Hayati Magufuli alikosea kwenye mambo mengi mno. Kubwa mojawapo ni kumchagua huyu mtu


Tulia we trafiki

Maujinga yenu tunayafahamu na Samia alisimulia mlivyo wapumbavu sio kama ana chuki nanyie
 
Muwe wakweli wa nafsi zenu, halamishi kupendwa wakati kila siku anatumia wasanii na waandishi wa habari wasio na akili kumsifu! Halazimishi kupendwa wakati kila siku yuko busy kuponda mtangulizi wake ili yeye aonekane mwema na anawatumia mpaka mawaziri wake kufanya hivyo, halazimishi kupendwa wakati mikutano yake wanafunzi wanasombwa kwa maroli wafanyakazi hawaendi kazini ili aonekane ana umati, barabara zote zimejaa mabango ya anaupiga mwingi mithiri ya mawe ya Mwigulu kipindi cha kampeni za urais 2015 utadhani kampeni zimeanza. Analazimisha kupendwa sema hapendeki.

Kwamba ameongeza mishahara sawa lakini huo mshahara unaoongezwa wakati kila kitu kimepanda bei una impact gani kwa maisha ya mtumishi ambaye aliongezewa elfu ishirini? Unamuongezea mshahara ila wote unaukata kata kwa tozo akitaka kumtumia ndugu yake kiasi kidogo cha kujikimu, unamuongezea mshahara ila unapandisha bei ya cement mtumishi atajenga? Unamuongezea mshahara unashindwa kudhibiti bei ya mafuta mtumishi hiyo nyongeza ataiona?

Inawezekana hizo hoteri unazozisema zinafurika kweli lakini je zinaajili watanzania au muwekezaji anaamua anachokitaka habanwi na sheria? Je kama zinaajili watanzania zinafuata sheria ya ajira na mahusiano kazini au wafanyakazi wananyanyasika na kwa kuwa wana shida wanaamua kuvumilia? Siku zote mamlaka zikisimamia sheria zilizopo inaweza kupunguza huo uwekezaji sababu mamlaka zinasimamia maslahi ya watu wake lakini ikiwa ya njooni muwekeze na siwabani mkitaka na watafanyakazi wapigeni virungu lazima waje kwa kasi maana ni banana republic. Lakini pia hotel zinajengwa kwa kuwafurusha watu wako kwa nguvu mfano Loliondo?

Kamba miradi inaendelea huenda ni kweli lakini je inakamilika kwa wakati au ni sababu zisizo za msingi kila kukicha mf bwawa la Mwl Nyerere? Je thamani ya fedha inaonekana au ndo CAG anakuja na madudu na hakuna hatua zinachukuliwa? Mazuri huenda yapo lakini ya kutafuta kwa tochi sawa na punje ya sukari baharini haiwezi kubadili ladha ya maji.
 
Hapo kwenye mishahara na marupurupu umeongeza chumvi. Aliongeza pesa ndogo sana huwezi kununua hata kilo 2 za nyama na hakuna marupurupu yoyote yaliyoongezwa. Kwanza wanaopata marupurupu ni viongozi wachache sana kwenye utumishi wa Umma. Siyo wafanyakazi wote.
 
Mkuu umesema kweli kabisa. Nakumbuka hayati Magufuli alipigania ajira kwa wazawa kwa kuamini tunaweza. Alienda mbali na kuweka utaratibu wa kila kampuni isizidi raia wakigeni 5. Sasa huyu kafungulia goli, wageni wanapewa vibali kwa mgongo wa expert visa. Wanafanya kazi tunazoweza kufanya. Kibaya zaidi wanatengeneza cartels na kucheza na mifumo ya Tehama ili walipe kodi kidogo. Magu nilimpongeza sana kwa hili……
 
Kumbuka kauli ya Makonda wakati wa kuahirisha bunge la katiba. Alipiga utani kuwa Samia afikiriwe kuwa makamu wa Rais uchaguzi unaofuata.

Lakini, kama ilivyo ada kwa wanasiasa kuandaa warithi wao - ngazi ya urais, Kikwete pia alifanya hivyo. Ila baada ya upepo kuvuma kinyume, alikuja na mbinu mbadala ya kumweka japo makamu wa Rais ili kama Rais hatakuwa mtiifu kwake basi ajue ya sirini kwa Rais.

Alifanikiwa aiseee! Ndo kisa cha huyu mama kuwa alipo sasa. Ni mkakati mkali.
 
Ni hivi,Magufuli hakuwahi kuwa na nia ya kuwasaidia watz kwa ujumla.Mfano ni KIWANDA CHA SARUJI CHA DANGOTE.Kikwete aliwaangalia raia na kuwatafutia njia za kuwafanyia wepesi katika kupiga hatua kimaendeleo.Ujio wa Dangote ulilenga kuwasaidia raia katika kuleta makazi bora kwa kila raia,alikiruhusu kiwanda kizalishe Saruji ya viwango vyote ili kuwawezesha raia wa vipato vya kawaida pia kumudu gharama ya kununua Saruji kwa ujenzi wa makazi.
Kiwanda cha Dangote kilifanya Saruji huku mikoani kuuzwa kwa Tsh12000 kwa mfuko.
Magufuli alipoingia madarakani alimzuia Dangote kuzalisha Saruji ya viwango vyote na kumtaka abaki akizalisha Saruji ya viwango vya kimataifa tu ambayo mfuko mmoja ni kati ya Tsh 25000 hadi 35000.
Leo hii hakuna tena Saruji ya Dangote madukani huku mikoani,bei ya Saruji kwa sasa ni kati ya Tsh 18000 hadi 22000.

