Hayati Magufuli alikuwa na utashi lakini alikosa uwezo

Hayati Magufuli alikuwa na utashi lakini alikosa uwezo

Haya maneno ya kizalendo lakini unasemaje...ameweka mbele utaifa badala ya ubinafsi wenu...unasahau Kuna watu wanafia nchi ili iendelee..watu wanapigana Vita Kongo kutetea nchi yao, wengine wanakufa Kwenye vita ili nchi iendelee kuwa na amani..hivi haya huyaelewi..wewe utakuwa sio Mtanzania halisi
Mbona jpm Sasa alikuwa anatuingiza Chaka.
 
Kinachonisikitisha mimi mpaka kesho ni badala kama nchi kujaribu ku own vision yake kwa faida ya nchi na kumwondoa yeye kama person katika scene, ili nchi isiingie hasara mara mbili, tumeweka visasi at individuals mpaka tumefanya kuwa agenda ya kitaifa vitu ambavyo ni very personal na kwasababu hiyo vitaliumiza taifa zima na kuongeza hasara mara mbili kisha kama nchi itatubidi turudi nyuma kwanza badala ya kuendelea mbele....Hapa tumeonyesha udhaifu katika tasnia ya uongozi, we are not resilient!
Na tunakubali kuleta uhasama wa individuals kwenye level ya utendaji wa kitaifa badala ya kuzingatia uongozi wa kitaasisi...Hapa ndipo napokubaliana na watu wote wanaopendekeza Katiba mpya...Maana individuals wameonyesha ku abuse power zao kwakua tu hakuna instruments strong za kuwa mitigate preferences zao....A big weakness kwa katiba tuliyonayo sasa
 
Kumbuka miaka mitano hakuweza kuajiri kabisa ndo chanzo Cha walimu, madaktari na manesi kujaa mtaani ambapo amempa shida sana mama kuwaabsorb wote Hawa. Kundi ni kubwa mno. Jk alikwenda vizuri sana ambapo alikuwa anaajiri sector hizi kwa maelefu labda ukatae mwenyewe kuajiriwa na serikali na ukumbuke enzi za jk private sector ilikuwa strong kiasi ambacho wengi hawakitaka kuajiriwa serikalini kabisa. Halafu ukumbuke miaka mitano yote hakuweza kuongeza kabisa mishahara ambapo jk alikuwa anaongeza kila mwaka na hii ikapelekea mzunguko wa pesa kuwa mkubwa. Hili neno vyuma vimekaza limeanza kuimbwa kipindi Cha jpm. Hii ni proof kwamba serikali ya jpm haikuwa na hela ila mabavu tu na ndo mana alitamani kuvifuta vyombo vyote vya habari ali asihojiwe kwa lolote na udictator umeanzia kwake.
Mkuu acha uongo tuliopata ajira chini ya JPM tupo wengi sana ninawashkaji zangu walipata ajira TANAPA huko 2018 na walimaliza chuo 2014, nina watu ninaowafahamu walisoma biomedical waliajiriwa 2017 ninawafahamu pia jamaa zangu tena mainjinia waliajiriwa na JPM 2020 kwenda kufundisha shule za ufundi. Achilia mbali wahasibu. Sasa unaposema hakuajiri unamaana gani kama hauna ushahidi kaa kimya usitende dhambi bure na inawezekana wewe sio mfuatiliaji wa mambo unapenda kusikiliza maneno ya wanasiasa bila wewe kufanya utafiti.
 
Wale wananchi wanaomsikiliza TL kwenye mikutano ni wajinga? Wanafurika vile na ukosoaji unaendelea.

Jpm aliteka nyoyo za watu wajinga wajinga tu. Ila wanaoelewa na kupata habari zake walikinai
Hapa una prove kitu, kwamba hao unaowaita waelewa na unaodai wana access kwenye taarifa sahihi, ndiyo ambao unawachongea hapa ujinga wao, maana wameshindwa kuonyesha kwa vitendo aliyoonyesha JPM kwa hao unaowaita wajinga. Then it means tuna watu ambao siyo sahihi kwenye hizo positions kwa context ya wapiga kura wao na una verify kwamba siyo democracy inaamua bali dola, sorry to say so!
 
Hivi umelewa kweli nilichoandila? Nimesemea kwamba aim ni kujiajiri ili kupata kipato kikubwa ila lazima upate pa kuanzia. Huwezi kujiajiri from no where. Ndo mana nikatoa mfano wa Elon musk

Mtaji wa masikini ni nguvu zake mwenyewe…acha kupotosha jamii kwa uvivu wako bro…kusoma sio utajiri…na I doubt km hata hio elimu unayo na kama kweli unayo basi una shida nyingine maana nina marafiki madaktari wasingeongea hivi..

