Mbona jpm Sasa alikuwa anatuingiza Chaka.Haya maneno ya kizalendo lakini unasemaje...ameweka mbele utaifa badala ya ubinafsi wenu...unasahau Kuna watu wanafia nchi ili iendelee..watu wanapigana Vita Kongo kutetea nchi yao, wengine wanakufa Kwenye vita ili nchi iendelee kuwa na amani..hivi haya huyaelewi..wewe utakuwa sio Mtanzania halisi
Mkuu acha uongo tuliopata ajira chini ya JPM tupo wengi sana ninawashkaji zangu walipata ajira TANAPA huko 2018 na walimaliza chuo 2014, nina watu ninaowafahamu walisoma biomedical waliajiriwa 2017 ninawafahamu pia jamaa zangu tena mainjinia waliajiriwa na JPM 2020 kwenda kufundisha shule za ufundi. Achilia mbali wahasibu. Sasa unaposema hakuajiri unamaana gani kama hauna ushahidi kaa kimya usitende dhambi bure na inawezekana wewe sio mfuatiliaji wa mambo unapenda kusikiliza maneno ya wanasiasa bila wewe kufanya utafiti.Kumbuka miaka mitano hakuweza kuajiri kabisa ndo chanzo Cha walimu, madaktari na manesi kujaa mtaani ambapo amempa shida sana mama kuwaabsorb wote Hawa. Kundi ni kubwa mno. Jk alikwenda vizuri sana ambapo alikuwa anaajiri sector hizi kwa maelefu labda ukatae mwenyewe kuajiriwa na serikali na ukumbuke enzi za jk private sector ilikuwa strong kiasi ambacho wengi hawakitaka kuajiriwa serikalini kabisa. Halafu ukumbuke miaka mitano yote hakuweza kuongeza kabisa mishahara ambapo jk alikuwa anaongeza kila mwaka na hii ikapelekea mzunguko wa pesa kuwa mkubwa. Hili neno vyuma vimekaza limeanza kuimbwa kipindi Cha jpm. Hii ni proof kwamba serikali ya jpm haikuwa na hela ila mabavu tu na ndo mana alitamani kuvifuta vyombo vyote vya habari ali asihojiwe kwa lolote na udictator umeanzia kwake.
Hapa una prove kitu, kwamba hao unaowaita waelewa na unaodai wana access kwenye taarifa sahihi, ndiyo ambao unawachongea hapa ujinga wao, maana wameshindwa kuonyesha kwa vitendo aliyoonyesha JPM kwa hao unaowaita wajinga. Then it means tuna watu ambao siyo sahihi kwenye hizo positions kwa context ya wapiga kura wao na una verify kwamba siyo democracy inaamua bali dola, sorry to say so!Wale wananchi wanaomsikiliza TL kwenye mikutano ni wajinga? Wanafurika vile na ukosoaji unaendelea.
Jpm aliteka nyoyo za watu wajinga wajinga tu. Ila wanaoelewa na kupata habari zake walikinai
Hivi umelewa kweli nilichoandila? Nimesemea kwamba aim ni kujiajiri ili kupata kipato kikubwa ila lazima upate pa kuanzia. Huwezi kujiajiri from no where. Ndo mana nikatoa mfano wa Elon musk
Naunga mkono hojaUjui uwezo wa Magufuli Wewe, Magufuli alifungua masoko ya madini na akaingia mkataba na warabu kuwa madini yote yatanunuliwa kutoka hapa nchini,akawa anapata kodi yake bila buguza,ndio maana haukuweza kuona mambo ya tozo,mashariti ya hovyo kwenye mambo ya mikopo,mairais wa nchi kubwa waliomwitaji walikuja wenyewe, pasipo yeye kujipereka kama changu kuuza rasilimali za nchi eti unatafuta wawekezaji,huku wakija unawaambia wasilipe kodi miaka 5, lakini wananchi wako unawaibia chao kupitia tozo na kodi mbalimbali.
Hakuna maana ya kuongeza mishahara kama huwezi kudhibiti mfumko wa bei,unawaongeza unawaongeza tsh 12000,halafu unaruhusu mfumko mkubwa wa bei?Kumbuka miaka mitano hakuweza kuajiri kabisa ndo chanzo Cha walimu, madaktari na manesi kujaa mtaani ambapo amempa shida sana mama kuwaabsorb wote Hawa. Kundi ni kubwa mno. Jk alikwenda vizuri sana ambapo alikuwa anaajiri sector hizi kwa maelefu labda ukatae mwenyewe kuajiriwa na serikali na ukumbuke enzi za jk private sector ilikuwa strong kiasi ambacho wengi hawakitaka kuajiriwa serikalini kabisa. Halafu ukumbuke miaka mitano yote hakuweza kuongeza kabisa mishahara ambapo jk alikuwa anaongeza kila mwaka na hii ikapelekea mzunguko wa pesa kuwa mkubwa. Hili neno vyuma vimekaza limeanza kuimbwa kipindi Cha jpm. Hii ni proof kwamba serikali ya jpm haikuwa na hela ila mabavu tu na ndo mana alitamani kuvifuta vyombo vyote vya habari ali asihojiwe kwa lolote na udictator umeanzia kwake.
Ni kipindi gn madaktari waligoma?Mi mwenyewe dakatari hapa singida hospitali ya rufaa niliajiriwa kipindi Cha jk. Hapa Kuna uhaba mkubwa wa madaktari kama kumi hivi wanahitajika upande wa epidemiology nk. Sasa kama mjini Kuna uhaba he vijijini si ni kero na wakati huohuo mtaani wamejaa.
