Hayati Magufuli alikosea kwenye mambo mengi mno. Kubwa mojawapo ni kumchagua huyu mtu

Hayati Magufuli alikosea kwenye mambo mengi mno. Kubwa mojawapo ni kumchagua huyu mtu

Mkuu

Ongeza vitu viwili alivyonavyo wa hapo TZ
1. Hasira isiyo na mithili ila ameificha kwenye ngozi (Reference JK voice)
2. Visasi vya bayana (Reference-kukamatwa na trafiki akiendesha gari na kudharau kusimamishwa na askari trafiki halafu alipookota uhangaya alitamka wazi wazi jinsi anavyochukizwa na cops!!! Kurejesha viongozi wote walioharibu kwenye dhamana na wanaendelea kuharibu bila kuchukuliwa hatua zozote
3. Nepotism
4. Kuthamini mali ya kupewa naye kugawa ya nyumbani bila ridhaa ya wenye umiliki wa asili

Tulia we trafiki

Maujinga yenu tunayafahamu na Samia alisimulia mlivyo wapumbavu sio kama ana chuki nanyie
 
Mkuu kuna mengi yanayoendelea muda huu sema wewe huwezi kuyaona wala kuyathamini na ni haki yako kuwa hivyo.

Mwendo kasi unamaliziwa kujengwa. Utalii unaifungua nchi. Mahoteli kama uyoga yanaajiri wafanyakazi kila kukicha.

Ni mengi tu yanayoendelea, JPM hakuongeza mshahara hata mara moja katika miaka yote sita, SSH keshaongeza hiyo mishahara na marupurupu mengi wanalipwa wafanyakazi.

Samia hana umaarufu kwa sababu hatafuti sifa kwa nguvu, halazimishi kupendwa na watu.
Muwe wakweli wa nafsi zenu, halamishi kupendwa wakati kila siku anatumia wasanii na waandishi wa habari wasio na akili kumsifu! Halazimishi kupendwa wakati kila siku yuko busy kuponda mtangulizi wake ili yeye aonekane mwema na anawatumia mpaka mawaziri wake kufanya hivyo, halazimishi kupendwa wakati mikutano yake wanafunzi wanasombwa kwa maroli wafanyakazi hawaendi kazini ili aonekane ana umati, barabara zote zimejaa mabango ya anaupiga mwingi mithiri ya mawe ya Mwigulu kipindi cha kampeni za urais 2015 utadhani kampeni zimeanza. Analazimisha kupendwa sema hapendeki.

Kwamba ameongeza mishahara sawa lakini huo mshahara unaoongezwa wakati kila kitu kimepanda bei una impact gani kwa maisha ya mtumishi ambaye aliongezewa elfu ishirini? Unamuongezea mshahara ila wote unaukata kata kwa tozo akitaka kumtumia ndugu yake kiasi kidogo cha kujikimu, unamuongezea mshahara ila unapandisha bei ya cement mtumishi atajenga? Unamuongezea mshahara unashindwa kudhibiti bei ya mafuta mtumishi hiyo nyongeza ataiona?

Inawezekana hizo hoteri unazozisema zinafurika kweli lakini je zinaajili watanzania au muwekezaji anaamua anachokitaka habanwi na sheria? Je kama zinaajili watanzania zinafuata sheria ya ajira na mahusiano kazini au wafanyakazi wananyanyasika na kwa kuwa wana shida wanaamua kuvumilia? Siku zote mamlaka zikisimamia sheria zilizopo inaweza kupunguza huo uwekezaji sababu mamlaka zinasimamia maslahi ya watu wake lakini ikiwa ya njooni muwekeze na siwabani mkitaka na watafanyakazi wapigeni virungu lazima waje kwa kasi maana ni banana republic. Lakini pia hotel zinajengwa kwa kuwafurusha watu wako kwa nguvu mfano Loliondo?

Kamba miradi inaendelea huenda ni kweli lakini je inakamilika kwa wakati au ni sababu zisizo za msingi kila kukicha mf bwawa la Mwl Nyerere? Je thamani ya fedha inaonekana au ndo CAG anakuja na madudu na hakuna hatua zinachukuliwa? Mazuri huenda yapo lakini ya kutafuta kwa tochi sawa na punje ya sukari baharini haiwezi kubadili ladha ya maji.
 
