Hayati Lowassa alivyomponza Kikwete akatimuliwa Msasani kwa kufokewa na Mwalimu Nyerere

Hayati Lowassa alivyomponza Kikwete akatimuliwa Msasani kwa kufokewa na Mwalimu Nyerere

Ni vema kuweka records Sawa.
1995 majina matatu yalipelekwa mkutano mkuu.
Wagombea walikuwa
Cleopa Msuya (Waziri Mkuu na Makamu wa kwanza wa Rais)
Benjamin Mkapa (Waziri wa Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia)
Jakaya Kikwete (Waziri wa Fedha)

JK aliongoza kwa kura akifuatiwa na BWM na Msuya akawa wa 3.
Katiba ya CCM ilitaka mshindi awe na zaidi ya 51%, kitu ambacho JK hakufikisha.

Ni uongo kuonesha JK alionewa.

Ndio maana aliposhinda kwa wingi wa kura 2005 kwa kuwabwaga SAS na Mark Mwandosya, alikuja na kauli..."safari hii, kura zimetosha".

Hoja za wazi ni vema zikajengewa hoja kwa uwezi maana kumbukumbu za 1995 tunazo.

Wasalaam!
Acha porojo. Kura za maoni tangu na tangu haziangalii mtu kupata asilimia zaidi ya 50.

Hata leo hii majimboni kura za maoni huwa zinapigwa na mtu akizidiwa hata kura moja tu basi shughuli imeisha. Unaelewa maana ya kura ya maoni?

Mwaka 1995 baada ya duru ya kwanza ya kura Kikwete aliongoza na alipaswa ndiye awe mgombea. Hakuna katiba wala kanuni iliyoongelea chochote kuhusu kura ya maoni mtu kupata zaidi ya asilimia 50. Ni kamati ya uchaguzi ndio ilileta huo muongozo baada ya kuona mtoto wa mjini kawakalia kooni.

Wakati huo aliyekuwa mwenyekiti wa vijana mkoa wa Dar-es-salaam marehemu Masaburi alihoji hilo ila wazee wa chama wakamnyamazisha. Hata marehemu Sukwa Saidi Sukwa, mjumbe wa sekretarieti ya CCM taifa na katibu wa UVCCM alijua wazi utaratibu haukufuatwa.

hizo ni porojo tu. Nchi hii ina wenyewe. Katiba na kanuni si chochote si lolote. Hata Lowassa hakukatwa jina na kamati kuu bali ni watu wachache walitimba kwenye kikao na majina yao matano mfukoni. Kumbuka marehemu mzee Ngombalimwilu alilalamikia hili.
 
Magufuli alishindwa uchaguzi ule, kura za mmonduli zilikuwa nyingi zikazikwa. Lkn kwa nn magu aliwaadhibu Januari na wenzake ila Emmanuel nchimbi akampa ubalozi?? Wakati nchinbi alimuunga mkono mmomonduli waziwazi??
 
Kwenye hiyo hotuba Jakaya aliongea nini? Mbona unatupa kazi ya kupatwa hisia bila sababu🤣
Weka japo Summary Mkuu.
Summary ni jk alikubali matokeo na akatangaza kuvunja mtandao na kutaka wote sasa wamusupport mkapa,,ndo nyerere akasimama kupiga makofi,watu wakafuatia kusimama kupiga makofi huku mkapa akitoka na kwenda kumkumbatia jk🤷
 
Another sadist fella
Roho ya kwa korosho tu, kwa nn mnorth ana pesa kuliko yeye. Amekufa maskini hakuna mtoto.wake hata mmoja aliyetoboa, alitaka waTZ wabaki maskini. Huyu mwanakwenda naye kafuata ujinga uleule eti kanda fulani usipeleke fedha, wawasubiri wenzao. Kalagha baho, yuko wapi? Kwenda mwana kwenda kafie mbali kama ulivyomtumbua yule baba na kweli akaenda kufa. Dunia jamani, kweli kila kwenye ngoma na acheze
 
kumzuia Dr Ibrahim Msabah aliekuwa Waziri wa Nishati na Mbunge wa Kibaha ku approve advance payment ya 10 Billion kwa Kampuni feki ya Richmond ambayo ilikuwa ya mwisho kwenye Procurement process lakini Management ya Tanesco ikalazimishwa kwa Vimemo iwape Tender

baada ya kupewa Tender wakataka walipwe advance payment hiyo wakati haikuwemo kwny terms of contract

ndipo Mh.Rais akastukia kitu akatumia weledi wake wa kimedani akajua Watu aliowaamini wameanza kumzunguka.

Media zikaanza ku report hiyo kashfa nae akaridhia uchunguzi huru kwa Bunge kuchunguza

Report kabambe ya Uchunguzi ya Dr Harrison Mwakyembe, akisaidiwa na Eng. Stella Manyanya kama Makamu Mwenyekiti pamoja na Wajumbe kina Lucas Selelii Mbunge wa Nzega wa wakati huo wakafanya kazi kubwa na ya kizalendo

matokeo kuletwa Bungeni ikabidi ijadiliwe then watuhumiwa ambao ni Wabunge wajibu hoja

Hoja za Utetezi zilipoanza alisimama Peter Serukamba Mbunge wa Kigoma Mjini kumtetea Lowassa

lowassa akamuomba Spila Sitta amzuie Serukamba na badala yake akatangaza kujiuzulu akafuatia Karamagi then Msabaha

Rostam akiwa Katibu wa Uchumi wakati huo akabadilishwa baada ya muda mfupi

JK hakuwafanyia figisu lolote zaid ya kuwatoa kwny Serikali yake na nongwa ikaanzia hapo
☝️🙆
 
Msli
Sho...
Nimesoma hayo hapo juu kuhusu Prof. Malima na ningependa na mimi niseme machache niyajuayo kuhusu Prof. Malima.

