Hayati Dkt. Magufuli aliletwa duniani mahsusi na Mungu ili kuleta masomo fulani tujifunze

Ametuonyesha pia watanzania hata uwe mwema na mpenda nchi yako kiasi gani bado watu watakusema vibaya na kukusingizia uovu pasipo vithibitisho.
 
Nilipoona neno "Karne" umeliandika "Kalne" nikapatwa mashaka sana na ulichoandika
 
Mjomba yako alikuwa mtumishi hewa wewe mwenyewe ulikuwa na vyeti feki lazma uponde tu

Kumbuka duniani kote hapakuwawi kutokea kiongozi ambaye alipendwa na jamii yake yote bila kupingwa

Tofauti ipo kwenye alama zinazoachwa na uongozi wao hapa duniani matendo makuu kwa watu wa chini

Kuwa heshimisha masikini na wanyonge wasio na haki na haswa wale tuliopo vijijini

Ndugu zangu utampima vp kiongozi bora kama si kwa alama alizoacha alama ambazo zilishindikana kwa miaka mingi huku tukipewa polojo ni vi story vya kitoto

Niamini mimi alipotoka mwl JK aliye fuata ni Dkt John na baada ya hapo tunayo safari ndeeeefu labda Mungu pekee aamue hii kesi
 
Rejea sababu zilizopelekea kudai na kupigania Uhuru wa Tanganyika zilikuwa ni zipi?

Maendeleo ya vitu hata Mkoloni angeweza kuleta zaidi ya tulipo!
 
ungemsifia tu mbowe, unachojaribu kuaminisha watu its impossible
 
Kuna watu walijilipa mamilioni ya pesa MH.waziri mkuu mpaka akasikitika hivi wamechukuliwa hatua gani? au mchakato wa KESI unaendelea? Enzi zake angemalizana nao Siku Ile Ile na ingekuwa fundisho
 
No moja hpn kbs, mzalendo wa kweli kweny taifa hili tena asie na makando kando ni Mwalimu Julius Kambarage Nyerere pekeee!
 
Kweli kabisa kaka.

Sema wanao mnanga wale chawa wa vyeti feki, Chawa wa ma boss walio kwepa kulipa kodi na panga lika waathiri hadi hao chawa.
 
Mtoa mada nakushauri nenda kwenye forum mbalimbali ambako Magufuri ametajwa au kuanzishiwa mada and then angalia komenti au replies za watu ili zikupe somo.

Although inaonekena wewe ni mmoja wa waliokuwa wamebanwa kupitia ile mianya ya🐁 ya kura bila ruhusa!.
 
No moja hpn kbs, mzalendo wa kweli kweny taifa hili tena asie na makando kando ni Mwalimu Julius Kambarage Nyerere pekeee!!!
Ni kweli mkuu lakini alikuwa ni mtu wa pekee sana uzalendo wake ulikuwa wa vitendo haswaa
 
Na Je, kama hayo masanduku walihusika mabeberu kuvuruga.

Ili wapinzani wasio na sera zinazo eleweka na wapenda madaraka je...? na hao tuwazungumzieje?

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Jamaaa alikuwa mbinafsi sana na roho mbaya sana wenzio aliwafungia akaounti zao za mshahara mfano mbowe ila yy aliendelee kupokea mshahara kwa jasho letu watz
 
Mzee JPM angekumbukwa sana kwa utendaji wake na ufuatiliaji wa maelekezo anayotoa, lakini alikuwa na dosari kubwa sana ya HAKI ZA BINADAMU. Kwenye hili eneo alikuwa "Sufuri" kabisa. Ubaguzi wa vyama vingine kuwaona hawana maana isipokuwa chama chake tu, chaguzi zikawa zinatolewa matamko tu, namtaka fulani mniletee,BADALA ya sanduku la kura liamue nani awe nani.

Eneo hili la haki za binadamu kama JPM angekuwa analimudu vema ikichanganywa na utendaji wake wa kazi ilivyokuwa, basi JPM angekuwa bora sana, lakini kwa kuwa eneo hili alifeli kwa kiwango kikubwa sana, basi atabaki tu kuwa Rais wa hovyo kupindkia, na chama chake hakipaswi kabisa kuiga U-hovyo huo wa kupitisha wagombea kwa mabavu ya bila kupingwa, kuwaagiza Wakurugenzi wapitishe wa chama chake tu kwa kuwa anawalipa vizuri na mafuta ya magari anawapa, halafu wapitishe mwingine! U-hovyo wa aina hii umeacha balaa kubwa katika Taifa ambapo mshikamano wa Kitaifa umepotea.
 
Ongezea na hizi

1.Wahalifu wa Kibiti walikiona cha moto.Kila wakitaka kujipanga kuvuruga amani ya Nchi yetu walikula tako za kutosha waka tulia tuli kama....

