Hayati Dkt. Magufuli anapohukumiwa kwa kifo chake

Hivi nani mwenye ushahidi wa kweli, tuache porojo za kusikia, kuwa Magufuli ndiye alie uwa hao unao sema, Magufuli ndiye sijui alifanya hiki. Mimi huko staki kuongelea sina ushahidi. Awe Magufuli alifanya au hakufanya. Je binadamu tuna mamlaka ya Kuhukumu? Ndo maana nilipokuwa chekechea nilishanga kwanini Mungu anamlinda mtu alie uwa. Tena alie uwa ndugu yake! Mpaka Mungu anaapiza kuwa ole wake atakae muuwa Kaini.
Hii sikuielewa wakati ule, nilimshangaa Mungu sana.
 
Ndugu huyo unaesema watu wanamhukumu baada ya kifo siyo kweli. Watu walianza kumsema kabla ya kufa.

Na kuhusu kuijua bible mimi naona bado sana. Wewe huyo unasema kifo Mungu ndo anapanga bila kujua kifo kilitokana na shetani. Ukihitaji mistari sema nikumiminie hapa ili utulie.
 
Nje kidogo ya mada:

Mungu alizuia kuawa kwa Kaini, ukoo wa Adam ungeendeleaje, kama baada ya Abel kuuawa na Kaini auawe, maana yake angesalia mtoto mmoja tu wa kiume.

Hivi unajua kuwa kifo kimtokeapo mwanadamu, huzuni na majonzi ni kwa ndugu wa karibu, siyo marehemu? Hapa ni kwa mara ya kwanza, ile adhabu ya Mungu kwa Adam na Eva, wanaionja ubaya wake.

Unakumbuka kisa cha kifo cha mtoto wa Daud kwa mke wa Uria? Mtoto alikuwa na hatia gani? Kosa la mfalme Daud, kwa nini kifo kikampate mtoto? Jibu, kifo huwaumiza walio hai na siyo marehemu. Ndiyo maana, wengine tunaona ni vema adhabu ya kifo ikafutwa.
 
Muuaji ni muuaji tu.
 
Hakuna sehemu nimesema Mungu anapanga kifo. Nadhani unasoma ukiwa na fikira zako na kupandikiza maneno. Soma tena. Nilichosema kuwa Mungu anajua sababu ya kifo, iwe mtu kauwawa na shetani, iwe mtu kauwawa na binadamu Mungu utambua. Na akiamua kutoruhusu kifo hata shetani hawezi. Mungu anakuwa hajaamuuwa mtu huyo kufa.
Ndo nikasema alimkataz ashetani asitoe roho ya Ayubu.

Mada yangu aijaongelea magufuli kusemwa kabla ya kufa. Hapa naongelea kifo cha Magufuli kinavyomhukumu! Ndugu yangu inaonesha uelewi kabisa mada hii inaongelea nini!
Mie nimejikita hukumu za watu wanazo zitoa kwa Magufuli baada ya kufa.

Ndo nikatoa rai kwa jamii tusimmuhuku Magufuli sisi si Mungu kujua kuwa kwanini magufuli kafa, na kusema kafa kwa mabaya yake. Nikasema hayo tumwachie Mungu. Awe ametenda mabaya Mungu ndiyo anajua si binadamu.

Hayo unayosema kaanza kuongelewa hajafa siyo mada yangu. Waweza kuanzisha nawe mada yako. Mada yangu ni hukumu baada ya kifo.
Kuhusu kuijua Biblia naijua sasa wewe si mwalimu wangu na sijakwambia wewe hujui. Uwa sishindani katika neno la Mungu, kwani roho wa Mungu ndiye utuwezesha na kutufunulia hata yale tusiyo yajua. Hivyo sijaja hapa kushindana.

Na pia hata shetani anaijua Biblia, alimwendea na kumjaribu Yesu kwa kutumia vifungu na mistari ya Biblia. Kikubwa ni nini kilichopo ndani ya mtu, je amejazwa na roho wa namna gani amwongozae kusema asemacho.
Hata Petro aliingiwa na shetani, Yesu akamkemea shetani na kusema rudi zako nyuma shetani. Alishajua Petro kaingiliwa na roho ya tofauti.
 
Tunapangiana kupenda au kuchukia tangu lini?
 