Katika Bunge mwezi June 1994 Prof. Malima akiwa Waziri wa Fedha alileta mswada kuwa misamaha yote ya kodi iwe chini ya Waziri wa Fedha badala ya kuiachia iwe katika mamlaka nyingi tofauti.

Maadui zake ndani ya Bunge wakalalamika kuwa Prof. Malima alikuwa anataka kujijengea himaya.

(Kwa nini Prof. Malima alikuwa na maadui ni mada ya kujitegemea).

Hata hivyo fikra zilitulia na mantiki ikatawala kuwa hilo ni jambo jema na mswada ule ukapita.

Baada ya mwezi mmoja kupita wakati Prof. Malima yuko nje ya nchi Baraza la Mawaziri likaitishwa kwa shinikizo la Waziri Mkuu John Malecela akiungwa mkono na mawaziri wanne wakongwe nia ikiwa kugeuza suala la misamaha ya kodi uliopitishwa mwezi mmoja tu uliopita.

Prof. Malima aliporejea nchini na kukuta kuwa uamuzi wa Bunge kuhusu misamaha ya kodi umepinduliwa na Bunge, Prof. Malima alimtahadharisha Rais Ali Hassan Mwinyi kuhusu matokeo ya kwenda kinyume na maamuzi ya Bunge na matakwa ya wahisani.

Rais akaitisha Baraza la Mawaziri lililokaa kwa siku nne.

Prof. Malima alihimili hoja zote kutoka kwa maadui zake katika serikali akitetea uamuzi wa Bunge.

Baada ya siku nne Baraza la Mawaziri lilirejea nyuma katika uamuzi wa Bunge.

Maadui zake waliumia sana na chuki yao dhidi yake ikazidi.

Hayo yote ya kuwa Prof. Malima alikuwa fisadi si kweli.

Prof. Malima hakuwa na mali nimemuona kwa karibu sana nyumbani kwake jirani na Victoria na nimeiona nyumba yake Kisarawe siku ya mazishi yake.

Prof. Malima hakuwa na mali na kama alivyokuwa akipenda kusema katika uhai wake, ‘’Hakula cha mtu.’’

Ametajwa hapa Kikwete kuwa alipewa nafasi ya Waziri wa Fedha badala ya Prof. Malima lakini mwandishi kaishia hapo tu.

Inataka ushughulishe bongo lako ujiulize kwa nini Kikwete?

Yapo mengi.

Kwa nini hakuyasema mengine na ni muhimu katika historia ya Prof. Malima?

Hakuyasema inawezekana kwa kuwa hayajui.

Malima alichafuliwa na story ya fedha zake sijui kuwa freezed itakuwa fake
 
Mwalimu hakuchukia matajiri halali wenye kulipa kodi !
Bali aliwachukia wenye mali zisizofahamika zilipatikanaje !
Huwezi kutumikia mabwana wawili !

Ukitaka utajiri tuachie kazi na ofisi yetu uende ukafanye biashara halali kisha ulipe kodi !
Huo ndio ulikuwa msimamo wa Mwalimu Nyerere !
Msidanganywe !! 🙏🙏
Nyerere alitaifisha nyumba za watu kwa maelfu,,unaweza ku justify vipi hii?watu wamesota tangu ukoloni huko,akaja kuchukua majumba...
 
Alivyokuwa anajitapa kichinjio cha 2015 anacho yeye alikuwa anamaanisha nini??

Baada ya kuwaondoa hao kwenye serikali yake, Rushwa na ufisadi wa kutisha uliisha??
Naona hujaelewa,pohamba anamaana,baada ya kugundua kuna watu wake wanamzunguka concerning ishu ya Richmond,,JK alimpiga stop msabaha waziri wa nishati kulipa advance na akabariki kamati ya mwakyembe kufanya uchunguzi,,then things started to happen,,
Ni Rais wa ajabu tu atakubali mtu aliyechafuliwa na kashifa eti ampe nchi kwa kisingizio eti ni Rafiki wa karibu,,
 
Naona hujaelewa,pohamba anamaana,baada ya kugundua kuna watu wake wanamzunguka concerning ishu ya Richmond,,JK alimpiga stop msabaha waziri wa nishati kulipa advance na akabariki kamati ya mwakyembe kufanya uchunguzi,,then things started to happen,,
Ni Rais wa ajabu tu atakubali mtu aliyechafuliwa na kashifa eti ampe nchi kwa kisingizio eti ni Rafiki wa karibu,,
EL hakuwa anataka favor ya JK. Alihitaji mchakato huru tu. Ni wangapi wala rushwa JK aliwakumbatia? Yeye pia hakuwa mla rushwa??
 
EL hakuwa anataka favor ya JK. Alihitaji mchakato huru tu. Ni wangapi wala rushwa JK aliwakumbatia? Yeye pia hakuwa mla rushwa??
Jk hajawahi kumbatia wara rushwa,, kumbuka ni awamu ya jk ambako mawaziri kibao walifungwa na kufikidhwa mahakamani ,wengine kujiuzulu akiwemo lowasa,msabaha,karamagi,tibaijuka,idd simba,etc,
 
Back
Top Bottom