Hayati Lowassa alivyomponza Kikwete akatimuliwa Msasani kwa kufokewa na Mwalimu Nyerere

Hayati Lowassa alivyomponza Kikwete akatimuliwa Msasani kwa kufokewa na Mwalimu Nyerere

Tumeshazika sasa tunajibu hoja kwa hoja

Walioshadadia Kashfa ya Monduli

1) Freeman Mbowe
2) Godbless Lema
3) Chrstopher Ole sendeka
4) Anne Kilango Malecela

wote hawa wanatokea unapotokea Wewe mbaguzi

au wakati wa Kashfa ya Richmond mlikuwa bado wadogo

Waliotupiwa zigo la Monduli walifanyie kazi walikuwa Home boy ambao leo ndio hao hao wanalalamikia wakwere walivyokuwa akili nusu Mlingoti

hao hao ndio walikuwa wanamtukana Mkwere kuwalinda wana mtandao!
Mwanasiasa Mahiri na madhubuti lazima uwe mtulivu, akili nyingi sana na mvumilivu na sifa zote hizo Adui yenu mkuu anazo

Sifa kubwa sana ambayo Mkwere na Mzee wa Monduli pamoja na kutofautiana walikuwa nayo ni kutopenda kulalamika lalamika

ukim snitch anaku snitch na wakikutana kila mmoja anajibu am fine

Walimzunguka Bosi kwny Richmond nae akawapelekea moto kwa kutumia hiyo hiyo Richmond

walipotolewa nje ya Game wakaunda magenge mengi sana ya hujuma hadi migomo mikubwa mikubwa akapiga kimya akawasubiri 2015 akala kichwa

Wakahamia upande wa pili wamuoneshe show kwa kuwa wana watu na pesa nae akawaonesha ana akili na dola wakamalizana kibingwa

na wote hawakuwahi kulalamika hadharan

Kitu cha kujivunia Jk alisikiliza kilio cha Wengi cha kulipasua Kundi lake la Wanamtandao

2017 alimtumia Mzee wa Kundi Samwel Sitta kumpumzisha Ngoyai na 2010 akatumia nguvu na ushawishi wa Ngoyai kupitia NEC kuweka vipengele cha Jinsia kumpumzisha Uspika Mzee Sitta

2011 akamtumia aliekuwa Mwanamtandao wa Mzee Sumaye Ndugu Nape akampa Ukatibu wa Itikadi akaanza ku deal na mapacha watatu na Tajiri wa Igunga akavua jezi

na 2015 akakamilisha madaraka yake kwa kuhakikisha Wanamtandao hawapo tena kama kundi


Pamoja na tofauti zote na rafu zote za Siasa hakuwa na muda kuhujumu uchumi au biashara ya Mtu japo alikuwa na uwezo wa kufanya hivyo

alijua Michezo ya Siasa itaishia kwny Siasa sio kutafutana kwenye Bank Accounts na Assets za mtu
Asante sana mkuu!!

Angalau wewe unaongea facts!!

Kwamba Dola haikutaka makundi ya wanamtandao kutuamulia hatma ya uongozi wa nchi!na jk akatumika ipasavyo kusambaratisha kingmaker's!!

Watu wamejawa na hisia zaidi kuliko facts!!
 
Asee ht najiuliza hili swali, mwenye majibu atuwekee wakuu mana naskia jamaa alikuwa na mzigo tangu enzi za TANU
Ila kumbuka nyumba nyingi za NHC zilizoko upanga,kitumbini,kisutu,na city center zilikuwa za indians na nyerere alizitaifisha Akizialocate kwa msajiri wa majumba kabla ya kuhamishiwa TBA na NHC
 
Tuliokuwa ndani ya UV CCM wakati huo tunafahamu mengi sana

kama Mama Anna Makinda angeamua kuandika kitabu au kuandika ya nyuma ya pazia angeliandika vyema sana hili

Mwalimu alimwita Anna Makinda na kuna ujumbe aliotumwa binafsi kwa Jakaya na JK kabaki na siri hiyo nadhan hajawahi kuiweka hadharan aliambiwa nini na Anna Makinda

ni kama vile Mama Getrude Mongela alipopewa ujumbe rasmi na Mwalimu ampelekee Ndugu Ally Hassan Mwinyi 1985 muda mchache kabla ya uchukuaji fomu

Siasa ina mengi sana

Hatujui kwanini Jakaya baada ya kushinda kwny CCM 1995 iliamriwa kura zipigwe tena na baada ya hapo akaomba fursa azungumze japo vijana wenzie tulitamani agome

JK alikuwa Makonda wa Mwl Nyerere kwa mliokuwa hamjui

ndie alikuwa Katibu wa vikao vyote vya vita ya Kagera

ndie alietumwa kumshawishi Salim agombee Urais

ndie alie deal na Kighoma Malima n.k

pengine alipewa maelekezo maalum kuhusu Monduli maana hata Edward Moringe alitajwa sana kuwa Mrithi wa Mwalimu na ikashindikana