Nafura unapojenga hoja. Kaini asingeweza kuuwawa na wazazi wake. Wakati huo alikuwepo Adam na Eva, pamoja na watoto wao wawili. Hivyo bado adamu aliendelea kuzaa si kwamba hakuendelea kuzaa, hivyo kizazi kingeendelea. Swala la kutouwawa kwa Kaini lilikuja baada ya Kaini mwenyewe kumlilia Munguhuku akiomba msamaha na kusema takuwa na maisha ya namna gani kwa hilo alilolitenda. Aliona atakoswa ushirikiano katika jamii na kuonekana mbaya na hata pengine kuuwawa nae pia. Kumbuka katika agano la kale ukiuwa nawe unauwawa.
ndipo Mungu akampunguzia adhabu na kusema mtu atakae muuwa kaini atahadhibiwa mara zaidi.
Na Mungu alimchukua na kumpeleka nchi ya mbali aliishi huko na kuwa na familia, wakati huku adamu na Eva walizaa watoto kibao.
Swala la Daudi na mke wa Uria, Mungu kweli alifanya ili Daudi ajifunze. Kuwa haikuwa haki kuchukua mke wa mtu kwa kumuuwa mmewe. Ndo maana baada ya Daudi kujua Mungu ndo katenda kifo cha mtoto kutokea uzuni ilimtoka na akavua magunia ya kuomboleza na kuvaa nguo nzuri huku akiwa mwenye furaha.
Ndo maana vifo vingi tunaambiwa tusilie sana au kusema sana tukaja kufuru. Hatujui Mungu alikuwa na sababu ipi kifo kutokea.
Nakubaliana nawe, ni heri adhabu ya kifo indolewe. Tuna baadhi ya majaji wengi wamestaafu, katika hukumu zao ukwepa sana kumhukumu mtu adhabu ya kifo.
Wakati fulani kuna jaji alisaidia dada mmoja alie muuwa mwanae wa kumzaa, japo kesi ilikuwa murder lakini jaji alisema moyo wa binadamu umejawa hofu, mpaka mtu anauwa mtoto wake mdogo wa kumzaa kuna jambo ambalo si zuri na hasa uwenda mama alikuwa na roho mchafu. Hivyo tukimpa murder yule mdada tutamuuwa kwa jambo ambalo akufanya kwa akili zake. Tanzania hakuna sheria za imani za majini na mashetani au uchawi. Yule dada alipelekwa kupimwa akili madakitari walisema ni mzima hana tatizo la akili, lakini ndugu walidai yule dada anamashetani, ndo maana alimshika mtoto wake na kumnyonga. Wakati nafagia fagia pale mahakama Kuu, jaji akawataka wanasheria kusoma sheria mbalimbali na hasa toka Afrika magharibi kule Nigeria, na kuangalia kesi za Nigeria zenye mlengo au kushabiana na kesi ya huyo dada. Nigeria wanasheria za kichawi na mashetani kulingana na mila zao. Ni moja ya kesi ambayo sinto isahau ktk maisha yangu. Ila jaji alionekana anaupendo. Nakumbuka alituita wote ofisini kwake kujadili kwanza kabla ya kesi kuanza kusikilizwa. Nami mfagiaji nikabahatika kuwepo katika mjadala huo. Usiniulize kwanini. Huyu jaji siku zote alijaribu kutotoa adhabu ya kifo.
Nilimpenda sana huyu jaji, alikuwa na moyo wa msamaha, moyo wa unyenyekevu. Aliachia watu wengi huru hasa anapokuwa kesha kaa mahabusu muda mrefu.
 
Tunapangiana kupenda au kuchukia tangu lini?
Mtu anapokuwa hana hoja. Hoja yangu binadamu hatujapewa mamlaka ya kuhukumu, ndo maana Neno la Mungu linasema usihukumu usije hukumiwa. Ni wapi nimesema mpende au upende! Niwapi nimesema uchukie? Soma na elewa mada. Narudia naongelea HUKUMU.
Na kuhukumu si kwamba unapenda au upendi au unachuki.
 
Weye umeona wapi huyo rafiki yako anahukumiwa?Acha kujishukushuku utayumba maishani.
 
Hapa sijadili matendo ya mtu najadili mwanadamu kumhukumu mwanadamu mwingine baada ya kufa. Je ni haki? Neno la Mungu linasema Usihukumu ukaja hukumiwa. naongelea kifo si penye uhai.
Swala la kuomba si lazima kujikusanya, naamini Lisu aliombewa na watu wengi binafsi. Nakumbuka hata nami nilikuwa namwombea. Na sikukatazwa kuomba binafsi ndani kwangu.
Na uzuri Mungu hapokei maombi kwa sababu ya T shirt zilizo andikwa, bali upokea maombi ya toka rohoni na yakweli. Vya kiroho uenda kiroho na si kimwili.
Makamu wa Rais mama Samia, Rais msitaafu Mwinyi, Jaji mstaafu na wengineo walienda mbona sikuona hizo jinai unazosema, ebu nitajie kesi ipi ilikuwa mahakamani kwa watu walioenda kumuona Lisu?
Watanzania tusiwe watu wa kuweka chumvi au kuzidisha maneno ili tu kutaka kuonesha uhalali.
 
