Haya yote yanatokea sababu wananchi hawana pa kusemea

Lamomy

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2023
Posts
43,349
Reaction score
104,110
Ni kwamba serikali na viongozi mlitegemea nini mnapomfunga mtanzania kutoa malalamiko yake?!

Mwanzo watanzania tulizoea wapinzani watusemee na kutuwakilisha kwa kile kinachotuumiza mioyo yetu. Mkaona sio sawa mkaamua kumchukua na kumuweka kizuizini mwenyekiti wa upinzani, haitoshi mkafungia chama kisijishughulishe na mikutano..!!

Mkaenda mbali zaidi mkafungia Twitter (X) na Jamii Forum

Matokeo yake wananchi wameamua kujisemea wenyewe na kuanza kuwakataa wazi wazi bila uoga kitu ambacho huko nyuma hakikuwahi kutokea. Week hii wote tumeshuhudia wananchi walivyogomea mwendokasi na kuamua kujisemea wenyewe.

Hivi mlitegemea haya? Kama kuna siku watanzania watapiga kelele bila woga wakiikataa CCM mchana kweupe wakiwa kwenye mabasi?

Leo kaibuka mwanajeshi, ameongelea matatizo yetu na wananchi tumefurahi. Hiki ndio kitu tunachokitaka. Niwaambie tu hii haitoishia hapo kila sekta itajitokeza kujisemea.
Sababu waliokuwa wanatusemea mmewafunga midomo.!!

Si ajabu akajitokeza polisi wa rank yoyote na yeye kusema kitu kwa taifa.
 
Lamomy mambo?
FB_IMG_1759593571300.jpg
 
Ni kwamba serikali na viongozi mlitegemea nini mnapomfunga mtanzania kutoa malalamiko yake?!

Mwanzo watanzania tulizoea wapinzani watusemee na kutuwakilisha kwa kile kinachotuumiza mioyo yetu. Mbaya zaidi mkaamua kumuweka kizuizini mwenyekiti wa upinzani, haitoshi mkafungia chama kisijishughulishe na mikutano..!!

Mkaenda mbali zaidi mkafungia Twitter (X) na Jamii Forum
Matokeo yake wananchi wameamua kujisemea wenyewe na kuanza kuwakataa wazi wazi bila uoga kitu ambacho huko nyuma hakikuwahi kutokea. Week hii wote tumeshuhudia wananchi walivyogomea mwendokasi na kuamua kujisemea wenyewe.

Hivi mlitegemea haya? Kama kuna siku watanzania watapiga kelele bila woga wakiikataa CCM mchana kweupe wakiwa kwenye mabasi?

Leo kaibuka mwanajeshi, na haitoishia hapo kila sekta itajitokeza kujisemea.
Sababu waliokuwa wanatusemea mmewafunga midomo.!!

Si ajabu atajitokeza polisi wa rank yoyote na yeye kusema kitu kwa taifa.
^Nimeambiwa hapa kwamba unajua kwenye protocol za Jeshi

Captain anaongoza kikosi kizima so huyu kwenye kikosi chake tu akiamuru kiwake kinawaka mazima maana akiita parade wanakuja wote mpaka walioko nje ya Dar.

Halafu Mwanajesh mmoja ni sawa na police 3-5.^

Haya mambo ndo nimejua leo, yajayo yanaburudisha😂
 
Sijui kwa nini hawa viongozi wetu hawajui kuwa ni hatari sana kuongoza watu ambao wana taarifa na wamenyimwa uhuru wa kuzungumza, watu wamefuga hasira wanasubiri tu kusikia paaa. Watawala bado wana akili, fikira na mawazo ya miaka ya 80 huko
 
😹😹😹 hatari sana hii..!!
Na hiyo midude ikichafukwa hapatakalika
 
Sijui kwa nini hawa viongozi wetu hawajui kuwa ni hatari sana kuongoza watu ambao wana taarifa na wamenyimwa uhuru wa kuzungumza, watu wamefuga hasira wanasubiri tu kusikia paaa. Watawala bado wana akili, fikira na mawazo ya miaka ya 80 huko
Hii ni mbaya sana, hata hao CCM wenzao hawapendezwi na haya..!! Taifa linahitaji uponyaji hili.. bado hawajachelewa
 
Mi naona viongozi walidhani Lissu na CHADEMA ni kikwazo kwao, mwenyekiti akawekwa ndani na chadema kuzuiwa kufanya siasa. Tuliliandika litaibuka jinamizi kali zaidi na la kutisha kuliko Lissu na chadema hawakuelewa. Bora wasingemuweka ndani mwenyekiti na kuwazuwia chadema kufanya siasa. Chadema ni wananchi hawahawa kama ccm wangefanya siasa ingesaidia kubalansi siasa za nchi na kuondoa hizi presha za sintofahamu yatakayojiri. Waliambiwa msifanye uchaguzi huu kwanza bila reform huku mkila shushu kwa kipindi cha mpito walau miaka isiyozidi mitatu reform itakuwa tayari wakashupaza shingo. Sasa yanaibuka majinamizi ya kutisha yasiyohusiana na chadema. Watajuta kutokufanya reform na kuikumbuka chadema, maana yake huko mbele ni giza hata wakijitangaza kushinda uchaguzi kwa kishindo majinamizi yatawasumbua hawatatawala vema. Reform ilikuwa ni usalama na ustawi wa nchi
 
Chadema ilipoacha kusema wameinuka wa kutusemea na haitoishia hapa..
 
Ni kwamba serikali na viongozi mlitegemea nini mnapomfunga mtanzania kutoa malalamiko yake?!

Mwanzo watanzania tulizoea wapinzani watusemee na kutuwakilisha kwa kile kinachotuumiza mioyo yetu. Mkaona sio sawa mkaamua kumchukua na kumuweka kizuizini mwenyekiti wa upinzani, haitoshi mkafungia chama kisijishughulishe na mikutano..!!

Mkaenda mbali zaidi mkafungia Twitter (X) na Jamii Forum

Matokeo yake wananchi wameamua kujisemea wenyewe na kuanza kuwakataa wazi wazi bila uoga kitu ambacho huko nyuma hakikuwahi kutokea. Week hii wote tumeshuhudia wananchi walivyogomea mwendokasi na kuamua kujisemea wenyewe.

Hivi mlitegemea haya? Kama kuna siku watanzania watapiga kelele bila woga wakiikataa CCM mchana kweupe wakiwa kwenye mabasi?

Leo kaibuka mwanajeshi, ameongelea matatizo yetu na wananchi tumefurahi. Hiki ndio kitu tunachokitaka. Niwaambie tu hii haitoishia hapo kila sekta itajitokeza kujisemea.
Sababu waliokuwa wanatusemea mmewafunga midomo.!!

Si ajabu akajitokeza polisi wa rank yoyote na yeye kusema kitu kwa taifa.
Tesha sio mwqnajeshi, ana kasoro nyingi sana pale alipo, wajuba tumenotice.
 
Back
Top Bottom