- Thread starter
- #41
Chadema hamna pa kushikilia!
Tumepashika penyewe. Tunajua mchawi siyo CCM bali kuna agenda mpya tokea awamu 5 inaitwa urais ni taasisi.
Haijulikani hii taasisi mpya ni kwa mujibu wa kifungu kipi cha katiba. Haijulikani ilikampeni wapi kuwa yenyewe. Haijulikani wajumbe wake ni nani.
Hii bila shaka ni taasisi ya watu wasiojulikana.
Hii ina majibu yetu ya nani nyuma ya kesi ya mwamba. Nani nyuma ya kupotea Lijenje, Ben, Azory na hata nani walikuwa kwenye viroba. Nani nyuma ya shambulizi la Lissu. Hii inajua nani wapo nyuma ya SABAYA.
Hawa ndiyo wenye kesi na hukumu zao pale law school.
Hao ndiyo wenye uhusika ukuu na wahanga wa Corona.
Hawa ndiyo wanaotuharibia nchi.
Hao ndiyo wanaotugombanisha.
"Hawa ni ama zao ama zetu!"