Wilderness Voice
JF-Expert Member
- May 19, 2016
- 921
- 1,649
- Thread starter
- #41
Unauhakika kwamba watanzania walifunga na kuomba ili uongozi wake ukome? Ulifanya utafiti! So mtu akifa madarakani uongozi wake mbaya? Tusihukumu na kujifanya tunajua zaidi kuliko Mungu.Wapo wanadamu ambao hufa kwa sababu wameishi na kumpendeza Mungu, na baada ya kutimiza mapenzi yake, huwarudisha watakatifu wake. Na wengine, kupitia vifo vyao, Mungu hutaka kutufundisha tuliosalia kuonesha kuna watakatifu wake ambao wameishi kwa kumpenda na kumtumikia yeye tu.
Mateso na vifo vya mitume na waumini wa kale, ni moja ya vifo ambavyo vilituhakikishia kuwa kuna watakatifu wa Mungu waishio Duniani. Hawa walikufa kwa vifo vizuri maana waliilinda imani hatankatika mazingira magumu na ya mateso Makuu. Hata hivyo Mungu aliwaimarisha katika safari zao ili wayashinde mauti.
Wapo watu waliokufa kwa vito vya adhabu ili kuwalinda watu/wana wa Mungu. Askari wa Pharaoh waliuawa ili kuwalinda Waisrael. Herode alikufa ili mtoto Yesu awe salama. Kwa hiyo tutambue kuwa, ni kweli wapo wanaokufa ili kunusuru wengine. Nisiloweza kutamka, japo maisha ya Maguguli yaliondoa uhai wa baadhi ya watu, yalileta majonzi kwa wengi na kuleta mateso makubwa kwa baadhi ya watu, kama mwanadamu siwezi kusema kama kifo chake ilikuwa kuwanusuru wengi ambao wangeendelea kuangamia. Kilicho dhahiri, watanzania wengi walifunga na kuomba au marehemu apate hekima ya uongozi au uongozi wake ukome. Hawa wote walioomba, wana haki ya kumshukuru Mungu, siyo kwa sababu Magufuli amekufa bali kwa sababu ombi lao la kutaka uongozi wake ukome, sala yao imesikilizwa.
Sababu za Magufuli kufa azijuae ni Mungu pekee, na anakusudi lake! Tusijifanya tunaelewa juu ya uondoaji wa roho za watu!