Hayati Magufuli alifanikiwaje kuwafanya watu wa vipato vya chini kumuamini kiasi kile?

Hayati Magufuli alifanikiwaje kuwafanya watu wa vipato vya chini kumuamini kiasi kile?

matunduizi

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2018
Posts
9,514
Reaction score
23,523
Jana maeneo ya matumbi matraffic wakiwa wametanda kila kona, Dereva wa daladala alipowaona tu akasema " Baba yetu amefariki sasa wameanza kutusumbua".

Kauli kama hizi zimekuwa zikisikia kwa watu wa vipato vya chini kuona kama hayati alikiwa ndio kila kitu. Na sasa hivi kila rekebisho linalotokea na litakalotokea inaonekana ni kwa sababu mtetezi wao hayupo.

Hizo mbinu alizotumia kuteka mashabiki wengi kuliko wafuasi wa chama chake ni zipi na kwa nini wabunge, madiwani na serikali za mitaa walishindwa kututeka hivyo miaka yote?

Angalau Deo Filikunjombe na yeye alifanikiwa kwa kiasi flani.

Nawasilisha
 
Alikiuwa anawaambia wao ni wanyonge na kwamba wamechezewa sana? Halafu anamalizia na kumtumbua afisa mmoja wa karibu aliyepo hapo wananchi weweeeeeeee.[emoji2223][emoji2223][emoji2223][emoji2223][emoji2223]
 
Alikiuwa anawaambia wao ni wanyonge na kwamba wamechezewa sana? Halafu anamalizia na kumtumbua afisa mmoja wa karibu aliyepo hapo wananchi weweeeeeeee.[emoji2223][emoji2223][emoji2223][emoji2223][emoji2223]
Jamaa alikuwa genius wa kufanya manipulation hatari, alaf anaongea kana kwamba ana uchungu kweli na kiukwel hamna alichowafanyia kikubwa.... Mwamba alikuwa mhuni Sana Yule
 
Brainwashing tactics. kwa mfano propaganda 24/7 TBC1

Kuminya uhuru wa vyombo vya habari, visiandike ukweli

Kuziba watu midomo wasichallange madudu yake waziwazi na hivyo jamii kuendelea kuwa gizani

Kutunga sheria kandamizi juu ya takwimu hivyo kuzuia data za kuwafumbua macho watu kutolewa au kupatikana kiurahisi

Kutumia populist approaches za kujifanya anawatetea, anawasemea, kujifanya ni mwema na mkarimu kama vile kugawa hela njiani
 
Baada ya Rais Mstaafu Kikwete kutoka Madarakani Matajiri walikuwa na Jeuri za kila aina mpaka Kuamua Uhai wa Watu Masikini na wasifanywe lolote lile kwani walimweka Mifukoni mwao.

Alipoingia Hayati Rais Dkt. Magufuli alitaka Kuwaheshimisha Masikini (GENTAMYCINE nikiwemo) kuwa hata Sisi pia ndani ya hii Ardhi ya Mama Tanzania pia tuna Thamani yetu hivyo akatupa (akatujaza) Jeuri mpaka Matajiri nao wakaanza Kutunyari (Kutuogopa)

Kwa hivi sasa ndani ya huu Utawala wa Rais Mama Samia Matajiri na Masikini bado tunamsikilizia (tunampima) Mama tuone Yeye atalia upande wowote ili tuanze Kumlaumu (Kumsiliba) japo ninavyomuona ni kama vile anataka kutuweka katika Mzani sawa kitu ambacho si kibaya pia na Mimi nakiunga mkono.
 
Njia ni rahisi tu.

Masikini wengi wana roho mbaya, wivu na akili ndogo hivyo:

Kwasababu huwa wana wivu na chuki kwa kila aliyenacho, wewe hakikisha unatukana kila siku mwenye nacho na kuwadhalilisha hadharani huku ukiwasifia wao masikini.

Tukana sana wazungu. Na hakikisha wakikupa pesa zao, hao masikini wasijue.

Dhibiti habari zote za mabaya yako, hakikisha unasifuwa na kutangazwa muda wote kwenye vyombo vya habari kwa mema tu.

Jifanye mcha mungu, na kila ukienda kwenye ibada hakikisha watu wanajua na picha zinatoka ukiwa mnyenyekevu.

Ukimsaidia ombaomba hata Jero hakikisha unachukua picha na video na zinaruka kila wakati kwenye TV ili kukuonesha ulivyo mwema .

Kila ukiongea na tajiri au mwenye cheo hakikisha unamfojea LIVE kwenye TV ili watu waone.
 
Wakati huo kijani waliwachonganisha walala hoi, wenye vipato bus chini,wale wa kipato cha wastani na matajiri.
 
Alikiuwa anawaambia wao ni wanyonge na kwamba wamechezewa sana? Halafu anamalizia na kumtumbua afisa mmoja wa karibu aliyepo hapo wananchi weweeeeeeee.[emoji2223][emoji2223][emoji2223][emoji2223][emoji2223]
[emoji23] [emoji23] [emoji23] umemaliza
 
Ni tajiri gani aliyewahi hata kuwekwa mahabusu kwasababu za kumyanyasa masikini ??

Mimi nawajua masikini wengi waliofungwa, kutekwa, kuuawa, kufungwa kwenye viroba, na kutishiwa bastola.
Hapa unaniambia, unanisuta, unanigombeza au unanielekeza? Leo unaonekana kuwa na Kisirani ( Kisununu ) fulani hivi. Kulikoni?
 
Hata mimi pia najiuliza alitumia mbinu gani kuwafanya watu wenye kipato cha chini(wanyonge kama yeye alivyokuwa anawaita) wawachukie matajiri?

Nilikuwa nashangaa unakuta mtu kaajiriwa na Mo dewji na 90% ya maisha yake yanategemea mshahara, hapohapo anamchukia tajiri huyo bila sababu.
 
Back
Top Bottom