Benjamini Netanyahu
JF-Expert Member
- Aug 7, 2014
- 102,675
- 126,930
Amelaaniwa amtegemeaye mwanadamu na kumfanya kuwa kinga yake.
Hivi ni vitu vidogo tu, nilidhani umepigwa risasi kumbe umetishiwa, tena na wanaolinda usalama wako, tena waliokuwa wanalinda mali za kitaifa zenye migogoro na mabeberu.Mimi mwenyewe nilishawahi kutishiwa bastola wakati nafanya kazi za ulinzi. Tena nilitishiwa na watu wa usalama waliokuwa wanalinda makinikia.
Na vipi yule dereva wa roli aliyetishiwa bastola na mume wa Zamaradi, au yeye siyo mnyonge!!
Jifunze kwanza kuandika.Hivi ni vitu vidogo tu, nilidhani umepigwa risasi kumbe umetishiwa, tena na wanaolinda usalama wako, tena waliokuwa wanalinda mali za kitaifa zenye migogoro na mabeberu.
Mkuu mbona US, SA wanapigana hovyo lisasi sisi mwaka sijui wa ngapi huu kesi ni moja tu ya Lissu tena haijajulikana kapigwa na nani hadi leo maana kwa ninavyomjua angejua angesemamkwa ushahidi wakisheria.
Ni kwa kuwa Tanzania inaongoza kwa nchi zenye wananchi wapumbavu na elimu duniJana maeneo ya matumbi matraffic wakiwa wametanda kila kona, Dereva wa daladala alipowaona tu akasema " Baba yetu amefariki sasa wameanza kutusumbua".
Kauli kama hizi zimekuwa zikisikia kwa watu wa vipato vya chini kuona kama hayati alikiwa ndio kila kitu. Na sasa hivi kila rekebisho linalotokea na litakalotokea inaonekana ni kwa sababu mtetezi wao hayupo.
Hizo mbinu alizotumia kuteka mashabiki wengi kuliko wafuasi wa chama chake ni zipi na kwa nini wabunge, madiwani na serikali za mitaa walishindwa kututeka hivyo miaka yote?
Angalau Deo Filikunjombe na yeye alifanikiwa kwa kiasi flani.
Nawasilisha
Akili ninazo Bro.Jifunze kwanza kuandika.
Kwahiyo, Kutishiwa ni jambo dogo, unataka watu wauawe kabisa kama Akwilini Akwilini au wapewe ulemavu kama Tundu Lissu ili urudi hapa kusema hata Marekani na SA wanaua!!
Una akili timamu kweli???
Huna akili
Huku ndio kubrainwash watu.Ni kwa kuwa Tanzania inaongoza kwa nchi zenye wananchi wapumbavu na elimu duni
Ukiwa masikini hohehae unayumbishwa yumbishwa kama takataka. Unaishi kwa matumaini yasiyokuwepo.Ni kwa kuwa Tanzania inaongoza kwa nchi zenye wananchi wapumbavu na elimu duni
Kama mpaka leo kuna watu wanaishi maisha duni huko vijijini ila bado unakuta kaweka bendela ya ccm nyumbani kwake, sasa katika mazingira kama hayo sidhani kwamba kwa Magufuli kufungia vyombo vya habari na kuzuia mikutano ya siasa ndio imefanya apendwe na hao masikini.Kwa kufungia vyombo vya habari na mikutano ya kisiasa,afu akawa yeye tu ndo anazunguka tz nzima kila siku
[emoji1787][emoji1787]Alikiuwa anawaambia wao ni wanyonge na kwamba wamechezewa sana? Halafu anamalizia na kumtumbua afisa mmoja wa karibu aliyepo hapo wananchi weweeeeeeee.[emoji2223][emoji2223][emoji2223][emoji2223][emoji2223]
Mbona aliwaambia serikali haijaleta tetemeko na hela za michango akazichukuwa na ipo mifano kama hii.Ila lijamaa lilkuwa linajua kutengeneza sura ya unyenyekevu na huzuni utazan hvyo vtu linavyo kumbe hapana,
Kama siku Mv nyerere ilivyozama huko ukara lilkuwa linaongea kinyenyekevu mpaka nkaona linaigiza
Kila kitu kina sababu hivyo inawezekana kuna sababu zilizopelekea hao raia kuwa hivyo.Sababu kubwa ya hao unaowaita wa kipato cha chini kumpenda na kumshabikia mfu Magufuli ni kwamba ni wanafiki sana, walikuwa wanafurahi sana mtu kufukuzwa kazi eti na yeye asote kama wao. Pia walikuwa wanafurahi sana mtu aliyeajiriwa au mwenye kipato kizuri kufukuzwa kazi au kufilisiwa kwa hoja kuwa eti alikuwa anaringa!
