Sho...
Nimesoma hayo hapo juu kuhusu Prof. Malima na ningependa na mimi niseme machache niyajuayo kuhusu Prof. Malima.
Katika Bunge mwezi June 1994 Prof. Malima akiwa Waziri wa Fedha alileta mswada kuwa misamaha yote ya kodi iwe chini ya Waziri wa Fedha badala ya kuiachia iwe katika mamlaka nyingi tofauti.
Maadui zake ndani ya Bunge wakalalamika kuwa Prof. Malima alikuwa anataka kujijengea himaya.
(Kwa nini Prof. Malima alikuwa na maadui ni mada ya kujitegemea).
Hata hivyo fikra zilitulia na mantiki ikatawala kuwa hilo ni jambo jema na mswada ule ukapita.
Baada ya mwezi mmoja kupita wakati Prof. Malima yuko nje ya nchi Baraza la Mawaziri likaitishwa kwa shinikizo la Waziri Mkuu John Malecela akiungwa mkono na mawaziri wanne wakongwe nia ikiwa kugeuza suala la misamaha ya kodi uliopitishwa mwezi mmoja tu uliopita.
Prof. Malima aliporejea nchini na kukuta kuwa uamuzi wa Bunge kuhusu misamaha ya kodi umepinduliwa na Bunge, Prof. Malima alimtahadharisha Rais Ali Hassan Mwinyi kuhusu matokeo ya kwenda kinyume na maamuzi ya Bunge na matakwa ya wahisani.
Rais akaitisha Baraza la Mawaziri lililokaa kwa siku nne.
Prof. Malima alihimili hoja zote kutoka kwa maadui zake katika serikali akitetea uamuzi wa Bunge.
Baada ya siku nne Baraza la Mawaziri lilirejea nyuma katika uamuzi wa Bunge.
Maadui zake waliumia sana na chuki yao dhidi yake ikazidi.
Hayo yote ya kuwa Prof. Malima alikuwa fisadi si kweli.
Prof. Malima hakuwa na mali nimemuona kwa karibu sana nyumbani kwake jirani na Victoria na nimeiona nyumba yake Kisarawe siku ya mazishi yake.
Prof. Malima hakuwa na mali na kama alivyokuwa akipenda kusema katika uhai wake, ‘’Hakula cha mtu.’’
Ametajwa hapa Kikwete kuwa alipewa nafasi ya Waziri wa Fedha badala ya Prof. Malima lakini mwandishi kaishia hapo tu.
Inataka ushughulishe bongo lako ujiulize kwa nini Kikwete?
Yapo mengi.
Kwa nini hakuyasema mengine na ni muhimu katika historia ya Prof. Malima?
Hakuyasema inawezekana kwa kuwa hayajui.