Mkuu kuna mengi yanayoendelea muda huu sema wewe huwezi kuyaona wala kuyathamini na ni haki yako kuwa hivyo.

Mwendo kasi unamaliziwa kujengwa. Utalii unaifungua nchi. Mahoteli kama uyoga yanaajiri wafanyakazi kila kukicha.

Ni mengi tu yanayoendelea, JPM hakuongeza mshahara hata mara moja katika miaka yote sita, SSH keshaongeza hiyo mishahara na marupurupu mengi wanalipwa wafanyakazi.

Samia hana umaarufu kwa sababu hatafuti sifa kwa nguvu, halazimishi kupendwa na watu.
Hapo kwenye mishahara na marupurupu umeongeza chumvi. Aliongeza pesa ndogo sana huwezi kununua hata kilo 2 za nyama na hakuna marupurupu yoyote yaliyoongezwa. Kwanza wanaopata marupurupu ni viongozi wachache sana kwenye utumishi wa Umma. Siyo wafanyakazi wote.
 
Mkuu umesema kweli kabisa. Nakumbuka hayati Magufuli alipigania ajira kwa wazawa kwa kuamini tunaweza. Alienda mbali na kuweka utaratibu wa kila kampuni isizidi raia wakigeni 5. Sasa huyu kafungulia goli, wageni wanapewa vibali kwa mgongo wa expert visa. Wanafanya kazi tunazoweza kufanya. Kibaya zaidi wanatengeneza cartels na kucheza na mifumo ya Tehama ili walipe kodi kidogo. Magu nilimpongeza sana kwa hili……
 
Mtu huyo ni Rais Samia!

Nashawishika kabisa kuamini kuwa huyu Samia alichaguliwa kutokana na jinsia yake tu [kama ilivyojuwa kwa Kamala Harris…the word salad queen…kule Marekani].

Kamala yeye alichaguliwa na Biden kuwa mgombea mwenza kwa sababu ni mwanamke mweusi [ingawa kiuhalisia ni chotara wa Kihindi na Kijamaica].

Kamala ni mweupe kabisa. Yaani hovyo to the nth degree. Anaongeaga mashudu tu [word salads].

Hana kabisa uwezo wa kuongoza. Yeye ni kucheka cheka tu na kuongea mambo yasiyoeleweka.

Ukimwangalia Biden, unaona kabisa jamaa anapaswa awe nyumbani. Kazi ya urais wa Marekani kwa sasa haiwezi.

He is a creepy old guy. Hebu angalia hapa



Hivi alikuwa anafanya nini hapo kwa hako katoto? Na hiyo ni wiki iliyopita alipokuwa Finland baada ya kutoka Lithuania kwenye mkutano wa NATO.

Biden muda wowote anaondoka. Iwe kwa kujiuzulu, kuamua kutogombea tena muhula wa pili, au hata kufa [ingawa kifo hakina mwenyewe].

Wazo la Kamala kuja kuwa Rais wa Marekani endapo Biden ataondoka, linatisha watu wengi sana.

Haya, tuje kwa huyu wa kwetu hapa.

Huyu naye alichaguliwa kwa sababu ya identity politics tu. Ni mwanamke na ni Mzanzibari.

Kwa ninayoyaona, ni mtu asiye na uwezo wa kiuongozi ngazi ya Rais wa nchi.

Hakuchaguliwa kutokana na sifa zake za kiuongozi.

Inavyoonekana Magufuli alikuwa anataka sifa ya kuwa na mgombea wa kwanza wa CCM kumchagua mwanamke kuwa mgombea mwenza wake.

Haiwezekani kabisa kuwa Samia alichaguliwa kutokana na sifa zake kiutendaji [kwa sababu hana].

Jahazi limeshamshinda hivi sasa. Kabaki kutoa vitisho na kutumia dola kukabiliana na wanaompinga.