Malizia sentensi vizuri, yaani wengi wasio jitambuaMagufuli alikuwa kipenzi cha wengi.
Ni tajili yupi aliyenyanganywa ela yake?ungeliweka na ushaidi kuliko kubwabwaja tu.Sema Magufuri alilazimisha hao mnaoita matajiri kulipa kodi kitu ambacho ktk utawala wa Mkwere kilikuwa nadra sana,tajiri alijiamlia kulipa kodi anavyotaka.Bora umekuja na Id yako tunayoikubali. Ukweli ni kuwa Magufuli hakuwahi kuwa msaada kwa hao masikini, na hakuna tajiri yoyote aliyekuwa akimuogopa masikini. Ila yeye alidhulumu matajiri wengi, kitu ambacho masikini walifurahi kwani ni kawaida kwa masikini kufurahia mtu anaposhuka kama wao.Alichokifanya ni kuminya uhuru wa habari na uhuru kujieleza, na akawabrainwash hao masikini kwa propaganda kuwa anawajali.
Kikubwa alichokifanya ni kuruhusu biashara holela ya wamachinga, na lengo hasa ni kujificha nyuma yao kwenye hiyo mindgame ya kuwa ni kiongozi wa wanyonge, huku akiendesha dhuluma, hujuma, ukatili na unyama kwa wote wenye mitazamo mbadala na yeye, pamoja na wafanyabishara ama matajiri. Kwa maneno mafupi alikuwa ni dhalimu aliyejivika ngozi ya kondoo, na kushurutisha aaminike kuwa ni mtetezi wa wanyonge.
Siungi mkono masikini kuchukia tajiri ila ukiangalia hawa matajiri zetu vipato wanavyowalipa masikini huko kwenye viwanda vyao ukilinganisha na mazingira ya kazi zenyewe pengine hizo chuki alizotengeneza zilikuwa na za pa kuanzia.Wanyonge ni wajinga sana , na mwendazake aliwaaminisha kwamba watu wote wenye pesa ama uwezo flani ni maadui yaani wao wanasababisha maskini kuwepo kwasababu ya utajiri wao which is wrong, alitengeneza chuki nyingi sana baina ya matajiri na wasionacho , Kimsingi jamaa alikua crap sana
Wanyonge maana yake wamesharidhika na maisha yao ni watu duni wanaochukuliwa kutokuwa na thamani hivyo hata ukiangalia baadhi ya comments za watu humu jinsi wanavyowaelezea utakubaliana na mimi, kwahiyo inawezekana ikitokea ukatambua uwepo wao na kuwaheshimisha kwao huwa ni jambo kubwa sana maana si kwamba walikuwa wakitaraji kutajirishwa.Madikteta wote drama zao ufanana.
Hapa iddi amini akimpeleka mnyonge hospitalini Ili kudraw attention zao kupata sapoti ya kisiasa kupata kura zao.
View attachment 1766470
Wanyonge walibrainwashed kwamba matatizo yao yameletwa na matajiri.Kumbe unyonge wao umeletwa na Utawala dhalimu.Wanyonge maana yake wamesharidhika na maisha yao ni watu wanaochukuliwa kutokuwa na thamani hivyo inawezekana ikatokea kuwatambua uwepo wao na kuwaheshimisha kwao huwa ni jambo kubwa maana si kwamba walikuwa wakitaraji kutajirishwa.
Kwa kuanzia nenda kwa wenye Bureau de change kisha ulete mrejesho hapa. Huo ni mfano halisi namba moja, ukitaka tuendelee sema. Ama unadhani kwakuwa kipindi cha dhalimu vyombo vya habari vilifungwa midomo ndio ukweli hatuujui?Ni tajili yupi aliyenyanganywa ela yake?ungeliweka na ushaidi kuliko kubwabwaja tu.Sema Magufuri alilazimisha hao mnaoita matajiri kulipa kodi kitu ambacho ktk utawala wa Mkwere kilikuwa nadra sana,tajiri alijiamlia kulipa kodi anavyotaka.
Duniani kote na toka dunia iumbwe masikini ndio wengi kuliko wengine, sasa ukisema unauchukia umasikini unanifikirisha sana.Imagine masikini ni mtu mbaya sana asee, nauchukia umasikini
Mifano basi japo michache ya roho nzuri kwa matajiri maana kila mtu naona anaishia kusema watu wa vipato vya chini wana roho mbaya.Watu wa vipato vya chini wengi wana roho mbaya sana. Furaha yao ni kuona wengine wanapata tabu. Ndio maana walienda sawa na mzee, maana nae mikato yake ndio hiyo hiyo.