Weye umeona wapi huyo rafiki yako anahukumiwa?Acha kujishukushuku utayumba maishani.
Nijishuku na nini, siishi kwa kujipendekeza, najitambua na naendesha maisha yangu bila ushabiki. Naongea kilichopo. Mwenye kuyumba ni wewe ulie na chuki za marehemu. Mtu yoyote anae ishi kwa chuki hana furaha ya maisha. Nakuona weye hapo ulivyoyumba. pole sana.
 
Huyo Magufuli wako alikuwa ndio Mungu wako? Yeye Magufuli alikuwa na mamlaka ya kuhukumu binadamu wenzake na kuwaua. ...eboo. ! Kazi ya kuwaita watu ni ya Muumba, na Magufuli hakupewa mamlaka ya kuhukumu binadamu. Watu wanaokotwa viroba baharini, Risasi mchana kweupeee na hakuna uchunguzi. Tena afe mara 2 huko Akhera...unaleta kichefu chefu
 
Vile mwendakuzimu amefurahia andiko lako refu kutokea huko kuzimu😁😁😁
 
Watu wengine wa ajabu sana mada inaongelea kitu kingine, mtu anakurupuka huko na mahesabu yake, sipo hapa kusema Magufuli alifanya hki bali... usihukumu usije ukahukumiwa.
Pia Mungu wangu nae mwamini si wakuchezea, Na mwamini Mungu mmoja tu, alie ziumba mbingu na nchi. Hivyo usiniletee za kuleta, na uwa sijibiwi ovyo, nakuonya.
Kama nakuletea kichefu chefu ingia chooni katapike. Mie natahadhalisha kuwa hatupo kuhukumu kazi ya kuhukumu ni Mungu. Magufuli awe ametenda Mabaya au mazuri anae hukumu ni Mungu tumwachie yeye.
Unapo jadili hoja jadili kwa adabu. Hivi unadhani mimi sijui matusi au dharau! Ebo!
 
Too long to go through

Labda ungeandika amefufuka ningesoma haki.
 
Too long to go through

Labda ungeandika amefufuka ningesoma haki.
Uvivu wa mtu kusoma si dhamana kwa wengine wenye uwezo wa kusoma. Sikulaumu nami zamani nilikuwa mvivu kusoma, ila nikajikuta nimeenda kusoma sehemu fulani kwa wiki natakiwa kusoma vitabu si chini ya kumi na page kibao. Mbona nilibadilika.
Ila nikagundua ndo maana wenzetu ni waelewa wa mambo mengi. Wanasoma sana, tena sana.
 
Hitimisho langu kwenye huu mjadala baada ya hapa sitachangia chochote kwenye huu Uzi.
1.JPM alilikuwa kiongozi muuwaji.
2.JPM alikuwa kiongozi aliyedhulumu haki.
3.JPM alipenda kuabudiwa alikuwa infallible asiye na makosa na aliwaumiza waliomkosoa.
Nk
Kiufupi Marehemu magufuli alikuwa kiongozi mbaya mno katika historia ya taifa letu alipotawala taifa zima lililia juu ya ukatili wake. Watanzania walimlilia Mungu naye 17/3/2021 akasikia kilio Chao. Na kufunika ubaya wake alifanya yafuatayo.
1. Alitunga Sheria kandamizi dhidi ya media.
2.ALIUWA wakosoaji wake walioponyoka wakakimbia nchi.
3.Alitengeneza vikundi Kama MATAGA vikundi vya propaganda za kumsifu na kumuabudu hata kwa mabaya ya wazi.
4.Alitumia ujinga wa watanzania (kukosa kwao elimu) kuwahadaa aonekane mwema mfano kugawa hela mbele ya kamera kwa masifa ya kijinga wakati hata vitabu vya dini vinasema ukitoa hata mkono wako wa kushoto usijue ulichotoa.
Alijidai na kujibrand mtetezi wa wanyonge kumbe alikuwa mtetezi wa wajinga.
Alienda kwenye madhabahu ya bwana asubuhi kujionyesha yeye ni mchamungu kumbe ikifika jioni anavaa mzula usoni na kugeuka muuwaji mtekaji na mkwapuaji.

Mwisho vyombo vya ulinzi na usalama visije kamwe kuruhusu RAIS MUNGU katika ardhi ya taifa letu.
 
Hujambiwa unamfanyia kampeni umeambiwa unamtetea baada ya watanzania kumtia hatiani kwa makosa yake ya kujiona kuwa yeye ni bora kuliko yeyote kukandamiza watu kuzurumu na mfano wa hayo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…