Na ukiongeza na inferiority complex aliyonayo kutokana na jinsia yake, ndo kabisa anakuwa paranoid kwamba kila anayempinga, anafanya hivyo kwa kusukumwa na chuki dhidi yake kwa sababu yeye ni mwanamke!

Rais Magufuli hakuwa kiongozi mzuri. Nilishasema mara nyingi tu kuwa yeye alikuwa msimamizi/ mnyapara mzuri.

Yeye mpe kazi au mradi ausimamie, halafu umpe mamlaka ya kutosha kuweza kufanya maamuzi ndani ya ukomo fulani, utampenda maana hakuwa wa mchezo mchezo.

Sidhani kabisa kuwa Magufuli aliwaza kuhusu yeye kuishia njiani na kumwacha Samia ndo awe Rais.

Nadhani alidhani kuwa atamaliza vipindi vyote viwili na kustaafu kama walivyofanya waliomtangulia.

Lakini haikuwa hivyo. Tumeachiwa huyu Samia.

Makamu wa Rais, Dkt. Mpango, kwa mtazamo wangu, ni bora mara 100 kuliko Samia [I got bars too [emoji3]].
Kumbuka kauli ya Makonda wakati wa kuahirisha bunge la katiba. Alipiga utani kuwa Samia afikiriwe kuwa makamu wa Rais uchaguzi unaofuata.

Lakini, kama ilivyo ada kwa wanasiasa kuandaa warithi wao - ngazi ya urais, Kikwete pia alifanya hivyo. Ila baada ya upepo kuvuma kinyume, alikuja na mbinu mbadala ya kumweka japo makamu wa Rais ili kama Rais hatakuwa mtiifu kwake basi ajue ya sirini kwa Rais.

Alifanikiwa aiseee! Ndo kisa cha huyu mama kuwa alipo sasa. Ni mkakati mkali.
 
Tujilaumu wenyewe Kwa kumpinga na kumtukana Magu aliyedhamiria kuibadili Nchi Kwa muda mfupi,

Hivi sasa, watu wameficha petrol na diesel na hawafanyi kitu,

Magu aliwatisha kufuta lesseni walipogomea EFD na waliufyata.

Aje Dikteta mwingine tafadhali[emoji120][emoji120]
Ni hivi,Magufuli hakuwahi kuwa na nia ya kuwasaidia watz kwa ujumla.Mfano ni KIWANDA CHA SARUJI CHA DANGOTE.Kikwete aliwaangalia raia na kuwatafutia njia za kuwafanyia wepesi katika kupiga hatua kimaendeleo.Ujio wa Dangote ulilenga kuwasaidia raia katika kuleta makazi bora kwa kila raia,alikiruhusu kiwanda kizalishe Saruji ya viwango vyote ili kuwawezesha raia wa vipato vya kawaida pia kumudu gharama ya kununua Saruji kwa ujenzi wa makazi.
Kiwanda cha Dangote kilifanya Saruji huku mikoani kuuzwa kwa Tsh12000 kwa mfuko.
Magufuli alipoingia madarakani alimzuia Dangote kuzalisha Saruji ya viwango vyote na kumtaka abaki akizalisha Saruji ya viwango vya kimataifa tu ambayo mfuko mmoja ni kati ya Tsh 25000 hadi 35000.
Leo hii hakuna tena Saruji ya Dangote madukani huku mikoani,bei ya Saruji kwa sasa ni kati ya Tsh 18000 hadi 22000.

Sasa kwa mfano huu unaweza kusema Magufuli alikuwa akiwajali raia na maisha yao?.
Huo uzalendo mnaouimba toka kwake ni upi hasa?.
Kwa hiki alichokifanya kwa Saruji ya Dangote,alikifanya kwa manufaa ya nani?.
Tunawezaje muamini mtu wa aina yake katika maamuzi aliyofanya tukiangalia mfano wa kiwanda cha Dangote?.
 
Mwenye uwezo wa kuweka ile video ya JPM akisema yeye chaguo lake kuwa Dr Mwinyi lakini ikabadilishwa na akawa SSH, tafadhali aiweke hapa ili tuisikilize tena.

