Wanao jua nini maana ya maisha, ni watu wa Chini, tabu zao, mvua na jua ni Lao, kuna wakati watu wa Chini wakiugua, Kwa sababu ya umasikini walionao, Huamua kutembea na magonjwa Yao huku wakipiga kazi na magonjwa hujikuta yakipona bila hata panaldo,
Ukiwajengea uwezo wa wao kupata Chao bila bughudha, bila kunyanyaswa, na Kwa kuwa hao ndio wengi, watakuamini na kukupenda, lkn hata hivyo, tajiri anafahamu ziliko baraka zake, ni Kwa wahitaji, mandiko pia yanasema, atakayemkaribisha Masikini, amkaribisha Mungu nyumbani mwake
Na kiongozi yeyote anayewakumbuka Masikini anaheshimika Sana, sasa nyinyi matajiri, Kwanza huwa mnadhani heshima yenu inatokana na Mali zenu hata kama wewe ukiwa mkorofi na mdhurumaji
Huwa tunawaangaliaga tu, tunasema iihiiiiii...!