Tofautisha kura za maoni kwenye level ya majimbo na kura za mkutano mkuu wa CCM (T).
Kinachofanyika kati ya majina 3 lazima kwenye duru kwa kwanza mshindi apate zaidi ya 51%.
1995 JK aliongoza kwa kura, akifuatiwa na BM na Msuya akawa wa mwisho.
Then kura zikarudiwa kati ya JK na BM, ndipo Mkapa akaongoza.
Tofautisha kabisa kura za maoni na kura za maamuzi ya Mkutano mkuu CCM (T).
Labda nikusaidie kujua nguvu ya mkutano mkuu CCM (T), Mkutano mkuu CCM (T) ukipiga kura; maana ya yake hayo ni maamuzi ya chama.
Wakati SSH anataka kujaza nafasi ya uenyekiti, ililazimu Mkutano Mkuu maalumu CCM uitishwe ili kumthibitisha kwa kura.
Hivyo, ondoa neno kura ya maoni kwenye kuchagua Mgombea Urais CCM. Pale ni kura ya maamuzi sio maoni.