Kwa maoni yangu mimi ni kwamba JPM alikuwa kama akilalamika (maana alisema ni siri ila lazima aiseme) kuwa hakupewa nafasi kumchagua mtu aliemtaka yeye ili awe Makamu.

Maana alisema wazi kuwa alimfahamu Dr Mwinyi kwa miaka 10 na hata kusifia kuwa aliongoza wizara ya Ulizni kwa miaka hiyo 10.

Wengi humu ni wajuvi hivyo mwafahamu kuwa ukigundua umekosea mahala ni lazima utafute namna ya kuja kurekebisha kosa lako.
Hii hapa mkuu wala usiteseke sana.

 
Mkuu

Ongeza vitu viwili alivyonavyo wa hapo TZ
1. Hasira isiyo na mithili ila ameificha kwenye ngozi (Reference JK voice)
2. Visasi vya bayana (Reference-kukamatwa na trafiki akiendesha gari na kudharau kusimamishwa na askari trafiki halafu alipookota uhangaya alitamka wazi wazi jinsi anavyochukizwa na cops!!! Kurejesha viongozi wote walioharibu kwenye dhamana na wanaendelea kuharibu bila kuchukuliwa hatua zozote
3. Nepotism
4. Kuthamini mali ya kupewa naye kugawa ya nyumbani bila ridhaa ya wenye umiliki wa asili
Hahahaaa!Wamiliki wa asili.
JamiiForums1972983755.jpg
 
Many a times you came across as this obnoxious self opinionated person to me through your comments/threads (my personal opinion probably biased while at it, no offence intended) lakini uzi huu umedhihirisha uelewa wako mkubwa mno katika ku observe vitu.

Samia kama anapitia mitandao kama anavyosema, ajaribu kujitafakari afanye lililo sahihi n kuachia madaraka kabla hajaharibu zaidi.
 
Kwenye mkutano mkuu wa ccm 2020 Magufuli alisema wazi kabisa kwamba yeye chaguo lake namba moja la mgombea mwenza alikuwa Hussein Mwinyi ila wazee wakamchagua Samia yeye hakumpenda kabisa ila chama kiliamua

Sisi wengine alipoingia tu madarakani tulilisema hili mapema tu kuwa vyama vyote viwe
makini kwenye kuchagua wagombea wenza.
 
Kila kitu kimepangwa kuhusu Kamala, wakubwa wa Dunia wanataka kudestroy western Christian civilization na ndiyo maana wamemuweka Biden ambaye atamuachia Kamala ambaye anakwenda kuizika USA na Western christian world kimoja tuombee sana Ukristo (western) usishindwe, kuhusu kwetu Magufuli hakujua wala hakuwahi kudhani nafikiri kama Uraisi wake ungekatishwa nadhani aliamini kabisa kama Maraisi wengine kwamba angeongoza Miaka 5 na mitano mingine na kumwachia mwingine lkn sidhani kama alifikiria hata kidogo kama mambo yangebadilika/shwa wengi TZ maraisi hawakukifikira sana cheo cha Umakamu wa raisi kwa kifupi ni president in waiting.

Women Destroy Nations …
Mwanaadamu hapaswi kukiweka kifo kama kipaumbele kwa kuwa hakina ratiba.Ila kama nchi tulitakiwa kuzingatia kwamba kuna kesho, hivyo tuweke wasaidizi bora kwa ajili za dhatrura kama zile.
 
Mkuu, NN, kwanza asante kwa hoja hii maana tayari imenipa bandiko!.

Pili naomba kuheshimu mawazo yako lakini sio lazima kukubaliana na wewe,
Uwezo wa urais is relative na unafuata principles of relativity kama ganda la mua la jana, kwa wengine ni uchafu la kutupa na wengine ni kivuno!.

Ikifanyika beauty pageant, kushirikisha 100 beautiful girls, wale the last ten, wakishindanishwa kuna the most beautiful wao.

2015 niliendesha shindano hili humu jf Siku ya Wanawake Duniani: Je, tuna Wanawake wenye sifa za Presidential Material? kwa kuwashindanisha wanawake high profile women wa Tanzania kwa sifa za urais, Samia Suluhu Hassan ndio akaibuka the top and the best, hivyo she might be not the best kwa vigezo vyako, but she is the best of what we have!.

