Hayati Magufuli alifanikiwaje kuwafanya watu wa vipato vya chini kumuamini kiasi kile?

Hayati Magufuli alifanikiwaje kuwafanya watu wa vipato vya chini kumuamini kiasi kile?

Mtu mnyonge ni yule anaepata Milo mitatu kwa siku kwa shida, inabidi achakarike na asisumbuliwe, mf. Mmachinga anafukuzwa na Askari sehemu yake anayofanya biashara. JPM aliwapa kibali Cha unafuu, wataacha kumpenda?
 
hata mimi pia najiuliza alitumia mbinu gani kuwafanya watu wenye kipato cha chini(wanyonge kama yeye alivyokuwa anawaita) wawachukie matajiri?.

nilikuwa nashangaa unakuta mtu kaajiriwa na Mo dewji na 90% ya maisha yake yanategemea mshahara, hapohapo anamchukia tajiri huyo bila sababu.
Masikini ni kiumbe mwenye tabia mbaya sana, chuki, wivu vyote vyake
 
Ni kweli watu wanaemchukia jpm wanaembeza na kumkashfu kwenye mitandao wako katika kundi hili Vyeti feki, watumishi hewa, wauza madawa ya kulevya, watakatishaji fedha, wanasiasa wafitini waliopoteza majimbo kutokana na kasi za maendeleo ya JPM, wakwepa kodi, wonyonyaji, majambazi, wala rushwa na mafisadi na wanajifanya wao ndio wananchi walioonewa na serikali ya JPM.
 
Kupitia state Propoganda.

Abbasi, Jiwe, Musiba na vyombo vyote vya habari.
 
Baada ya Rais Mstaafu Kikwete kutoka Madarakani Matajiri walikuwa na Jeuri za kila aina mpaka Kuamua Uhai wa Watu Masikini na wasifanywe lolote lile kwani walimweka Mifukoni mwao.

Alipoingia Hayati Rais Dkt. Magufuli alitaka Kuwaheshimisha Masikini ( GENTAMYCINE nikiwemo ) kuwa hata Sisi pia ndani ya hii Ardhi ya Mama Tanzania pia tuna Thamani yetu hivyo akatupa ( akatujaza ) Jeuri mpaka Matajiri nao wakaanza Kutunyari ( Kutuogopa )

Kwa hivi sasa ndani ya huu Utawala wa Rais Mama Samia Matajiri na Masikini bado tunamsikilizia ( tunampima ) Mama tuone Yeye atalia upande wowote ili tuanze Kumlaumu ( Kumsiliba ) japo ninavyomuona ni kama vile anataka kutuweka katika Mzani sawa kitu ambacho si kibaya pia na Mimi nakiunga mkono.
Bora umekuja na Id yako tunayoikubali. Ukweli ni kuwa Magufuli hakuwahi kuwa msaada kwa hao masikini, na hakuna tajiri yoyote aliyekuwa akimuogopa masikini. Ila yeye alidhulumu matajiri wengi, kitu ambacho masikini walifurahi kwani ni kawaida kwa masikini kufurahia mtu anaposhuka kama wao.Alichokifanya ni kuminya uhuru wa habari na uhuru kujieleza, na akawabrainwash hao masikini kwa propaganda kuwa anawajali.

Kikubwa alichokifanya ni kuruhusu biashara holela ya wamachinga, na lengo hasa ni kujificha nyuma yao kwenye hiyo mindgame ya kuwa ni kiongozi wa wanyonge, huku akiendesha dhuluma, hujuma, ukatili na unyama kwa wote wenye mitazamo mbadala na yeye, pamoja na wafanyabishara ama matajiri. Kwa maneno mafupi alikuwa ni dhalimu aliyejivika ngozi ya kondoo, na kushurutisha aaminike kuwa ni mtetezi wa wanyonge.
 
Jibu rahisi.Alijinasibu wazi kuwa yeye ni Rais wa wanyonge.

"Kazi hii ni ngumu"
"Tumechezewa sana nchi hii"
"Msiwasumbue mama ntilie na machinga, kitambulisho cha 20,000 kinatosha. Wafanye biashara kokote"
"We're in a right track"
"Niombeeni kwa Mungu"
"iiiiiiiiiii.....Ahaaaa"

Hizo ni baadhi ya kauli zake zilizomzolea mtaji wa watu wa hali ya chini.
 
Wakati huo huo katika miaka 25 aliyokuwa ndani ya Serikali alikuwa mwizi na fisadi mkubwa kutokea awamu ya tatu hadi ya tano. Miaka 60 ya maccm madarakani bado kuna wanyonge chungu nzima, nani alaumiwe!?
Jibu rahisi.Alijinasibu wazi kuwa yeye ni Rais wa wanyonge.

"Kazi hii ni ngumu"
"Tumechezewa sana nchi hii"
"Msiwasumbue mama ntilie na machinga, kitambulisho cha 20,000 kinatosha. Wafanye biashara kokote"
"We're in a right track"
"Niombeeni kwa Mungu"
"iiiiiiiiiii.....Ahaaaa"

Hizo ni baadhi ya kauli zake zilizomzolea mtaji wa watu wa hali ya chini.
 
Maskini wengi waliopo Afrika hasa Kusini mwa Jangwa la Sahara wana kanuni za maisha zinazofanana ili waweze kuishi kwa kujifariji. Kwanza wengi hupenda maisha ya kupewa vitu vya bure hata kama vina ubora duni.

Hupenda sana kufanya shughuli zilizokuwa shaghalabaghala na zisizokuwa na mpangilio ili tu waweze kufanya shughuli zao za kutafuta maisha. Mbali ya hili hawapendi kabisa kulipa kodi hukuwakidhani kuwa jukumu hilo ni la watu matajiri.