Hayati Jaka Mwambi aliekuwa Balozi wetu Russia na Msiri wa JK angeweza kuandika kitabu kizuri kuhusu Siasa za Wanamtandao

Huwezi kuzungumza rafu na makando kando ya Wanamtandao bila ya kuwataja Viongozi wa Wanamtandao

JK angelegea na kuruhusu kuachia Nchi wana Mtandao angelaaniwa na kila kiumbe kinachopata sunlight
Kama jk alikua kama makonda was Nyerere,Basi makonda wa jpm ni Rais ajaye kama asemavyo magamba matatu happy 2030!noted!
 
Rejea hotuba za Magufuli

nakukumbusha tu

alisema hadharani hakuwa na Mpango wa kuchukua fomu ila alienda Ikulu kumshtaki Saada Mkuya kwa kutompa pesa za kulipa wakandarasi 900 billion , Jk akamuuliza Wewe huchukui fomu ?akamuuliza ninatosha ? akamjibu Wewe kachukue kutosha au kutotosha tutajua Sisi

Hapo maana yake Rais alikuwa na Plan Kadhaa kutokana na yatakayojiri

waki react hivi itakuwa hivi na jinsi walivyo react wakaamua kadri walivyoamua na iliyobaki ni historia

Sina uhakika ila ninaamini

Jakaya, Mkapa, Mangula na Kinana walikaa kama kamati kuamua nani awe nani kwa kutumia report na ushauri wa Mamlaka za kiuchunguzi na pale Dodoma walienda kutekeleza tu maamuzi maana hata Mgombea mwenza Samia anatuambia Kamati kuu walikuwa wanakula biscuit wakati vingunge wanakamilisha taratibu kupitia chumba maalum
Mkuu unaandika ukweli nahisi wewe unahudumu kitengo cha Siasa.

Ukifuatilia urais wa Magufuli ni wazi ulikuwa wa bahati tu na hii comment yako inadhihirisha hilo
 
Alianza kidogo kidogo akiwa CCM mikoani.aliposhinda ubunge 1990 na kuwa ofisi ya waziri mkuu kitengo cha maafa alizipiga kweli,akiwa ardhi ndio balaa kajimilikisha ardhi na viwanja vingi sana prime areas,kaingia mikataba ya kimagumashi sana,aliwahi kumtapeli hadi john malecele mgawo wa rushwa,malecela skiwa bosi wake,jamaa slikuwa fisadi kweli sio uongo
hakumdhulumu malecele..iliikuwa kuna ununuzi mkubwa wa magari lowasa akashangaa bosi anataka kampuni mbovu ipewe ..baadaa ya magar kuja .wakaleta dola mil 2 cash ofisini sasa miaka hiyo hakuna simu kuja ofisini ndo kumkuta lowasa akawaambia anajua mzigo huo akapokea akaficha. Lowasa akakausha naxo mzee kuziulizia akamwambia tukamuulize rais .so hata ingekuwa ww mtu alitaka akupige bil 6 tena hakushirikishi ili ale apige ale mwenyewe je ww ungempa hata mia
 
Binafsi nimwombea JK na viongozi wetu wote wakuu waliopo maisha marefu na yenye baraka tele, wamefanya mengi kwa maslahi mapana ya Taifa letu na Mungu Mwenyezi awajalie hekima zizidi na kutuachia urithi mzuri na misingi na mfumo imara kuhakikisha Taifa letu Tanzania li salama na katika mikono salama , na kwa Viongozi wetu walio lala Mungu Mwenyezi awajalie pumziko la amani la milele 🙏
 
Kama jk alikua kama makonda was Nyerere,Basi makonda wa jpm ni Rais ajaye kama asemavyo magamba matatu happy 2030!noted!
JK na George Bush huwa wanachukuliwa poa ila nikwambie hao ni wanasiasa kwa kurithi pia wako vizuri kichwani na ni watoto wa mjini,mafias.Geoge Bush kadoma Yale universitu chuo borasana kule USA😃JK ana bachelors toka UDSM mwaka 1975 kipindi hicho wasomi ni wachache sana nchini,makonda hata kuandika sentensi moja ya kingereza hawezi
 
Kitabu kimeshaandikwa muds mrefu huko Jijini New York ila mara kwa mara anaahirisha kukizindua kwa sababu kadhaa wa kadhaa na hasa sababu za kisiasa

Uongozi Institute walihusika kwa namna fulani kufanya review
Mkuu pohamba nakufuatilia hapa JF toka 2014

Unaweza kuhisi kwanini jana kikwete alitoweka pale Monduli msibani ghafla tena akavunja protocol ya kuondoka meza kuu kabla mkuu wa nchi kuondoka?
Inadaiwa hata hakuaga!!
 
kumzuia Dr Ibrahim Msabah aliekuwa Waziri wa Nishati na Mbunge wa Kibaha ku approve advance payment ya 10 Billion kwa Kampuni feki ya Richmond ambayo ilikuwa ya mwisho kwenye Procurement process lakini Management ya Tanesco ikalazimishwa kwa Vimemo iwape Tender

baada ya kupewa Tender wakataka walipwe advance payment hiyo wakati haikuwemo kwny terms of contract

ndipo Mh.Rais akastukia kitu akatumia weledi wake wa kimedani akajua Watu aliowaamini wameanza kumzunguka.