2.Aliwaumbua hao ma Professor walio kuwa walimu wa hivyo vyuo ambao ndo wanatoa wanafunzi wao
Kwa kushindwa kuandaa Riport nzuri ya Madini.
Kwa kupotosha Uma kwa kutudanganya madini yalio kuwa yanasafirishwa kule bandari[emoji23]
Sasa kama hao Maprofesor vilaza itakuwaje.

3.JPM alinifurahisha kwa kuto fuga majambazi yakala kodi manineee.[emoji23] Jombaa waliliona Joto.

Any way nikikumbunguka na vingine ntakujaa tena.

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Wewe kwani kufa nyie hamfi huko?

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Hayo mbona hayaonekani yamefutika within 6 month
 
Magufuli aliwafaa sana wajinga wasioelewa chochote. Alizuia uhuru wa vyombo vya habari ili wajinga azidi kuwalisha ujinga kiasi kwamba wengine waligeuka kuwa wendawazimu:

1) Kwenye madini aliwadanganya sana watu wajinga, wengine mpaka leo wamebakia na ujinga aliowalisha marehemu. Ripoti ya Prof. Mruma ambaye alilazimishwa na marehemu aandike kuwa tunaibiwa ilikuwa ni report kwaajili ya wajinga. Anayefahamu, atajua ni upumbuvu. Ni sawa mtu akuambie nimemwona mwizi ameiba magunia 1000 ya mahindi, amebeba kwenye Hilux pickup, na wewe ukaamini. Chininya marehemu, uzalishaji wa dhahabu ulishuka kutoka kuwa mzalishaji wa 3 Afrika mpaka kuwa mxalushaji wa 6 Afrika. Mapato yaliongezeka kudogo kutokana na kupanda sana kwa bei ya dhahabu, lakini hatukufaidi vya kutosha kama yalivyofaidi mataifa mengine kutokana na kuanguka kwa uzalishaji. Aliua utafiti wa madini kiasi kwamba leo hii hakuna kampuni inayofanya utafiti wa madini Tanzania. Alisababisha uwekezaji mkubwa wa pili Duniani kwenye gas uondoke Tanzania na kuhamia Msumbiji. Marehemu alihangaika sana mpaka anakufa kutaka kuwarydisha wawejezaji wake, lakini walimkatalia katakata.

2) Aliangusha ukuaji wa sekta zote za uchumi. Kwenye ukuaji wa uchumi wa jumla, aliangusha kutoka 7.5% mpaka 1.9%. Kwenye ukuaji wa sejta ya utalii aliangusha toka 15% mpaka 3.6%. Kwenye uwekezaji aliangusha toka 24% mpaka 4%. Thamani ya mauzo ya mazao ya kilimo, aliangusha kwa 50%. Per capita income, kwa miaka 5 aliipindusha kwa dola 80 tu wakati Mkapa katika miaka 10 aliipandisha kwa dola 400, na Kikwete kwa dola 380%. Kwenye uchumi aliua kila kitu. Alikuwa ni kiongozi wa uharibifu.

3) Kwenye demokrasia, uhuru wa watu na haki, kila mmoja anajua. Alileta siasa za kishenzi, za kuteka, kuua, kubambikia watu kesi na kuwapoteza. Hapa, utaona kabisa uthibitisho wa au huyu mtu alikuwa mgonjwa (ukichaa wa aina fulani) au ndani yake kulikuwa na roho ya shetani.

4) Kwenye mahusiano ya kimataifa, he was a zero performer. Hakuna nchi yoyote Duniani inaweza kuwepo bila ya mataifa mengine, na zaidi hizi nchi maskini. Akawaita watu ni mabeberu (labda yeye alikuwa jike). Kwenye Ulimwengu wa leo uliostaarabika, unaita binadamu wenzako mabeberu! He was a primitive leader worth for primitive creatures.

Funzo la jumla ni kuwa bila katiba nzuri ambayo ina uwezo wa kuzuia watu wa ajabu kuchukua madaraka, nchi bado ipo kwenye hatari kubwa ya kuweza kumpata wa namna yake au mbaya zaidi. Fikiria mtu kama Mwigulu awe Rais, si itakuwa afadhali ya marehemu?
 
Tunaambiwa kalamu ndio inafoka.

Inafoka inafoka vipi ndio kitendawili maana ikifoka lazima WINO ukuchafue wewe mshika KALAMU.
 
bado kivul cha mwamba kinawatesa mnamwongelea kila kukicha. Hiyo ndo maana halis ya huwez chafua oil chafu bal utachafuka wewe, miez kadhaa badae mtu keshafukiwa lakin bado anawakuna tu.

Jpm oyeee...hatotokea tena kama JPM

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…