Hayati Dkt. Magufuli anapohukumiwa kwa kifo chake

Magufuli asafishiki hata iweje kaua watu mno yule mzee..na ndo kitu kinachofuta mazuri yake
 
1.All in all, mtu huyu hatetembea tena kwenye uso wa dunia.
2. History lazma iandikwe ili watoto wetu wajue yawapasa kutenda yapi wanapopata madaraka
3.Kibinadamu ni vigumu sana kutokujisikia ahueni kwa kifo cha mtu aliyetulazimisha tumwabudu
4. Mungu anisamehe kwa namna furaha inavyojaa moyoni nikikumbuka kifo cha huyu bwana,....yaan ilifikia mahala ilifikia watu wakamfananisha na YESU.
 
LoL! The man is gone. Na ameshasahaulika. Learn to live with that reality! Ameenda na hatorudi!
 
Nashukuru kwa kile ulichoeleza, na kile ulichoniongezea ambacho sikuwa nacho.

Lakini pia nakupongeza kwa kutokuhamaki wakati wote wa michango ya kila mmoja.

Wazo muhimu, wanadamu tumeaswa kutokuhukumu tusije tukahukumiwa. Andiko jingine lasema, hata tuwe na dhambi kubwa namna gani, tukiomba toba iliyo njema, tunapata msamaha kamili wa dhambi zetu kwa kuwa bwana wetu ni mwingi wa huruma na msamaha, si mwepesi wa hasira.

Juu ya marehemu, tunaweza kusema alifanya hiki kibaya na kile kizuri, lakini hatuwezi kusema ndiyo sababu ya kifo au kuishi kwake maana waovu na wema, wote hufa na wote huishi. Na kuna wakati waovu huishi zaidi kuzidi hata watu wema.

Yu wapi huyo ndugu yetu, miongoni mwa watakatifu au la, hutegemea hekima ya Mungu na maisha yake au ya kila siku, au dakika yake ya mwisho. Tukumbuke mfano wa Yesu juu ya mshahara wa wafanyakazi, mwingine aliyeanza tangu asubuhi na mwingine dakika za mwisho, lakini wote walipata mshahara mmoja. Hata kama tukayajua yote mabaya ya marehemu (jambo ambalo si rahisi), hakuna ajuaye dakika yake ya mwisho alimwambia nini Mungu wetu aliye mwingi wa msamaha.

Kifo ni ibada kwa tuliobakia, ni ujumbe mkuu kuwa siku moja nasi tutakufa. Tutakufa namna gani, ni fumbo. Kufa kwa mateso makubwa au bila mateso, siyo uthibitisho wa maisha yetu kuwa mema au mabaya. Kuna wakati watu wema hufa kwa mateso makali kuliko waovu, ili mateso yao yawe sadaka kwaajili ya wengine. Hivyo ni kosa kufikiria kuwa kila afaaye kwa mateso makali, basi alikuwa mdhambi mkubwa - nje kidogo ya mada.

Wale ambao maisha yao yalikuwa katika hatari ya kifo, mateso na dhuluma, na wengine wakamlilia Mungu, wana kila sababu ya kumshukuru Mungu pale anapowaondolea hatari hizo kwa namna yoyote iwayo. Hawa hawamhukumu mtu bali wanamshukuru Mungu kwa wema na ulinzi wake na kwa kuwa amewapa nafasi ya kuishi kwa amani na matumaini yaliyo hai.
 
Mkuu usiminyane Magufuli amekufa
Full stop
 
Nyie mnachuki pum.vu aliwanyoosha kwa wizi wenu shangilieni maana Sasa hayupo wa kuwazuia kuiba

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Furahi nafsini mwako maana umeweza kutukana.

Sisumbuliwi wala kuteseka kufikiria namna ya kumjibu anayetukana. Nateseka na kulazimika sana kutafakari mtu anapotoa hoja.

Anayetukana ni dhahiri, hana chochote cha kujenga moyoni na akilini, ni wa kuonewa huruma kuliko kumchukia.

Ujaliwe hekima, japo ndogo sana, ili uwepo wako Duniani uache hata kitu kidogo cha kuwajenga.
 
Usiangaike nao hao, maneno yamewachoma. Kwa hiyo wanajibaraguza!
 
Itoshe kusema tu, wew ni sukuma gang. Jiwe alishakufa kutokana na ujuaji uchwara wake.
 
Alikuwa na mamlaka ya kuunda tume ya kijaji kufuatilia matukio haya ambayo yalikuwa na public interest, he never did that, now will you tell us the motive behind! Makosa yapo ya kutenda na kutokutenda yote yaweza kuwa makosa.
 
Yeye mwenyewe alijisababishia hayo matokeo kwahiyo kama ni lawama ni zake mwenyewe hivyo mleta uzi usitafute wa kumlaumu,
Kama alivyosema Mzee Mwinyi kuwa "maisha ya duniani ni sawa na hadithi tu hivyo kuwa hadithi nzuri kwa hao watakaosimuliwa" hii maana yake utakavyoishi ndivyo utakavyosimuliwa kwa watu wakati wewe haupo umeshatangulia mbele ya haki.
Maisha ya bongo wakati mwingine yamejaa unafiki watu wapo tayari wakusifie kwa sifa za uongo ili mradi wapate wanachokitaka kutoka kwako hivyo mtu akili kichwani mwako.
 
Sasa mbona wew ndiye mwenye chuki, unasema tusihukumu ili hali unasema jamaa atakufa kifo cha ajabu. Wasukuma bhan, hata mkizeeka bado mnakuwa vile, mkipewa madaraka mnakuwa kama Jiwe.
 
Kwani ukifa ndio hauhukumiwi kama ulifanya mambo ya hovyo? Kifo sio excuse Mzee.Kwani Hitler na madikteta wengine huwa unaona wanasifiwa? .

Uliyotenda yatakufuata hata kaburini,mbona akisemwa vizuri huongei?
 
Kwani mwenzetu wewe unasoma maandiko yapi! Si ndio hayo yanayosema auaye kwa upanga atakufa kwa upanga! Si ndio hayo yamesema ole wake amwagae damu zisizokuwa na hatia! Si ndio hayo yaliyosema yaliyofungwa hapa duniani na mbinguni pia! Be serious.
 
Soma kitabu Cha Amos ujue kuwa hakika Mungu hatafanya jambo lolote bila kuwafunulia manabii wake Siri zake.
 
Walikuwa na kiu ya kuhakikisha kama kweli amekufa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…