Baada ya kusoma comment zako naona wewe unachuki tu na huyu mwamba..ebu msikilize mzee huyu upate picha kidogo ya wapambanaji…maana nikikuandikia vitabu vya kusoma hutasoma…maana ushasema kuandika hujui una prefer voice notes..

 
Ujui uwezo wa Magufuli Wewe, Magufuli alifungua masoko ya madini na akaingia mkataba na warabu kuwa madini yote yatanunuliwa kutoka hapa nchini,akawa anapata kodi yake bila buguza,ndio maana haukuweza kuona mambo ya tozo,mashariti ya hovyo kwenye mambo ya mikopo,mairais wa nchi kubwa waliomwitaji walikuja wenyewe, pasipo yeye kujipereka kama changu kuuza rasilimali za nchi eti unatafuta wawekezaji,huku wakija unawaambia wasilipe kodi miaka 5, lakini wananchi wako unawaibia chao kupitia tozo na kodi mbalimbali.
Naunga mkono hoja
 
Kumbuka miaka mitano hakuweza kuajiri kabisa ndo chanzo Cha walimu, madaktari na manesi kujaa mtaani ambapo amempa shida sana mama kuwaabsorb wote Hawa. Kundi ni kubwa mno. Jk alikwenda vizuri sana ambapo alikuwa anaajiri sector hizi kwa maelefu labda ukatae mwenyewe kuajiriwa na serikali na ukumbuke enzi za jk private sector ilikuwa strong kiasi ambacho wengi hawakitaka kuajiriwa serikalini kabisa. Halafu ukumbuke miaka mitano yote hakuweza kuongeza kabisa mishahara ambapo jk alikuwa anaongeza kila mwaka na hii ikapelekea mzunguko wa pesa kuwa mkubwa. Hili neno vyuma vimekaza limeanza kuimbwa kipindi Cha jpm. Hii ni proof kwamba serikali ya jpm haikuwa na hela ila mabavu tu na ndo mana alitamani kuvifuta vyombo vyote vya habari ali asihojiwe kwa lolote na udictator umeanzia kwake.
Hakuna maana ya kuongeza mishahara kama huwezi kudhibiti mfumko wa bei,unawaongeza unawaongeza tsh 12000,halafu unaruhusu mfumko mkubwa wa bei?
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Mi mwenyewe dakatari hapa singida hospitali ya rufaa niliajiriwa kipindi Cha jk. Hapa Kuna uhaba mkubwa wa madaktari kama kumi hivi wanahitajika upande wa epidemiology nk. Sasa kama mjini Kuna uhaba he vijijini si ni kero na wakati huohuo mtaani wamejaa.
Ninachosema inapaswa uelewe wewe Bado mdogo sana. Enzi za jk hakuna dakatari hata mmoja aliyemaliza akakaa mtaani bila ajira ila jpm aliwarindika mtaani na tatizo likaanzia hapo. Unakuta dakatari amesota miaka mitano muhimbili halafu anauza mitumba kariakoo elimu ikaanza kushuka thamani kipindi chake. We unafikiri kwa Nini wasomi au graduates wamefurahia sana uongozi wa mama
Ni kipindi gn madaktari waligoma?
 
Hakuna maana ya kuongeza mishahara kama huwezi kudhibiti mfumko wa bei,unawaongeza unawaongeza tsh 12000,halafu unaruhusu mfumko mkubwa wa bei?
Kuongeza mishahara siyo wishes za rais Bali ni sheria na IPO inafanyakazi unless kama jpm aliamia awe dictator kama alivyoamua kuwaambia wakurugenzi watangaze hivyohivyo mgombea wa ccm hata kama hajashinda ubunge. Ukiona rais ambaye anakanyaga sheria zilizopo Kuna tatizo kubwa
 
Mimi nakubali sana kuwa JPM alikuwa na utashi mkubwa na nchi hii lakini uwezo alikuwa hana. Hii inadhihirishwa na miradi mikubwa aliyoianzisha, japo nina uhakika asingeweza kuimaliza maana tayari alinipiga pini yeye mwenye kwa kuweza mazingira magumu kwa wafanyabiashara wakubwa, kutoamini kuwekeza tena nchini kwa sababu ya kufokafoka kwake na ikumbukwe hawa ndiyo walipa kodi. Yeye alibaki tu anazalisha machinga wengi ambapo kimsingi hawalipi kodi.

Pili alishajenga ukuta na mataifa wahisani kwa kauli zake hivyo mikopo au misaada tukanyimwa kabisa.

