Hayati Magufuli alijenga vituo vya afya 44 kwa miaka mitatu, Rais Samia anajenga 220 kwa miezi mitatu

Hizi tozo zingekuja wakati wa Magufuli dunia ingepasuka!!
 
Hivi vituo 220 vipya budget ya dawa manurse ambulance ikoje? Ni kweli watanzania ni wagonjwa kiasi hiki?
Mkuu wewe unishi sehemu zenye kila huduma, tembea uone, Kuna watu wanakata 15 km kufuata huduma za afya.
 
Magufuli alikopa trilioni 30 ndani ya miaka mi tano
mama Samia amekopa trilioni 20 ndani ya miezi mitatu
 
soma ripoti ya deni la taifa ipo kwenye tovuti ya wizara ya fedha na tovuti ya bot pia mwenye ripoti za cag


Lete hiyo ripoti, unaongopa,

Kuna Mikopo ilikopwa kabla ya Samia ila imekuwa dew wakati huu,

Pengine unasemea hayo,
 
Not mesoma tu kichwa Cha habari. Kusema rais amejenga mradi fulani ni ujinga wa kiwango cha juu sana. Miradi inajengwa kutokana na kodi tunazolipa sisi wananchi. Rais ni mtumishi kama watumishi wengine, na anatekeleza majukumu ya ofisi yake kwa mujibu was sheria, na miradi inayotekelezwa sio hisani ya rais bali ni stahiki za raia kutokana na kodi wanazolipa.
 
Sio vibaya kujenga vituo lkn wahudumu wa afya ni wauaji na hawana roho ya imani kabisa. Yaani mgonjwa anakufa kwa sababu ya uzembe wa kijinga tuu. Ukitaka kuwashauri hawasikii, sijui hata huko chuoni wanafundishwa nini, kuua au kuokoa maisha ya watu. Mungu anawaona kwa kweli na kuna siku mtatoa hesabu za matendo yenu
 
Wako wachache na maslahi finyu wanachoka ,wewe ukiumwa wapitishie rupia kidogo fasta utakuta wako na wewe mda wote
 
Vyovyote iwavyo sifa huwa zinaenda kwa kiongozi mkuu wa Serikali.Na diwani atasema nimejenga kituo hiki cha afya,halikadhalika mbunge.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…