Hayati Magufuli alichukizwa sana na waliotaka abadili katiba ajiongezee muda ndio maana Ally Kessy hakurudi Bungeni

Wewe uko Iringa hapo, sogea hapo Mbarali ni jirani mtafute Mtu anaitwa Misana Kwangura. Msituketee uongo eti Kessy alitolewa na Magufuli.
Wabunge wengi wa CCM walifeli lakini Leo wako bungeni ndio tunauliza kulikoni Kesi na Hawa Ghasia tu?!
 
MMM kamaliza kila kitu kumhusu huyu jamaa. Yaani ni kwamba aendelee kulala panapomstahili
Kwamba alitaka kujiongezea muda kweli? Mlaumu kwa vitu vingine ila hilo la kujiongezea muda alilipinga kwa nguvu, kwa maneno na matendo
 
Sasa kama kura hazikutosha ulikuwa unataka abebwe mgongoni? Ukweli ni kuwa wananchi walichukizwa na hoja yake na wakamkataa kwenye sanduku la kura
 
Ulikuwa ndani ya mawazo na moyo wake?
 
Mawazo yake????Ona alichofanya 2019.Baada ya kulaumiwa na watu mbalimbali pamoja na baadhi ya wastaafu pamoja na wapinzani wote kutishia kuwa 2020 hawatashiriki uchaguzi alifanyaje?Aliwaita viongozi wa dini pamoja na baadhi ya viongozi wa dini kuwa kilichotokea 2019 hakiwezi kutokea kwenye Uchaguzi mkuu.Lakini matokeo yake mpaka leo kuna wabunge 19 feki Bungeni kwa sababu yake.Yule mwehu alikuwa anacheza na akili za wajinga.
Ulikuwa ndani ya mawazo na moyo wake?
 
Mpuuzi wewe
 
Wabunge 19? Mbona wapo mpaka muda huu ili hali yeye hayupo?

Acha basi masikhala boss
 
Kila alichokianzisha kama Mwenyekiti wa CCM pia mrithi wake lazima akiendeleze huo ndiyo msimamo wa chama kwenye ilani ya ccm iliyosimamiwa na yeye ambayo ndiyo inayotumika mpaka 2025.
Wabunge 19? Mbona wapo mpaka muda huu ili hali yeye hayupo?

Acha basi masikhala boss
 
Kwa hoja hiyo Magufuli alikuwa anaamua nani arudi bungeni! Mtu wa aina hiyo angeshindwa nini kubadili katiba?
Ndio maana nikasema mlaumuni kwa vitu vingine ila hilo la kujiongezea muda alikataa kwa vitendo na kauli mara nyingi
 
We chawa wa shetani acha uwongo. Ila pia nashukuru umethibitisha kwamba magufuli alitumia madaraka vibaya kuingilia uchaguzi na kuamua huyu awe au asiwe mbunge.
 
Ndio maana nikasema mlaumuni kwa vitu vingine ila hilo la kujiongezea muda alikataa kwa vitendo na kauli mara nyingi
Angekataa kwenye uchaguzi wa 2020 kupendelea chama chake basi mimi ningeamini aliyokuwa anasema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…