Hayati Magufuli alikosea kwenye mambo mengi mno. Kubwa mojawapo ni kumchagua huyu mtu

Huu uzi ni mzito sana inatakiwa uwekwe kila mahali nchi nzima na kufundishwa mashuleni na vyuoni. Samia hamna kitu pale. Ni huu ujinga wa ccm kubebana kwa kujuana, mitala nk ila huyu hata uwaziri hatoshi achilia mbali makamu wa Rais na sasa hivi Rais. Mgufuli hakumchagua maana mpaka anateuliwa kugombea Urais alikuwa hana nguvu au ndani ya chama. Bahati nzuri juzi wakati Kikwete anahojiwa akiwa Arusha kuhusu uongozi wa Samia aliongea mengi na mojawapo ni kuwa yeye ndie alimfuata Magufuli na jina la Samia ili amteue kuwa mgombea wake mwenza naye Magu akakubali
 
Magufuli hakuwai kumchagua, juzi tu hapa kiwete amesema ni yy ndo alimshawishi John kumchagua huyo kitu bora na kiumbe dhaifu. Hivyo John ni kama alishurutishwa.
 
Kusema mkataba urekebishwe ni siasa nyepesi sana, hauna tatizo huo mkataba, na uusome kwa ujumla wake sio kushika kifungu kimoja na kuacha na kuhamia mahali pengine.

Usome wote kwa ujumla ili uweze kuuelewa. Usidhani kwamba waliouandika huu mkataba ni wajinga, ni wasomi wabobezi wa sheria. Na wameshautetea mkataba huu hadharani.

Huu ujanja ujanja wa kutaka kuikwamisha serikali kwa vitu vya kitaalam ni upotezaji tu wa muda. Serikali inajiandaa kuingia hatua inayofuata ya kusaini mikataba ya kibiashara.

Kuzeni uelewa wenu kwanza.
 
Kwanza siamini kua hii ni account rasmi ya kwako....sikuwai kuona unatuma andiko la hivi kabisa.Yaani umeshindwa ata kutueleza Mh.Rais ilibidi afanye nini na akaahindwa.Hao wasiopenda kufuata sheria unataka wabembelezwe kama watoto?
 
Kwa hili la kumchagua huyu Mama,Magufuli atanisamehe sana huko aliko aisee..ametuachia jitu la hovyo hakuna mfano.
 
Mtu huyo ni Rais Samia!

Nashawishika kabisa kuamini kuwa huyu Samia alichaguliwa kutokana na jinsia yake tu [kama ilivyojuwa kwa Kamala Harris…the word salad queen…kule Marekani].
La jinsia ni kweli, CCM walitaka kura za wanawake. Lilianza na Spika mwanamke Makinda.
Rais Samia alieleza mwenyewe kwenye mkutano mmoja jinsi alivyochaguliwa.
Samia alisema katika kikao cha kamati kuu baadhi walikaa nje vingunge wakaingia ndani.

Walipotoka Rais Kikwete akamweleza kwamba amechagulia. Samia anasema alilia kwanza akifokewa na Kikwete kwamba 'nenda ndani unalia lia nini'' haya yapo kwenye video Samia akieleza kwa uvccm.
Ukweli kwamba makamu lazima atoke Zanzibar, hilo likampa fursa moja kwa moja.
Wamarekani wana mambo ya ajabu kidogo, maana sioni kama Kamala ni tishio kuliko Trump
Kamala hana uwezo kama wa Senator Amy Klobuchar lakini mjinga anayesikiliza akiaambiwa ni bora kuliko mpumbavu asiyesikia au kuelewa na hapa Trump. Tuachie hapo
Huyu naye alichaguliwa kwa sababu ya identity politics tu. Ni mwanamke na ni Mzanzibari.
Hili la identity politics ni baya . Baadhi tulishahisi ipo siku tutakuwa na Rais kwa identity tu lakini si uwezo.
Inavyoonekana Magufuli alikuwa anataka sifa ya kuwa na mgombea wa kwanza wa CCM kumchagua mwanamke kuwa mgombea mwenza wake.JPM alikuwa mgombea na hakuwahi kuwa katika nafasi yoyote ya uongozi wa chama hapo awali.
JPM hakuwa na ushawishi wa aina yoyote ile kuwa VP, sijui kama alijua VP anatakiwa atoke Zanzibar achilia mbali mwanamke. Kwa hili namtetea sana JPM

Kwa utaratibu wa CCM M/kiti ana ushawishi mkubwa sana akiwa na kamati kuu 'aliyoitengeneza' na wajumbe wa NEC na wakati huo alikuwa JM Kikwete. Hivyo chaguo lilitoka kwa Kikwete na si JPM kwa kila sababu.
Na ukiongeza na inferiority complex aliyonayo kutokana na jinsia yake, ndo kabisa anakuwa paranoid kwamba kila anayempinga, anafanya hivyo kwa kusukumwa na chuki dhidi yake kwa sababu yeye ni mwanamke!
Hii ngao ya kwamba ni Mwanamke tuli ionya mapema kwamba yeye ni Rais aliyetokea kuwa mwanamke. Washauri, Machawa na wapiga debe walikomalia jinsia kwasababu tu lilionekana kama 'ni taboo' kumsema mwanamke.