Ana sifa zote hadi za ziada!, naomba nitajie Mwanamke mwingine yeyote mwenye nusu ya sifa hizi Siku ya Wanawake Duniani: VP Samia Suluhu: "Womanly, Genuine, Humble, Simple na Down To Earth!”

VP ni president in waiting, hana mamlaka yoyote ya kiutendaji, Samia Suluhu Hassan ni among the highest top profile women in Tanzania, nilimspot tangu 2010 New Cabinet: Baadhi ya Majina ni Haya Hapa!

She is human, sio super woman, hivyo anahitaji kusaidiwa, na wasaidizi huru tupo tumejitolea kumsaidia. Msaada mkubwa tutakaompa Rais Samia ni anapokosea, tumkosoe kwa lugha ya staha na kumshauri the right thing to do. Ni kweli hana ngozi ngumu ya kuhimili critics, hivyo tunamsaidia kama hivi Mzee Mwinyi, Mkapa, Kikwete na Hayati Magufuli, walisifiwa, walikosolewa! Haki ya kusifu/kupongeza iende sambamba na haki ya kukosoa!

Hata sisi waandishi alipotuasa tumkune vizuri, na alipotutisha wale tutakao mpara atatuparua, Rais Samia: Ukinikuna Vizuri, mimi nakukuna huku nnakupapasa na kukupuliza. Lakini "Ukinipara...Nakuparura!
kwanza tuliuliza humu Kauli ya Rais kwa waandishi 'Wapara' kuwa wakimpara "Atawaparua", Je Rais Samia ni katili?, Soma Jinsi ya kuwabaini makatili!. Ni kutumia macho tu!. kisha tukamshari https://www.jamiiforums.com/threads...rais-samia-tunakuomba-mama-usiwaparure-wapara

Mimi ni miongoni mwa tuliomshauri JPM, ampishe Samia 2020 Siku ya Wanawake Duniani: VP Samia Suluhu: "Womanly, Genuine, Humble, Simple na Down To Earth!” nilishauri


Kisha 2020 nikarudia "Watu waachwe Huru kuujadili Muungano"- VP, Samia Suluhu Hassan. Huyu mama anaongea vizuri kwa Unyenyekevu mpaka raha. Huchoki kumsikiliza