Ninachosema inapaswa uelewe wewe Bado mdogo sana. Enzi za jk hakuna dakatari hata mmoja aliyemaliza akakaa mtaani bila ajira ila jpm aliwarindika mtaani na tatizo likaanzia hapo. Unakuta dakatari amesota miaka mitano muhimbili halafu anauza mitumba kariakoo elimu ikaanza kushuka thamani kipindi chake. We unafikiri kwa Nini wasomi au graduates wamefurahia sana uongozi wa mama
Kuongeza mishahara siyo wishes za rais Bali ni sheria na IPO inafanyakazi unless kama jpm aliamia awe dictator kama alivyoamua kuwaambia wakurugenzi watangaze hivyohivyo mgombea wa ccm hata kama hajashinda ubunge. Ukiona rais ambaye anakanyaga sheria zilizopo Kuna tatizo kubwaHakuna maana ya kuongeza mishahara kama huwezi kudhibiti mfumko wa bei,unawaongeza unawaongeza tsh 12000,halafu unaruhusu mfumko mkubwa wa bei?
Naamin angeifikisha mbali hii nchi hasa kimiundombinu na uwajibikaji! But kilichofanya nione ana tatizo ni pale kuona upinzani ni adui no 1 Nchi hii. Pia kama kwel alitaman hii Nchi ifike mbali na ainyooshe alipaswa kuikita katiba mpya ambayo ni msumeno kama china, ukiiba au kufisad ni kifungo maisha au kunyongwa! Lkn unataka unyooshe Nchi kwa katiba hii? Never ever.Mimi nakubali sana kuwa JPM alikuwa na utashi mkubwa na nchi hii lakini uwezo alikuwa hana. Hii inadhihirishwa na miradi mikubwa aliyoianzisha, japo nina uhakika asingeweza kuimaliza maana tayari alinipiga pini yeye mwenye kwa kuweza mazingira magumu kwa wafanyabiashara wakubwa, kutoamini kuwekeza tena nchini kwa sababu ya kufokafoka kwake na ikumbukwe hawa ndiyo walipa kodi. Yeye alibaki tu anazalisha machinga wengi ambapo kimsingi hawalipi kodi.
Pili alishajenga ukuta na mataifa wahisani kwa kauli zake hivyo mikopo au misaada tukanyimwa kabisa.
Ndiyo alipenda nchi yake lakini uwezo alikuwa Hana. Akaanza kuvamia akaunti za matajiri ili kuiba hela kwa ajiri ya kumaliza miradi hiyo ambapo in the long run nchi ingeburuzwa mahakamani ndo ndo mana kila kukicha ndege zilikuwa zinakamatwa hapa na pale ambapo baadae shirika lingejikuta halina ndege tena.
Well said! Ndio maana mara zote nasema jpm alikuwa na dhamira ya dhati ya kuona nchi inasonga mbele na kwa nafasi yake kama kiongozi senior kwenye serikali miaka mingi anajua uhuni mwingi uliokuwa unaiumiza nchi . Shida ni pale alipoanza kuhangaika na upinzani wakati wapinzani wake wa kweli waliokuwa wanaifisadi nchi wako chamani mwake.Hapa nakubaliana na wewe, alipoteza energy yake kwa watu ambao hata siyo significant kwa nchi; hapa ndipo honesty ya watanzania inapokosa kuvuka mtihani. Wengi wetu tupo partial hata sasa, wengi wanashindwa ku cite makosa ya kweli ya JPM kwakukosa honesty na objectivity character....Utakuta mtu ana kinyongo chake personal kwa mambo yake binafsi anayafungamanisha na nchi as if yeye ni nchi. Ndiyo sababu mtu anaweza tumia cheo chake kumwadabisha mgoni wake na bado akaona okay...Ni dalili ya kukosa integrity na ustaarabu.
Kama kuwa victimized ni wengi tumekuwa victimized kwakua tu JPM alikuwa hana leadership skills na pia hakuwa anaangalia details zaidi ya dhamira yake ya kujenga nchi ambayo ali demonstrate kiuhalisia kila mtu objective analijua hili na kwa maoni yangu, hakuna kiongozi aliyewahi kubeba nchi na agenda zake kwenye nafsi yake kama yeye na baba wa taifa; but a lot of us forget this...Namshukuru Speaker juzi amelisema hili, tunafanya sana personification na kushindwa kuangalia issues at hand...Ni dalili ya kukosa critical thinking na ni indicator ya kutoelimika. Mataifa ya wenzetu wanaweza ku separate issues from persons...Unaweza mchukia mtu lakini ukampa haki yake...
Kama hakuna chakuongeza sheria itaongeza? Vitu vingine mtumie akili kuvisema...Kuongeza mishahara siyo wishes za rais Bali ni sheria na IPO inafanyakazi unless kama jpm aliamia awe dictator kama alivyoamua kuwaambia wakurugenzi watangaze hivyohivyo mgombea wa ccm hata kama hajashinda ubunge. Ukiona rais ambaye anakanyaga sheria zilizopo Kuna tatizo kubwa
Acha ku panic ndugu hoja kwa hoja au ndo msiojulikanaTafuta tarifa ujisomee acha kukalili maneno ya vijiweni,uliza Magufuli alifungua hospital na Zahanati ngapi,hao walopelekwa kwenye Zahanati na hospital walitokea wapi kama sio kuajiliwa?unaweza kuonyesha malalamiko ya hospital yeyeto nchini ikionyesha upungufu wa madaktari kama kipindi cha Kikwete? Magufuli aliajiri kwa tija sio kwa miemuko ,mradi umeajili.