Sasa kwa mfano huu unaweza kusema Magufuli alikuwa akiwajali raia na maisha yao?.
Huo uzalendo mnaouimba toka kwake ni upi hasa?.
Kwa hiki alichokifanya kwa Saruji ya Dangote,alikifanya kwa manufaa ya nani?.
Tunawezaje muamini mtu wa aina yake katika maamuzi aliyofanya tukiangalia mfano wa kiwanda cha Dangote?.
 
Hii hapa mkuu wala usiteseke sana.

Your browser is not able to display this video.
 
Hahahaaa!Wamiliki wa asili.
 
Many a times you came across as this obnoxious self opinionated person to me through your comments/threads (my personal opinion probably biased while at it, no offence intended) lakini uzi huu umedhihirisha uelewa wako mkubwa mno katika ku observe vitu.

Samia kama anapitia mitandao kama anavyosema, ajaribu kujitafakari afanye lililo sahihi n kuachia madaraka kabla hajaharibu zaidi.
 
Kwenye mkutano mkuu wa ccm 2020 Magufuli alisema wazi kabisa kwamba yeye chaguo lake namba moja la mgombea mwenza alikuwa Hussein Mwinyi ila wazee wakamchagua Samia yeye hakumpenda kabisa ila chama kiliamua

Sisi wengine alipoingia tu madarakani tulilisema hili mapema tu kuwa vyama vyote viwe
Your browser is not able to display this video.
makini kwenye kuchagua wagombea wenza.
 
Mwanaadamu hapaswi kukiweka kifo kama kipaumbele kwa kuwa hakina ratiba.Ila kama nchi tulitakiwa kuzingatia kwamba kuna kesho, hivyo tuweke wasaidizi bora kwa ajili za dhatrura kama zile.
 
Safi sana mkuu.
 
Kasome Ilani ya CCM alafu uone kama suala la kuleta wawekezaji halipo.
Sasa yeye kama anatekeleza Ilani ya chama chake,unataka chama kimuone hafai vipi?.
 
Mimi ni Tomaso, I just don't believe this!.
Baada ya kisa hicho, wazee wastaafu (ALI H MWINYI) wakaingiliya kati. Na ndipo mahusiano yakazidi kuwa tete.
Duh!.
Viongozi wenu waliokuwepo zanzibar waliiba Dola millioni 75 za mtoto wa mfalme wa Qatar.
Too good to be true!. Dola milioni 75 cash!. Sorry, I don't believe this!.
Magu alikuja akakaa siku tatu anaongea na watu wake namna gani fedha zimepotea.

Walikula Dr. Shein na watoto wake, Sefu Ali Iddi(mkongo), na makada kadha waCCM.
Utapata dhambi bure kumsingizia Dr.Shein mwizi wa mtindo wa ujambazi!.
Baada ya hapo, Haji kheri amejenga hoteli kumi na moja za kitalii.
Duh...!.
Wote hawa ni wapenzi wa Magu hatujui katika wizi huu na mahoteli haya , share ya Magu ni kiasi gani.
Duh...!
Duh...!, hizi fix nyingine...!.
Kama ni wizi , makada wote wa CCM ni wezi.
Sii kweli!, tupo wengi tuu, makada safi wa CCM ambao ni Nyerere type!. Tunafuata falsafa ya Nyerere... Kumbe watu wa Nyerere bado wapo na wana misimamo kama Nyerere. Hongera MFA, Dr. Mahiga kwa msimamo, tusikubali kuyumbishwa
Mama hakukubaliana na mambo mengine ya Magu ndio maana akawa mbaya. Wizi wa maduka ya dhahabu, forex kufungiwaetc etc zote wakati wa Magu.
duh...!.
Mimi nawashangaa sana wanao msifia Magu kuwa kaleta maendeleo.
Usiwashangae, it's true!. JPM ameleta maendeleo makubwa sana!. JNHPP, SGR, Fly Overs, Kuhamia Dodoma, the list goes on... Oktoba 28 ni mashindano kati ya Reality vs Ahadi Hewa? Je, Watanzania watachagua nini kati ya visible, tangible Deliverables vs The Empty Promises?
P
 
Jpm alikuwa kiongozi mbovu, ila huyu mamako ndo buure kabisa!
Boss inabid uanze na system ya uongozi wa nchi kwanza then ndio uje kwa hao viongozi wako

Kuna huyu jamaa wa Roma bwana Marcus Tullius Cicero aliwai sema "The best form of government embraces a balance of powers"... Simply hata watawala wakuu watakuwa watawala jeuli kama utawala wao hauta dhibitiwa ...

Ni kwamba hata democracy itashuka na nchi itatawaliwa na kikundi cha watu wachache hivyo kupelekea kutozingatiwa kwa kanuni za kikatiba ambazo zinadai hitaji la manufaa kwa nchi na wananchi kwa ujumla pamoja na usalama wao

Mifumo kwanza then hayo mambo mengine ni rahisi kubadilishika
 
Sikieni,suala la Bandari ni katika Ilani ya CCM.Hakuna kitakacho badilika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…