Katika kifupi Samia amefanya mengi, makubwa mazuri, haya ni miongoni mwake
  1. Asante Mungu kwa Rais Samia: Ni Msema Kweli na Mtenda Kweli, Ni Msema Haki na Mtenda Haki. Je, Ataruhusu Ubatili Huu Kuendelea Ndani ya Katiba Yetu?
  2. Samia Mpango wa Mungu kwa Tanzania: Kwa Hili, Atabarikiwa!, Taifa Litabarikiwa!. Asante Mungu kwa Samia, Mungu Mbariki Samia, Mungu Ibariki Tanzania
  3. Psychoanalysis Trends za Viongozi Wetu, Humbleness ya Rais Samia ni Bonafide Genuine, ni asili yake, ni nature yake, ndivyo alivyo, Ila...
  4. Haki Huinua Taifa! Rais Samia kwa Kauli na Matendo ameonesha ni mtu wa Haki. Akitekeleza hili kama alivyosema, atabarikiwa, Tanzania itabarikiwa
  5. Rais Samia ana nia njema Watanzania wapate haki, ila Watanzania hawajui Haki! Je, Tumsaidie kuelimisha umma Katiba, Sheria na Haki au?
  6. Asante sana Rais Samia kwa kuliponya Taifa. Umeonesha kwa kauli na matendo; tunajenga nyumba moja, hakuna sababu ya kugombea fito!
  7. Kwa “nonsense” ya Sukari, Rais Samia anastahili pongezi. Je, tuishie kwenye "nonsense" ya Sukari tu au tuangazie na "nonsense" nyingine zote?
  8. Asante Rais Samia kwa kuwasisitiza watendaji wa vyombo vya haki kuwa haki sio hisani, bali ni stahiki. Watende haki, tubadili Katiba kurudisha haki
  9. Kuelekea Usawa wa Kijinsia: Kumbe 50/50 Inawezekana!, Wanawake Hao wa 50/50 Wapo!. Hongera Sana Rais Samia Kwa Kuonyesha Njia! Je 2025 Tuwaonyeshe?
  10. Je, kuna kazi za kike na za kiume? Fupa hili lililowashinda wanaume wanne, mwanamke mmoja ataliweza?
Kufuatia kuzuka tabia ya uchawa, mtu ukimsifu na kumpongeza rais Samia, unaweza kuonekana ni chawa!. Mimi sio chawa wa Mama Samia wala sio chawa wa mtu yoyote!. Tofauti ya pongezi za kichawa na pongezi bonafide genuine, pongezi za kichawa ni kusifu tuu!. Pongezi bonafide genuine ni kupongeza panapostahili pongezi, na akikosea tunamkosoa
  1. Rais Samia, sio malaika ni binadamu anaweza kukosea. Tusimlaumu, kumshutumu na kumponda kwa makosa ya kukoseshwa. Tumvumilie tumpe muda
  2. Pongezi Zangu ni Bonafide-Genuine! Sisaki Teuzi, Sitaki Teuzi, Niko Naye Mbeya, Nitamweza!
  3. Watanzania, tuunge mkono 2025 ni zamu ya Mwanamke, ila sio lazima awe yeye bali yule aliyepangiwa na 'YEYE', kama ni yeye aliyepangiwa, then ni yeye!
  4. Voices From Within: Japo 2025 Tumepanga Twende na Mwanamke, 2025 Mama Akabidhi Kwanza Mwanamume, Kisha 2030 Ndipo Aje Mwanamke
  5. Japo Bunge Limeridhia, DPW Kuendesha Bandari Zetu, ni Makubaliano Tu, Tukithibisha Kuna Matatizo, Tunarekebisha Mkataba wa HGA, Kazi Nzuri Iendelee!
Namalizia kwa ushauri huu kwa wote Heshima kitu cha bure! Kwanini Rais Samia, japo sio lazima apendwe na wote lakini ni lazima aheshimiwe na wote? Akosolewe kwa staha na asitukanwe!

Paskali.
Safi sana mkuu.
 
As this Bandari saga goes on, I have of recent met with various people from various Countries East Africa, West Africa, America and Jamaica etc ...they were all agape when I showed them and they read our Inter-governmental Agreement IGA with the Dubai Emirates. Fast forward, they all asked me If the President read the Agreement, but I had no Answer because none of the Information available indicates that she has read it, again they asked "was she elected?" And I had to explain the circumstances she became President, suprisingly, they all had the same view as Nyanni Ngabu did.


Pamoja na kuwa nasimama Nyuma ya Raisi wangu Samia Suluhu, kwa hili la Bandari nimeshindwa kumtetea kwa watu wa nje. i have failesd miserably, sio kwa sababu siwezi kumtetea, No, ila kwa sababu Mkataba wenyewe unajitetea upande mmoja, kama alivyosema Profesa Shivji. Tanzania tuna wajibu mkubwa kuliko Dubai Ports. Unakuwa kichwa maji kuutetea.

Sasa kwasababu sijui siasa siwezi kusema nani atachagulika katika chaguzi zijazo, ila naweza kusema Raisi Samia Suluhu hapaswi kutafuta ngwe nyingine, because Chama chake kitaanguka vibaya.
Kasome Ilani ya CCM alafu uone kama suala la kuleta wawekezaji halipo.
Sasa yeye kama anatekeleza Ilani ya chama chake,unataka chama kimuone hafai vipi?.
 
