Ongezea na
1. Miradi ya tija kwenye jamii, zamani ilikuwa ni ndoto kuona lami uswahilini lkn wkt wa JPM tumeona.
2. Umeme, zamani tuliamini umeme hauwezi kuwa wa uhakika nchini kwetu kwani ni maskini nchi hii so tukawa tunaona umeme kukatika katika ni haki yake lkn baada ya JPM kuchukua madaraka umeme kukatika ikawa historia.
3. Miradi mikubwa ya historia, zamani viongozi wetu walishindwa kufanya miradi mikubwa wakisema kuwa nchi yetu ni maskini haiwezi kufanya miradi inayofanyika nchi zilizoendelea lkn wkt wa JPM tuliona ikifanyika mfano electrical SGR, ujenzi wa moja kati ya mabwawa makubwa kabisa ya umeme Africa na duniani JNHPP, flyovers na interchanges, Airports, Ports, ununuzi wa ndege kubwa, ujenzi wa meli kubwa kubwa, masoko n.k kiasi cha kwamba leo hii imeshakuwa fashion kwamba ili ukubalike na jamii lazima ufanye kama alivyokuwa anafanya JPM.
4. Thamani ya mwananchi, zamani mwananchi hasa wa hali duni alikuwa hathaminiki kabisa lkn baada ya JPM vyombo vya dola, wabunge na watumishi serikalini wakaijua thamani halisi ya mtanzania bila kujali ni tajiri au maskini.
5. Heshima ya Tanzania na Watanzania, zamani nchi yetu ilidharaulika sn hasa na nchi jirani, lkn miaka michache baada ya JPM nchi ikapanda thamani na kuwa mfano hapa Afrika kwa utekelezaji wa uchumi jumuishi (inclusive economy)
6. Shamba la bibi, zamani kabla ya JPM nchi yetu ilikuwa shamba la bibi lkn baada ya JPM kila mtu anajua kilichotokea.
7. Msimamo, JPM alikuwa kielelezo cha msimamo wa waafrika mbele ya wazungu kwamba tuna haki ya kupanga mambo yetu pasipo kuingiliwa na mtu yeyote.
8. Kujitambua, JPM amefanya watanzania wazijue haki zao kwamba hii nchi ni yetu sote na sio ya kikundi fulani fulani cha watu, na kwamba watanzania wanapaswa kutumikiwa na viongozi wanaowachagua.
9. Pesa ni za wananchi, JPM amefanya Watz wajue miradi inayofanyika ni pesa zao wananchi na kwamba inapaswa kufanyika na kuisha ndani ya muda muafaka, lkn pia miradi inayofanyika inapaswa kuwa bora na kuakisi thamani ya pesa (value for money).
10. Uchapakazi, JPM amefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuambukiza uchapakazi wake kwa Watz, leo hii Watz wanafanya kazi bila kuchagua, iwe ni kuajiriwa au kujiajiri, tunaona Watz wengi sasa wamekuwa wakifanya biashara ndogondogo na kubwa si wanawake wala wanaume wala c vijana, kila mtu yuko bize kutafuta maisha yake kwa njia halali mpk imekuwa kero huko mijini hakupitiki, hii yote ni kwasababu raia waliipokea vyema kauli mbiu ya HAPA KAZI TU.
Kuna mengi ya kumuelezea Magufuli ambapo kama nitaamua kuyaweka humu itakuwa ni kitabu, hivyo basi itoshe tu kusema kwamba JPM alikuwa moja kati ya viongozi bora zaidi kuwahi kutokea katika nchi hii japo kama mwanadamu hakukosa kasoro lkn kiukweli kabisa kasoro zake haziwezi kuficha mema mengi aliyoifanyia nchi hii.