Media zikaanza ku report hiyo kashfa nae akaridhia uchunguzi huru kwa Bunge kuchunguza

Report kabambe ya Uchunguzi ya Dr Harrison Mwakyembe, akisaidiwa na Eng. Stella Manyanya kama Makamu Mwenyekiti pamoja na Wajumbe kina Lucas Selelii Mbunge wa Nzega wa wakati huo wakafanya kazi kubwa na ya kizalendo

matokeo kuletwa Bungeni ikabidi ijadiliwe then watuhumiwa ambao ni Wabunge wajibu hoja

Hoja za Utetezi zilipoanza alisimama Peter Serukamba Mbunge wa Kigoma Mjini kumtetea Lowassa

lowassa akamuomba Spila Sitta amzuie Serukamba na badala yake akatangaza kujiuzulu akafuatia Karamagi then Msabaha

Rostam akiwa Katibu wa Uchumi wakati huo akabadilishwa baada ya muda mfupi

JK hakuwafanyia figisu lolote zaid ya kuwatoa kwny Serikali yake na nongwa ikaanzia hapo
Kikwete kuruhusu report ijadiliwe bungeni.

Ndio ilikuwa mwisho wa mbio za Urais hii ajali ilikuwa nzito kwa Edo
 
Binafsi nimwombea JK na viongozi wetu wote wakuu waliopo maisha marefu na yenye baraka tele, wamefanya mengi kwa maslahi mapana ya Taifa letu na Mungu Mwenyezi awajalie hekima zizidi na kutuachia urithi mzuri na misingi na mfumo imara kuhakikisha Taifa letu Tanzania li salama na katika mikono salama , na kwa Viongozi wetu walio lala Mungu Mwenyezi awajalie pumziko la amani la milele 🙏
Makubwa gani labda kumshawishi mama kuuza bandar na kujitajirisha
 
Binafsi nimwombea JK na viongozi wetu wote wakuu waliopo maisha marefu na yenye baraka tele, wamefanya mengi kwa maslahi mapana ya Taifa letu na Mungu Mwenyezi awajalie hekima zizidi na kutuachia urithi mzuri na misingi na mfumo imara kuhakikisha Taifa letu Tanzania li salama na katika mikono salama , na kwa Viongozi wetu walio lala Mungu Mwenyezi awajalie pumziko la amani la milele 🙏
NAKUAMBIA HIVI HUYU KIKWETE HUYU NA MADHAIFU YAKE YOTE!AMETUWEKA RELINI WENGI!!

KWASISI WATOTO WA MASKINI SISI AMBAO KALAMU NDIO UKOMBOZI BILA JK TUNGEPATA WAPI PA KUSHIKA!!?

ENZI ZILE AWAMU YA NNE DEGREE ZETU ZILIONEKANA ZA MAANA HATA KAMA MZAZI AKITOBOKA ANAJUA ZINARUDI,SASA HIVI AISEH UNAWEZA TEMBELEA KICHWA KAMA MDUNDIKO!!

KWA HILO TU NAMHESHIM KAULI MBIU YA "MAISH BORA KWA KILA MTZ "NAIHESHIMU HADI KESHO!!

MENGINE HAYO NI YA KIBINAADAMU,UADILIFU HUPIMWA KWA KIWANGO CHA TAMAA ALICHOZALIWA NACHO MTU!!

CHA MSINGI AIACHIE TANZANIA YETU IFANYE MAAMUZI BORA KWA MSTAKABALI UJAO NA SIO HISIA ZAKE!!
 
JK na George Bush huwa wanachukuliwa poa ila nikwambie hao ni wanasiasa kwa kurithi pia wako vizuri kichwani na ni watoto wa mjini,mafias.Geoge Bush kadoma Yale universitu chuo borasana kule USA😃JK ana bachelors toka UDSM mwaka 1975 kipindi hicho wasomi ni wachache sana nchini,makonda hata kuandika sentensi moja ya kingereza hawezi
😂😂😂😂😂😂😂 Tunajivunia kiswahili mkuu!!

Siku hizi hata ukitoa hotuba ya kiswahili congress ya America utaeleweka tu coz wanavaa translator!!
 
Back
Top Bottom