Lakini pia Rais SSH akachukulia hiyo kama fursa ya kutekeleza mambo ya jinsia, akawa ni advocate wa gender na kusahau kuwa ni kiongozi wa nchi. Tuliona '' gender balance'' badala ya uwezo katika nafasi
Kwasasa suala la jinsi limepoteza nguvu na yanayoendelea ni kuangalia madhaifu ambayo yanajitokeza wazi.
Sidhani kabisa kuwa Magufuli aliwaza kuhusu yeye kuishia njiani na kumwacha Samia ndo awe Rais.
JPM hakuwaza kuwa Rais hata siku moja, ilipotokea ikamfanya ajisahau kuwa ni mwanadamu.

Hakuwa na maono kama ya Nyerere ya kuandaa timu ya viongozi wajao au ikitokea lisilotarajiwa.
Kosa la JPM, aliogopa wakosaji wake ana alikuwa tayari kufanya kazi na vilaza akijua yupo tu.

Lakini pia kuna tamaduni za kipuuzi sana hasa kwa CCM , kwamba kiongozi amalize muda wake, na ilikuwa ngumu kwa JPM kumchagua VP mwingine kabla ya 10 years aliyodhani angeimaliza.
Nadhani alidhani kuwa atamaliza vipindi vyote viwili na kustaafu kama walivyofanya waliomtangulia.
Kujisahau kuwa ni mwanadamu. Madaraka yalimlevia sana
Makamu wa Rais, Dkt. Mpango, kwa mtazamo wangu, ni bora mara 100 kuliko Samia [I got bars too 😀].
Mpango ni tatizo . Fuatlia viongozi wa zama hizo kama akina Mzee Warioba, Mzee Msuya, Sokoine, Mkapa , Salim Ahmed n.k. Hao walikuwa na uwezo wa kumkabili Mwl Nyerere licha ya kwamba mzee yule altisha sana.

Ukifuatilia habari za vikao , 'vijana' wa Mwalimu Nyerere walikuwa na uwezo wa kumwambia hapana au ndiyo.
Unakumbuka Mzee Warioba alipoacha kikao cha Urais wa bahari za dunia akakimbia Msasani kumwabia Nyerere akitekeleza suala fulani anajiuzulu u-AG!

Mpango si kiongozi wa kaliba ya 'vijana' wa Mwalimu. Ni mtu anayeona mambo hayaendi vizuri anakaa kimya.

Ni mtu asiyeweza kusimamia jambo pengine akivizia ''Zamu' yake.
Matatizo mengi anayokutana nayo SSH hasa muungano chini ya ofisi ya VP ni kutokana na udhaifu wa Mpango

Hawezi kumweleza boss wake ukweli akivizia tu wakati ufike ili naye awe Rais.
Mpango si kiongozi katika 'A' list. Lini umemsikia akizungumza jambo la nchi ukasema VP kaongea! Hafai
 
Ubunifu ndo kwenda kusaini mkataba wa hovyo bila hata kushirikisha mwanasheria mkuu na serikali ,na ndo maana wwnahaha kila kona kumuabisha na aibu huku wakijichanganya wenyewe
Mkataba hauna shida yoyote zaidi ya ujinga wenu na maslahi binafsi waliyonayo kundi flani la watu ambao wanajua lakini wanapotosha makusudi
 

Kama wanaomzunguka ndo wanasababisha hali hii mbaya, basi kuna shida mahali. Kiongozi anaongoza!!!
 
samia she's missfit to the position.
 
Hapa ni CCM 100% unataka nikupe namba yangu ya Kadi?

Unajifanya unanijua, hunijui.

Anayesema wewe mfia dini? Anayesema wewe mwongo aliyejipenyeza hapa jamiiforums.? Huna lolote.
Bandari kapewa Dp world,mtake au msitake ishakuwa hivyo na hakibadiliki kitu.
 
Ukiiangalia video utaelewa kabisa Mwinyi ndo alikuwa namba moja ila chama "wazee" wakamchukua Samia kwa kigezo cha jinsia na sio uwezo
Wapi chama kilimpangia? Then mnadhani huyo Mwinyi ndio angekua better than Samia? Ukimtoa Maalim na kidogo OMO huko Zanzibar ni rare sana kupata watu strong and serious wengi ni "waungwana"
 
weekend hii tulikuwa baa nikakimbia kikao baada ya kuona washkaji wameanza matani eti maza aliipata yenye iliki ya arabuni akapoteza network kaamua kugawa nchi bure! Amependekeza serengeti na mlima kilimanjaro kama mfalme akimpea tena!
 
Bandari kapewa Dp world,mtake au msitake ishakuwa hivyo na hakibadiliki kitu.
Unaota. Watanganyika hawata kubali kunyanyasika. Na hao unaowatetea,wote waarabu na vibaraka wao, ni wa kuswekwa lumande tu. Kaa chonjo
 
Sio kweli hapo anasema alikuwa ashamfahamisha Mwinyi kwamba ndo atakuwa VP na akasema lakini hata alivyomteua Samia Mwinyi wala hakulalamika alitulia, akaongeza kwamba alivyomteua samia alilia maana hakujua kama atateuliwa. Hiyo ni ishara tosha kwamba jpm alikwenda kwenye kikao na jina la Mwinyi akalazimika kuliacha huko akarudi na jina la Samia hapo ni kusema kwa lugha nyingine kwamba hakuwa chaguo lake"la kwanz"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…