JPM alikuwa fundi sanaa hasa katika uongozi wake. Kwanza aliweza kuweka mambo wazi nyanja zotee.
1. Kimaendeleo hasa linapo kuja swalia za ripoti mbali mbali mfano.Madini kwakweli kupitia Mzee JPM nliweza kujua karibia kila kitu kilicho kuwa kinaendelea katika madini.
Lihali sasa naona giza tu hata taarifa za habari kutoka Channel na redio mbali mbali kukosa mvuto.
2. Aliweza kututia moyo sanaa hasa kwenye swala la kunitegemea na kutuamisha kuwa sisi ni matajiri basi hata kama ni uwongo basi sisi tulijihisi tunaweza na kila mtu alipata mhamko wa kuchapa kazi.JPM best of the Best.
3. Aliweza kukipa hadhi kiti cha uraisi na kueshimika kwa Jinsi alivyo jiweka na mdomaana mnaweza sema alijifanya Mungu mtu lakini kwakweli uraisi ulitua mahala sahihi.
4. Wale matajiri na wakwepa kodi mzee JPM alilala nao mbele mpaka wakakiona cha moto hadi wengine wamepotea kwenye ramani mpaka sasa wameshindwa kusimama tena.
5.Bila majungu nidham serikalini ilirudi kwa sehem kubwa tena sanaa.Si mahospitali nasehem zingine za kijamii.
6. Hakusafiri kwenda popote nje ya Bara la Africa na kulinda maslahi ya nchi yake kwa kuleta maendeleo kitu ambacho mabeberu walikonda sanaa.
Any way zipo zababu nyingi tuu nzuri na pia tunapaswa kujua Binadamu hatukosi kasoro katika maisha yetu ya kila siku.
ILA JPM MPAKA SASA KILA SEHEM HUKAI DAK KADHAA BILA KUTAMKWA JINA LAKE.
HAKIKA TUNA KAZI SANAA YA KUMSAHAU HASA KIZAZI HIKI CHA KWETU.
Magufuli aliwafaa sana wajinga wasioelewa chochote. Alizuia uhuru wa vyombo vya habari ili wajinga azidi kuwalisha ujinga kiasi kwamba wengine waligeuka kuwa wendawazimu:
1) Kwenye madini aliwadanganya sana watu wajinga, wengine mpaka leo wamebakia na ujinga aliowalisha marehemu. Ripoti ya Prof. Mruma ambaye alilazimishwa na marehemu aandike kuwa tunaibiwa ilikuwa ni report kwaajili ya wajinga. Anayefahamu, atajua ni upumbuvu. Ni sawa mtu akuambie nimemwona mwizi ameiba magunia 1000 ya mahindi, amebeba kwenye Hilux pickup, na wewe ukaamini. Chininya marehemu, uzalishaji wa dhahabu ulishuka kutoka kuwa mzalishaji wa 3 Afrika mpaka kuwa mxalushaji wa 6 Afrika. Mapato yaliongezeka kudogo kutokana na kupanda sana kwa bei ya dhahabu, lakini hatukufaidi vya kutosha kama yalivyofaidi mataifa mengine kutokana na kuanguka kwa uzalishaji. Aliua utafiti wa madini kiasi kwamba leo hii hakuna kampuni inayofanya utafiti wa madini Tanzania. Alisababisha uwekezaji mkubwa wa pili Duniani kwenye gas uondoke Tanzania na kuhamia Msumbiji. Marehemu alihangaika sana mpaka anakufa kutaka kuwarydisha wawejezaji wake, lakini walimkatalia katakata.
2) Aliangusha ukuaji wa sekta zote za uchumi. Kwenye ukuaji wa uchumi wa jumla, aliangusha kutoka 7.5% mpaka 1.9%. Kwenye ukuaji wa sejta ya utalii aliangusha toka 15% mpaka 3.6%. Kwenye uwekezaji aliangusha toka 24% mpaka 4%. Thamani ya mauzo ya mazao ya kilimo, aliangusha kwa 50%. Per capita income, kwa miaka 5 aliipindusha kwa dola 80 tu wakati Mkapa katika miaka 10 aliipandisha kwa dola 400, na Kikwete kwa dola 380%. Kwenye uchumi aliua kila kitu. Alikuwa ni kiongozi wa uharibifu.
3) Kwenye demokrasia, uhuru wa watu na haki, kila mmoja anajua. Alileta siasa za kishenzi, za kuteka, kuua, kubambikia watu kesi na kuwapoteza. Hapa, utaona kabisa uthibitisho wa au huyu mtu alikuwa mgonjwa (ukichaa wa aina fulani) au ndani yake kulikuwa na roho ya shetani.
4) Kwenye mahusiano ya kimataifa, he was a zero performer. Hakuna nchi yoyote Duniani inaweza kuwepo bila ya mataifa mengine, na zaidi hizi nchi maskini. Akawaita watu ni mabeberu (labda yeye alikuwa jike). Kwenye Ulimwengu wa leo uliostaarabika, unaita binadamu wenzako mabeberu! He was a primitive leader worth for primitive creatures.
Funzo la jumla ni kuwa bila katiba nzuri ambayo ina uwezo wa kuzuia watu wa ajabu kuchukua madaraka, nchi bado ipo kwenye hatari kubwa ya kuweza kumpata wa namna yake au mbaya zaidi. Fikiria mtu kama Mwigulu awe Rais, si itakuwa afadhali ya marehemu?