Asante sana King Kigoda kwa ushauri wako, nina matumaini nitapata darasa na ufunuo kwenye ilani ya Chama cha Mapinduzi , hatahivyo
KK, naomba tukubaliane kwamba sijasema kuwa Raisi Samia Suluhu, hafai, na kwa mlolongo huo huo niwaombe radhi wengine walio kwazika, kwani, halikuwa lengo langu kufanya hivyo.
KK, nimesema nipo nyuma ya Raisi Samia Suluhu na hilo halibadiliki kwa sasa.
Vilevile, sijasema kuwa suala la uwekezaji halifai, isitoshe hata hao wageni niliokutana nao hawakusema Uwekezaji haufai, amini usiamini mmoja wao wa Zambia alinidokeza mengi tu kuhusu yaliyowatokea Wazambia na Wachina, sinto enda huko, ila alitahadharisha kuhusu Mkataba wetu kwani wa kwao uliwahujumu, hivyo nasi tuwe makini yasije kututokea. Nakuomba usinilishe maneno.
Mkuu, ukinisoma vizuri nimesema Raisi Samia Suluhu hapaswi kutafuta ngwe nyingine, because Chama chake kitaanguka vibaya. Nikiwa na maanisha anaweza subiri ngwe nyingine kwa sababu sakati hili linafoka rushwa na hivyo kuiweka CCM katika hali ngumu kichaguzi.