Kama tunavyojua, Hayati Magufuli, pamoja na kuwa rais wa Tanzania, hajawahi kuwa Balozi hata wa Nyumba kumi. Ndani ya Miaka Miwili akalewa madaraka.
Kumbuka Lowassa ni Mwanajeshi wa zamani na aliyewahi kupigana wakati wa vita kati ya Uganda na Tanzania mwaka 1978/79. Kaitumikia Nchi hadi uzee wake.
Lowasa ndiye alifanikisha upatikanaji wa fedha za kujenga chuo kikuu cha Dodoma kilichoanzishwa 2007 pia alianzisha Shule za Kata. Miradi ya Maji kutoka Ziwa Victoria hadi Shinyanga nk.
Akatokea Mzilankende mmoja fulani kutokea huko kijiji cha Lubambangwe akaleta tafrani kwenye Nchi.
Mungu akamjalia
nafasi ya juu ambayo kabila zote za watu, mataifa na watu wa kila lugha walimhofu na kumwogopa. Wale ambao mzilankende huyu alitaka kuwaua, aliwaua; wale aliotaka kuwaacha hai, aliwaacha hai; wale aliotaka kuwapandisha cheo, aliwapandisha; aliotaka kuwashusha, aliwashusha. Lakini moyo wake ulipokuwa na majivuno na kuwa mgumu kwa kiburi, aliondolewa kutoka kwa kiti chake cha ufalme na kuvuliwa utukufu wake.
Kwamba Lowassa hatakiwi kusimama Geita kusalimiana na watu. Akachukuliwa na Polisi akapelekwa korokoroni Geita. Magufuli akawapongeza Polisi kwa kazi nzuri.
Hivi Magufuli alikuwa anajiona nani? Hakuwa na Tofauti na Belshaza.
Belshaza ni nani?
Belshaza ambaye alirithi ufalme toka kwa mfalme Nebukadneza. Siku moja Mfalme Belshaza alifanya karamu kubwa kwa ajili ya maelfu ya wakuu wake na akanywa mvinyo pamoja nao. Wakati Belshaza alipokuwa akinywa mvinyo wake, aliamuru viletwe vile vikombe vya dhahabu na fedha ambavyo Nebukadneza baba yake alikuwa amevichukua kutoka hekaluni huko Yerusalemu, ili mfalme na wakuu wake, wake zake na masuria wake waweze kuvinywea. Kwa hiyo wakavileta vile vikombe vya dhahabu ambavyo vilikuwa vimechukuliwa kutoka Hekalu la Mungu huko Yerusalemu, naye mfalme na wakuu wake, wake zake na masuria wake wakavinywea.
Ghafula vidole vya mkono wa mwanadamu vilitokea na kuandika juu ya ukuta, karibu na kinara cha taa ndani ya jumba la mfalme. Mfalme akatazama kitanga kilivyokuwa kikiandika.
Mfalme akawaita wasihiri, wanajimu na waganga waletwe, naye akawaambia hawa wenye hekima wa Babeli, “Yeyote asomaye maandishi haya.
Ndipo Danieli akamjibu mfalme, “Waweza kubaki na zawadi zako mwenyewe na kumpa mtu mwingine zawadi zako. Hata hivyo, nitasoma maandishi kwa mfalme na kumwambia maana yake.
Ndipo Danieli akamjibu mfalme, “Waweza kubaki na zawadi zako mwenyewe na kumpa mtu mwingine zawadi zako. Hata hivyo, nitasoma maandishi kwa mfalme na kumwambia maana yake.
“Haya ndiyo maneno yaliyoandikwa mene, mene, tekeli na peresi
“Mene: Mungu amezihesabu siku za utawala wako na kuukomesha.
Tekeli: Wewe umepimwa katika mizani na umeonekana umepungua.
Peresi: Ufalme wako umegawanywa na kupewa Wamedi na Waajemi.”
Ndipo kwa amri ya Belshaza, Danieli akavikwa nguo za zambarau na mkufu wa dhahabu shingoni, tena akatangazwa kuwa mtawala wa tatu katika ufalme.
Usiku ule ule, Belshaza mfalme wa Wakaldayo akauawa.
View attachment 2553528