Hayati Magufuli alikuja kuharibu maisha ya vijana, Mimi ni mmoja wa wahanga

Hayati Magufuli alikuja kuharibu maisha ya vijana, Mimi ni mmoja wa wahanga

Jiwe kuja na sera za serikali kufanya biashara badala ya kujikita kwenye kukusanya kodi alichemsha sana.Aliua sekta binafsi na kuja na swaga za kupata gawiwo fake toka mashirika ya umma. Jamaa alikuwa anajidanganya mwenyewe!Mashirika kama Air Tanzania ni "White Elephant "🤔
 
Alikuwa na roho mbaya,vijana wote waliomaliza vyuo 2015 aliwatumbukiza kwenye janga la kukosa ajira.

Hivi daktari au mwalimu anakosaje ajira wakati shule nyingi na hospitali hadi leo wafanyakazi hawatoshi ,shule ina wanafunzi 500+ waalimu wako 6 halafu ajira hamna.

Jamaa alikuwa mfalme Juha .
hospitali za umma zinaupungufu mkubwa wa watumishi, lakini vijana wahitimu wapo tu mitaani wanafanya vibarua
 
Jiwe kuja na sera za serikali kufanya biashara badala ya kujikita kwenye kukusanya kodi alichemsha sana.Aliua sekta binafsi na kuja na swaga za kupata gawiwo fake toka mashirika ya umma. Jamaa alikuwa anajidanganya mwenyewe!Mashirika kama Air Tanzania ni "White Elephant "🤔
True
 
Dah!mi nilikuwa nachukua used zanzibar nakujakuuza dar baada ya mwamba kuingia nilikutana na makodi utafkiri mzigo unatoka UK mwenyewe nilisanda mpaka leo sijaunga .
Acha nicheke,maendeleo hayana chama
 
Mimi nashauri vijana wote waliomaliza vyuo vya elimu juu, ufundi stadi, VETA wapewe pasipoti kubwa ya kusafiri nje bila masharti yoyote, wazewe kwenda ughaibuni.


Every United States citizen is entitled to a U.S. passport provided that they, or an adult acting on a child’s behalf, comply with all applicable requirements, and that there is no statutory or regulatory reason to deny the passport .. more : source : Fact Sheet on Passports for Judges and Lawyers


More links :
https://www.tcu.go.tz/?q=content/higher-education-statistics,


Utaenda ughaibuni kwa mluzi?
 
Mkapa hakuajiri?

Maswali yaliyomo kwenye andiko langu, kama utataka kuyajibu, tunaweza kujua ukweli wa mambo.

Ukijibu hivyo, maana yake unataka kusikia yale yakupendazayo bila kujali uhalisia na ukweli wake.

Nchi ina uwezo huo? Inahitaji waajiriwa kwa kiasi hicho? Waliopo, wanalingana na uzalishaji na huduma watoazo?

Wewe ukiwa na biashara, utafanya kwa mtindo huo? Mnapotaka wawekezaji, wao wanaajili kwa mtindo huo?

Wawekezaji, kazi za watu 4 mpaka 6 serikalini zinafanywa na mtu mmoja, hii inatengeneza ajira?

Acha siamba Mkuu, watu wote tumejionea ajira hazikuwa kipaumbele awamu iliyopita.

Kuhusu umaskini wa nchi hii hoja haina mashiko ukumbuke ilisemekana hii nchi ni "tajiri" alias "Dona Kantre" tatizo kubwa tuliwaza maendeleo ya vitu zaidi na kusahau maendeleo ya watu.

Binafsi I don't get it kwanini hizi project Nyerere dam na SGR ziliendeshwa pamoja kwanini tusingeanza na Nyerere dam ambapo ingechochea maendeleo ya viwanda huku ajira nazo zikiendelea then the next project ije kuwa SGR huku ajira na nyongeza za watumishi zikiendelea? Ku run maproject makubwa makubwa kama haya at once ni sawa na kukanyaga Brakes and Accelerator at once.
Ni hayo Mkuu
 
Babu yule alikua na roho ndogo sana, roho ya uharibifu na kimaskini, alitufanya kama Taifa zima ni wanae na anaweza kutuamulia atakavyo, daah acha
 
Maisha ndivyo yalivyo kuna kupanda na kushuka wewe muda huu unainjoi kuna mwenzako anapitia magumu.
 
Usimlaumu kwenye suala la Ualimu wewe uliziba nafasi ya ajira kwa wenye taaluma yao kwann hukuenda kujitolea kwenye fani yako JPM alikua anaweka mambo kwenye mstari hakutaka makanjanja
 
Nasikitika sana!

Mimi ni kijana mmoja wapo kati ya vijana wengi walioharibiwa maisha yao!

Siku zote ukweli hujitenga na uongo, sisemi uongo utawala wote wa awamu ya tano nimehangaika sana.

Nilihitimu chuo 2015 kada ya afya!

Kutokana na uhaba wa ajira nilikaa sana kitaa nikifanya mishe mishe mpaka nikaamua kwenda kuomba kufundisha shule ya private kwakuwa nilikua ninaufaulu mzuri wa masomo ya physics na hesabu, japo mshahara ulikuwa kiduchu lakini niliendelea kukomaa.

Nimefanya kazi pale baadae ukatoka waraka kuwa shule zote zifundishwe na walimu proffesionally sisi hatutakiwi! Mkurugenzi wa shule alinishauri nikasomee ualimu nikirudi atanipa nafasi tena, sikuamua kufanya hivyo kwakuwa tayari nilikua nina fani ya Afya na ugumu wa ajira ndio ulionileta hapo! Baasi nikapewa barua ya kuachishwa kazi, tulikua wawili wote tuliachishwa kazi kwa kigezo hicho kilichotoka Serikalini!

Nilikaaa bila ramani na baada ya muda nilijikita kwenye mambo ya habari nilifungua blog baada ya kuvutiwa na blog ya jamaa yangu aliyekua anavuta hela kupitia blog yake!

Kweli nilijitahidi sana mpaka nilianza kupata matangazo nakumbuka tangazo la kwanza kabisa nilipewa kutangaza ibada za hija na kanisa flani hivi, na tangazo la pili nilipewa kutangaza cables na dawa za mitishamba kupitia blog yangu!

Kiasi flani nilikua napata pata pesa japo zilikuwa kidogo.

Sikuchukua muda sana Serikali ya awamu ya tano ikazuia kuchapisha maudhui bila leseni na leseni ilikuwa mpaka 3M. Hapo ndo ukawa mwisho wa blog yangu nikajielekeza pengine kutafuta kipato!

Kiufupi ni kuwa mitego yangu yote awamu ya tano iligoma! JPM ametuharibia maisha wengi.

Nashukuru kwa sasa naendelea vizuri na ajira za mama nimebahatika hivyo naanza maisha upya.

Asante SSH, wakumbuke vijana wengi wanaishi maisha ya shida sana.
Mungu ambariki Rais wetu Samia. Hayo ndiyo matokeo ya conducive business environment and investment climate.

Mwendazake alikuwa HOSTILE na foreign investors na alikuwa reckless tyrant hata kwa local business people.

He had to DIE by any means for our country to escape becoming another Zimbabwe. Praise to our Lord
 
ukweli umuweka mtu huru , umeandika ukweli mtu . shida inakuja nani atakiona kilio cha vijana waliomaliza 2015 na 2016. jibu hakuna .
Maisha lazima yaendelee.
 
Back
Top Bottom