GUI1
JF-Expert Member
- Oct 4, 2017
- 4,007
- 5,290
Safi sanaTumeshazika sasa tunajibu hoja kwa hoja
Walioshadadia Kashfa ya Monduli
1) Freeman Mbowe
2) Godbless Lema
3) Chrstopher Ole sendeka
4) Anne Kilango Malecela
wote hawa wanatokea unapotokea Wewe mbaguzi
au wakati wa Kashfa ya Richmond mlikuwa bado wadogo
Waliotupiwa zigo la Monduli walifanyie kazi walikuwa Home boy ambao leo ndio hao hao wanalalamikia wakwere walivyokuwa akili nusu Mlingoti
hao hao ndio walikuwa wanamtukana Mkwere kuwalinda wana mtandao!
Mwanasiasa Mahiri na madhubuti lazima uwe mtulivu, akili nyingi sana na mvumilivu na sifa zote hizo Adui yenu mkuu anazo
Sifa kubwa sana ambayo Mkwere na Mzee wa Monduli pamoja na kutofautiana walikuwa nayo ni kutopenda kulalamika lalamika
ukim snitch anaku snitch na wakikutana kila mmoja anajibu am fine
Walimzunguka Bosi kwny Richmond nae akawapelekea moto kwa kutumia hiyo hiyo Richmond
walipotolewa nje ya Game wakaunda magenge mengi sana ya hujuma hadi migomo mikubwa mikubwa akapiga kimya akawasubiri 2015 akala kichwa
Wakahamia upande wa pili wamuoneshe show kwa kuwa wana watu na pesa nae akawaonesha ana akili na dola wakamalizana kibingwa
na wote hawakuwahi kulalamika hadharan
Kitu cha kujivunia Jk alisikiliza kilio cha Wengi cha kulipasua Kundi lake la Wanamtandao
2017 alimtumia Mzee wa Kundi Samwel Sitta kumpumzisha Ngoyai na 2010 akatumia nguvu na ushawishi wa Ngoyai kupitia NEC kuweka vipengele cha Jinsia kumpumzisha Uspika Mzee Sitta
2011 akamtumia aliekuwa Mwanamtandao wa Mzee Sumaye Ndugu Nape akampa Ukatibu wa Itikadi akaanza ku deal na mapacha watatu na Tajiri wa Igunga akavua jezi
na 2015 akakamilisha madaraka yake kwa kuhakikisha Wanamtandao hawapo tena kama kundi
Pamoja na tofauti zote na rafu zote za Siasa hakuwa na muda kuhujumu uchumi au biashara ya Mtu japo alikuwa na uwezo wa kufanya hivyo
alijua Michezo ya Siasa itaishia kwny Siasa sio kutafutana kwenye Bank Accounts na Assets za mtu