Maskini hujiona kuwa ni watu wa kuonewa huruma tu, na wanaamini umaskini wao hutokana na kiibiwa na watu matajiri, jambo linalopelekea kukosa shukurani hata pale waposaidiwa.

Mwisho lakini si kwa umuhimu ni wavivu kwa kufikiria hata kwa matendo yao pia, wanakosa ubunifu ama kiu ya maendeleo jambo linalopelekea kuwa ombaomba.

Kwa wengi wao ambao mwendazake aliwaita wanyonge, ambaye naye aliishi kwa fikra hizo hizo na kuwapa faraja waishi kwa kanuni za maisha hayo
Siwezi kuwalaumu kwa kuwa wapo katika nira za "vicious cycle of poverty " za CCM zinazozidi kusaweka ndani ya madhila ya ujinga, maradhi na umaskini zaidi.
 
magufuli alitumia akili ndogo sana kuwawin wanyonge, mikwara yake kwa watumishi wa umma kulipelekea wanaoitwa wanyonge wapate huduma za kijamii bila usumbufu kitu ambacho kilikua kero kubwa huko nyuma
 
Njia ni rahisi tu.

Masikini wengi wana roho mbaya, wivu na akili ndogo hivyo:

Kwasababu huwa wana wivu na chuki kwa kila aliyenacho, wewe hakikisha unatukana kila siku mwenye nacho na kuwadhalilisha hadharani huku ukiwasifia wao masikini.

Tukana sana wazungu. Na hakikisha wakikupa pesa zao, hao masikini wasijue.

Dhibiti habari zote za mabaya yako, hakikisha unasifuwa na kutangazwa muda wote kwenye vyombo vya habari kwa mema tu.

Jifanye mcha mungu, na kila ukienda kwenye ibada hakikisha watu wanajua na picha zinatoka ukiwa mnyenyekevu.

Ukimsaidia ombaomba hata Jero hakikisha unachukua picha na video na zinaruka kila wakati kwenye TV ili kukuonesha ulivyo mwema .

Kila ukiongea na tajiri au mwenye cheo hakikisha unamfojea LIVE kwenye TV ili watu waone.

Exactly, that was what the dude was doing. Jamaa alikuwa ni mtu muovu wa dhahiri.
 
Mnyonge ni nani ??

Na ni kitu gani hicho alichofanikiwa kukipata bila usumbufu??

Wanyonge labda hawa wamachinga aliowaruhusu kufanya biashara holela huku mijini. Lakini hajawahi kusaidia wanyonge katika mantiki halisi ya kusaidia wanyonge.
 
Njia ni rahisi tu.

Masikini wengi wana roho mbaya, wivu na akili ndogo hivyo:

Kwasababu huwa wana wivu na chuki kwa kila aliyenacho, wewe hakikisha unatukana kila siku mwenye nacho na kuwadhalilisha hadharani huku ukiwasifia wao masikini.

Tukana sana wazungu. Na hakikisha wakikupa pesa zao, hao masikini wasijue.

Dhibiti habari zote za mabaya yako, hakikisha unasifuwa na kutangazwa muda wote kwenye vyombo vya habari kwa mema tu.

Jifanye mcha mungu, na kila ukienda kwenye ibada hakikisha watu wanajua na picha zinatoka ukiwa mnyenyekevu.

Ukimsaidia ombaomba hata Jero hakikisha unachukua picha na video na zinaruka kila wakati kwenye TV ili kukuonesha ulivyo mwema .

Kila ukiongea na tajiri au mwenye cheo hakikisha unamfojea LIVE kwenye TV ili watu waone.
Hata wewe upo kwenye Hilo kundi la wenye chuki, roho mbaya na wivu kwa wenye nacho
 
Jana maeneo ya matumbi matraffic wakiwa wametanda kila kona, Dereva wa daladala alipowaona tu
Akasema " Baba yetu amefariki sasa wameanza kutusumbua".

Kauli kama hizi zimekuwa zikisikia kwa watu wa vipato vya chini kuona kama hayati alikiwa ndio kila kitu. Na sasa hivi kila rekebisho linalotokea na litakalotokea inaonekana ninkwa sababu mtetezi wao hayupo.


Hizo mbinu alizotumia kuteka mashabiki wengi kuliko wafuasi wa chama chake ni zipi, na kwa nini wabunge, madiwani na serikali za mitaa walishindwa kututeka hivyo miaka yote?
Angalau Deo Filikunjombe na yeye alifanikiwa kwa kiasi flani.

Nawasilisha
Hakujikweza mbele ya watu wa chini. Aliwasikiliza na kuwasaidia mbele ya macho yao.

Hakutafuta kuwa karibu na jamii za kimataifa. Alitafuta ukaribu na watu wa chini huku akiongea lugha inayowapa matumaini.
 
Brainwashing tactics. kwa mfano propaganda 24/7 TBC1

Kuminya uhuru wa vyombo vya habari, visiandike ukweli

Kuziba watu midomo wasichallange madudu yake waziwazi na hivyo jamii kuendelea kuwa gizani

Kutunga sheria kandamizi juu ya takwimu hivyo kuzuia data za kuwafumbua macho watu kutolewa au kupatikana kiurahisi

Kutumia populist approaches za kujifanya anawatetea, anawasemea, kujifanya ni mwema na mkarimu kama vile kugawa hela njiani
Kundesha uchumi kwa sera ambazo hazina mulekeo 'regime uncertainty and herding behavior' you can not plan business growth with policy uncertainty (herding behavior-ni maamuzi ya kikundi fulani kufanya maamuzi ya watu wengi kwakujitoa ufahammu) Herd behavior is the behavior of individuals in a group acting collectively (in ways that seem intelligent) without centralized direction.
 
Back
Top Bottom