Dah!
Sasa nijieleze vipi kwako ndipo upate kunielewa vizuri wewe mtu, hivi akili zenu huwa zinawekwa sumu ya namna gani hiyo inayoondoa kujiona mtu mwenye uwezo wa kuona jambo na kulielewa lilivyo, bila ya kuegemea upande ulioteka akili hiyo?
Samia hajawa na uungwana wowote, kama anadiriki kuingiza taifa kwenye janga kama hili analotafuta kutuingiza
Ungekuwa ni mtu mwenye akili huru, wala usingethubutu hata mara moja kuutumia huo mfano wa TICTS. Hakuna mfanano wa aina yoyote kati ya "Makubaliano/Mkataba" alioingia nao TICTS na huu mnaolazimisha nyinyi, na kwa bahati mbaya kabisa mnaingiza na udini humo humo.
Hivi taifa kuwa la kiarab, ni lazima litangulizwe na Uislam (dini) kabla ya uarab wao?
Mwarab hawezi kufanya mambo kinyume na dini ya kiislam?
Huyu Mungu unayemlilia hapa, siyo mali ya mtu yeyote, wala wa dini maalum.
Mungu aliyeiweka hii nchi hapa ilipo, anaipenda sana, bila kujali hizo dini mbalimbali zilizopo hapa. Hilo kwangu linatosha, na ninaamini ni Mungu huyo ndiye atakayetuondolea ujambazi huu mliotaka kuuleta hapa.
Mwanzoni nilidhani ni upinzani tu wa uwekezaji bandarini kwa kigezo cha mkataba.
Lakini Hamza Johari na Dr Possi waliuelezea kifungu kwa kifungu na nilimsikiliza na nikamuoja live kwenye TV wasiwasi wote ukanitoka.
Kila nikisikia hoja mpya zinazozaliwa naona kinachopingwa ni asili ya mwekezaji mwenyewe na sio mkataba, Mwabukusi na hao wachungaji wote wamefikia hatua ya kujiita watanganyika kisa ni mkataba.
Hii haihitaji akili ya mwanasayansi mvumbua roketi kuweza kuzisoma hizi akili ambazo kwanza kwa muda mrefu zilikuwa zinamchukia Rais Samia na muda huu ndio zimeupata wa kuonyesha zinavyomchukia na pili zinautumia uwekezaji wake kama nafasi ya kuweka chuki hadharani!.
Tuwe makini sana Tanzania ni moja tu, na awe ni mtu mwenye ushujaa ulioshiba upumbavu atakayependa kwa dhati kabisa kutoka moyoni mwake kuiona nchi hii inavunjika vipande vipande.
Kule Kenya kuna wasomi na wastaarabu kuliko Tanzania, tuwe makini sana mwelekeo wetu wa kitaifa usifikie hatua ya kufanana na wao.
Tulitakiwa tujikite katika kuifikiria geographical advantage tuliyonayo kwa sasa na sio sisi kuwa kama wapumbavu na kuanza kubaguana kwa kuitana yule mtanganyika na yule mbara, pathetic mindset.
Mkataba wa DPW hauna matatizo yoyote kwani umeshafafanuliwa kwa kina. Faida za uwekezaji ni nyingi kwa wafanya biashara sio kwa hawa wachungaji wanaoshinda makanisani na kondoo zao pamoja na masheikh wanaoshinda misikitini na waumini.
Faida ni kuwezesha usimamizi mzima wa TPA, kuondoa foleni na urasimu unaotengeneza kila aina ya rushwa.
Faida nyinfgine ni usomeshaji wa wataalam wetu wa masuala ya bandari, na hapo sijaongelea ongezeko la makusanyo ya TRA.
Mwendeshaji bandari akiwa na uzoefu wa kazi hata vifaa kama cranes vinapoharibika anaweza kuwasiliana na makampuni ya watengenezaji kwa haraka zaidi kuliko namna TPA wenyewe wanavyoweza kusogezewa miezi ya mbali zile order zao.
Pia ni faida kwa nchi kwani DPW ana mali huku Congo na Rwanda ambazo zinahitaji pia kutumia SGR yetu. End to end logistic chain ndio maana ya bandari kisasa.
Hakutakuwa na masuala ya upitishaji wa madawa ya kulevya unaowezeshwa na mifumo kutokuwa ya kisasa zaidi.
Ni suala jema, na litapiganiwa mpaka litimie bila ya kusikiliza hizi kelele za mawakala wa wapigaji na mafisadi.