 
Hebu tulieni acheni unafiki wenu, hivi watanzania nani katuloga? Wengi humu mlisema tumepigwa mzungu tumepigwa leo mnakuja kuanzisha thread za kuponda tena. Ni bora wengine tulomkubali toka mwanzo ila kama hivyo maji yameshamwagika. Simba itabaki kuwa Simba hata kama asipokuwepo Dejan kwanza alicheza mechi ngapi dkk zote mpk muanze hapa kumlilia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…