Ndiyo alipenda nchi yake lakini uwezo alikuwa Hana. Akaanza kuvamia akaunti za matajiri ili kuiba hela kwa ajiri ya kumaliza miradi hiyo ambapo in the long run nchi ingeburuzwa mahakamani ndo ndo mana kila kukicha ndege zilikuwa zinakamatwa hapa na pale ambapo baadae shirika lingejikuta halina ndege tena.
Naamin angeifikisha mbali hii nchi hasa kimiundombinu na uwajibikaji! But kilichofanya nione ana tatizo ni pale kuona upinzani ni adui no 1 Nchi hii. Pia kama kwel alitaman hii Nchi ifike mbali na ainyooshe alipaswa kuikita katiba mpya ambayo ni msumeno kama china, ukiiba au kufisad ni kifungo maisha au kunyongwa! Lkn unataka unyooshe Nchi kwa katiba hii? Never ever.
 
Hapa nakubaliana na wewe, alipoteza energy yake kwa watu ambao hata siyo significant kwa nchi; hapa ndipo honesty ya watanzania inapokosa kuvuka mtihani. Wengi wetu tupo partial hata sasa, wengi wanashindwa ku cite makosa ya kweli ya JPM kwakukosa honesty na objectivity character....Utakuta mtu ana kinyongo chake personal kwa mambo yake binafsi anayafungamanisha na nchi as if yeye ni nchi. Ndiyo sababu mtu anaweza tumia cheo chake kumwadabisha mgoni wake na bado akaona okay...Ni dalili ya kukosa integrity na ustaarabu.

Kama kuwa victimized ni wengi tumekuwa victimized kwakua tu JPM alikuwa hana leadership skills na pia hakuwa anaangalia details zaidi ya dhamira yake ya kujenga nchi ambayo ali demonstrate kiuhalisia kila mtu objective analijua hili na kwa maoni yangu, hakuna kiongozi aliyewahi kubeba nchi na agenda zake kwenye nafsi yake kama yeye na baba wa taifa; but a lot of us forget this...Namshukuru Speaker juzi amelisema hili, tunafanya sana personification na kushindwa kuangalia issues at hand...Ni dalili ya kukosa critical thinking na ni indicator ya kutoelimika. Mataifa ya wenzetu wanaweza ku separate issues from persons...Unaweza mchukia mtu lakini ukampa haki yake...
Well said! Ndio maana mara zote nasema jpm alikuwa na dhamira ya dhati ya kuona nchi inasonga mbele na kwa nafasi yake kama kiongozi senior kwenye serikali miaka mingi anajua uhuni mwingi uliokuwa unaiumiza nchi . Shida ni pale alipoanza kuhangaika na upinzani wakati wapinzani wake wa kweli waliokuwa wanaifisadi nchi wako chamani mwake.
 
Kuongeza mishahara siyo wishes za rais Bali ni sheria na IPO inafanyakazi unless kama jpm aliamia awe dictator kama alivyoamua kuwaambia wakurugenzi watangaze hivyohivyo mgombea wa ccm hata kama hajashinda ubunge. Ukiona rais ambaye anakanyaga sheria zilizopo Kuna tatizo kubwa
Kama hakuna chakuongeza sheria itaongeza? Vitu vingine mtumie akili kuvisema...
 
Tafuta tarifa ujisomee acha kukalili maneno ya vijiweni,uliza Magufuli alifungua hospital na Zahanati ngapi,hao walopelekwa kwenye Zahanati na hospital walitokea wapi kama sio kuajiliwa?unaweza kuonyesha malalamiko ya hospital yeyeto nchini ikionyesha upungufu wa madaktari kama kipindi cha Kikwete? Magufuli aliajiri kwa tija sio kwa miemuko ,mradi umeajili.
Acha ku panic ndugu hoja kwa hoja au ndo msiojulikana
 
Hhahaha..kwa kweli walikinai na habari zake za
-kununua midege 11 ndani ya miaka mitano
-kuanzisha mradi wa Stiglers
-kuanzisha mradi wa sgr
-kutengeneza mifumo ya barabara nchi nzima
-kujenga vituo vya mabasi na flyovers
-kujenga madarasa nchi nzima
-kutumbua watumishi hewa, vyeti feki..n.k
N.k n.k.n.k..lakini hii ni kazi ya ccm msijifanye hamuelewi..ni Utekelezaji wa Ilani ya ccm...ambayo mama yetu Dr SSH anaendeleza bila kuchoka..watu waendelee kukinai tu hakuna namna
 
Back
Top Bottom