. Magu aliwatukana wapemba hadi mama akakasirika. Akamjibu Magu. Magu akarusha kofi, yule body guard wa mama akaushika mkono wa Magu kabla kufika usoni. Magu alishituka sana. Usalama wa taifa wakamchukuwa Magu kando na kumpumzisha. Yule binti bado yupo na mama na ndio mlinzi wake namba moja.
Mimi ni Tomaso, I just don't believe this!.
Baada ya kisa hicho, wazee wastaafu (ALI H MWINYI) wakaingiliya kati. Na ndipo mahusiano yakazidi kuwa tete.
Duh!.
Viongozi wenu waliokuwepo zanzibar waliiba Dola millioni 75 za mtoto wa mfalme wa Qatar.
Too good to be true!. Dola milioni 75 cash!. Sorry, I don't believe this!.
Magu alikuja akakaa siku tatu anaongea na watu wake namna gani fedha zimepotea.

Walikula Dr. Shein na watoto wake, Sefu Ali Iddi(mkongo), na makada kadha waCCM.
Utapata dhambi bure kumsingizia Dr.Shein mwizi wa mtindo wa ujambazi!.
Baada ya hapo, Haji kheri amejenga hoteli kumi na moja za kitalii.
Duh...!.
Wote hawa ni wapenzi wa Magu hatujui katika wizi huu na mahoteli haya , share ya Magu ni kiasi gani.
Duh...!
Paul Makonda alikuwa akitumiwa kufanya kazi ya bwana mkubwa mpaka siku alipogusa sehemu isioguswa, uhusiano ukapunguwa. Kweli ukiwa hutaki kufuata amri ya Bwana Magu utakuwa mbaya. Makonda alikuja zanzibar baada ya wafanya biashara wawili kutuhumiwa kuiba madini. Basi katika makubaliano, alitumwa Makonda kuja zanzibar kuchukuwa dola zaidi ya elfu ishirini. Hiyo ndio hukumu ya MAGU.
Duh...!, hizi fix nyingine...!.
Kama ni wizi , makada wote wa CCM ni wezi.
Sii kweli!, tupo wengi tuu, makada safi wa CCM ambao ni Nyerere type!. Tunafuata falsafa ya Nyerere... Kumbe watu wa Nyerere bado wapo na wana misimamo kama Nyerere. Hongera MFA, Dr. Mahiga kwa msimamo, tusikubali kuyumbishwa
Mama hakukubaliana na mambo mengine ya Magu ndio maana akawa mbaya. Wizi wa maduka ya dhahabu, forex kufungiwaetc etc zote wakati wa Magu.
duh...!.
Mimi nawashangaa sana wanao msifia Magu kuwa kaleta maendeleo.
Usiwashangae, it's true!. JPM ameleta maendeleo makubwa sana!. JNHPP, SGR, Fly Overs, Kuhamia Dodoma, the list goes on... Oktoba 28 ni mashindano kati ya Reality vs Ahadi Hewa? Je, Watanzania watachagua nini kati ya visible, tangible Deliverables vs The Empty Promises?
P
 
Jpm alikuwa kiongozi mbovu, ila huyu mamako ndo buure kabisa!
Boss inabid uanze na system ya uongozi wa nchi kwanza then ndio uje kwa hao viongozi wako

Kuna huyu jamaa wa Roma bwana Marcus Tullius Cicero aliwai sema "The best form of government embraces a balance of powers"... Simply hata watawala wakuu watakuwa watawala jeuli kama utawala wao hauta dhibitiwa ...

Ni kwamba hata democracy itashuka na nchi itatawaliwa na kikundi cha watu wachache hivyo kupelekea kutozingatiwa kwa kanuni za kikatiba ambazo zinadai hitaji la manufaa kwa nchi na wananchi kwa ujumla pamoja na usalama wao

Mifumo kwanza then hayo mambo mengine ni rahisi kubadilishika
 
This is the crux of the matter. The whole truth, and I am glad you got around everything else you have written and found this truth at last!
But, again, you don't seem to get away from the conflict you have in your thought process. Why?

Kama bado unayo matumaini ya yeye kujifunza na kugeuza hali ilipofikia, nadhani utakuwa ni mtu wa miujiza wewe!

She is done.
Tanzania will pickup the pieces and mend itself before it moves forward.
This was a waste of precious time.
Sikieni,suala la Bandari ni katika Ilani ya CCM.Hakuna kitakacho badilika.
 
Back
Top Bottom