Hayati Magufuli alilewa madaraka, akaagiza Polisi Tanzania wamkamate Edward Lowassa awekwe Korokoroni

Hayati Magufuli alilewa madaraka, akaagiza Polisi Tanzania wamkamate Edward Lowassa awekwe Korokoroni

maskini lowassa alijua kuhangaika kuusaka uRais wa nchi hii nikikumbuka 2015 nacheka kimoyomoyo 😃
 
Kama tunavyojua, Hayati Magufuli, pamoja na kuwa rais wa Tanzania, hajawahi kuwa Balozi hata wa Nyumba kumi. Ndani ya Miaka Miwili akalewa madaraka.

Kumbuka Lowassa ni Mwanajeshi wa zamani na aliyewahi kupigana wakati wa vita kati ya Uganda na Tanzania mwaka 1978/79. Kaitumikia Nchi hadi uzee wake.

View attachment 2553514
Edward Lowassa​

Lowasa ndiye alifanikisha upatikanaji wa fedha za kujenga chuo kikuu cha Dodoma kilichoanzishwa 2007 pia alianzisha Shule za Kata. Miradi ya Maji kutoka Ziwa Victoria hadi Shinyanga nk.

Akatokea Mzilankende mmoja fulani kutokea huko kijiji cha Lubambangwe akaleta tafrani kwenye Nchi.

Mungu akamjalia
nafasi ya juu ambayo kabila zote za watu, mataifa na watu wa kila lugha walimhofu na kumwogopa. Wale ambao mzilankende huyu alitaka kuwaua, aliwaua; wale aliotaka kuwaacha hai, aliwaacha hai; wale aliotaka kuwapandisha cheo, aliwapandisha; aliotaka kuwashusha, aliwashusha. Lakini moyo wake ulipokuwa na majivuno na kuwa mgumu kwa kiburi, aliondolewa kutoka kwa kiti chake cha ufalme na kuvuliwa utukufu wake.

Kwamba Lowassa hatakiwi kusimama Geita kusalimiana na watu. Akachukuliwa na Polisi akapelekwa korokoroni Geita. Magufuli akawapongeza Polisi kwa kazi nzuri.

Hivi Magufuli alikuwa anajiona nani? Hakuwa na Tofauti na Belshaza.



Belshaza ni nani?
Belshaza ambaye alirithi ufalme toka kwa mfalme Nebukadneza. Siku moja Mfalme Belshaza alifanya karamu kubwa kwa ajili ya maelfu ya wakuu wake na akanywa mvinyo pamoja nao. Wakati Belshaza alipokuwa akinywa mvinyo wake, aliamuru viletwe vile vikombe vya dhahabu na fedha ambavyo Nebukadneza baba yake alikuwa amevichukua kutoka hekaluni huko Yerusalemu, ili mfalme na wakuu wake, wake zake na masuria wake waweze kuvinywea. Kwa hiyo wakavileta vile vikombe vya dhahabu ambavyo vilikuwa vimechukuliwa kutoka Hekalu la Mungu huko Yerusalemu, naye mfalme na wakuu wake, wake zake na masuria wake wakavinywea.

Ghafula vidole vya mkono wa mwanadamu vilitokea na kuandika juu ya ukuta, karibu na kinara cha taa ndani ya jumba la mfalme. Mfalme akatazama kitanga kilivyokuwa kikiandika.

Mfalme akawaita wasihiri, wanajimu na waganga waletwe, naye akawaambia hawa wenye hekima wa Babeli, “Yeyote asomaye maandishi haya.

Ndipo Danieli akamjibu mfalme, “Waweza kubaki na zawadi zako mwenyewe na kumpa mtu mwingine zawadi zako. Hata hivyo, nitasoma maandishi kwa mfalme na kumwambia maana yake.

Ndipo Danieli akamjibu mfalme, “Waweza kubaki na zawadi zako mwenyewe na kumpa mtu mwingine zawadi zako. Hata hivyo, nitasoma maandishi kwa mfalme na kumwambia maana yake.

“Haya ndiyo maneno yaliyoandikwa mene, mene, tekeli na peresi

“Mene: Mungu amezihesabu siku za utawala wako na kuukomesha.

Tekeli: Wewe umepimwa katika mizani na umeonekana umepungua.

Peresi: Ufalme wako umegawanywa na kupewa Wamedi na Waajemi.”

Ndipo kwa amri ya Belshaza, Danieli akavikwa nguo za zambarau na mkufu wa dhahabu shingoni, tena akatangazwa kuwa mtawala wa tatu katika ufalme.

Usiku ule ule, Belshaza mfalme wa Wakaldayo akauawa.

View attachment 2553528
Duh
 
ahahha kazi mnayo kwakweli enyi watumwa wa mafisadi. Hivi mnalipwa shilingi ngapi? Ni kwa mwezi au kwa kila uzi wa kipuuzi kama huu mnaoandika?
 
ahahha kazi mnayo kwakweli enyi watumwa wa mafisadi. Hivi mnalipwa shilingi ngapi? Ni kwa mwezi au kwa kila uzi wa kipuuzi kama huu mnaoandika?
 
Shule za Kata mhamasishaji na msimamizi ni nani??Au ulikuwa hujazaliwa??Na Chuo Kikuu Dodoma wakati kinajengwa Waziri Mkuu alikuwa nani??
Mwenye serikali yake ni rais naye ndio mtendaji wa kila jambo ndio maana hata leo tunaimba kumsifia rais acha ubwege wa kuniuliza maswali ya kijinga.
 
Tafiti hupingwa kwa Tafiti mpya
Magufuli alivyokuwa akijisifia mlikuwa na utafiti gani,nchi hii udini ni tatizo sana maana naona leo umeungana na wapinzani wako ku support ujinga kwa sababu tu ya chuki binafsi dhidi ya Kikwete hata sasa wengi wanamtukana na kumponda Rais Samia si kwamba hafanyi kitu ila tatizo ni dini yake, Uzanzibari wake na jinsia yake.
 
Tanzania bado tuna wajinga wengi sana,Yaan mtu mzima na akili zake timamu unaweza kumdhihaki marehem.R.I.P Jembe
 
Marais wote walikuwa na mawaziri wakuu na sifa wakapata marais lakini wakati wa rais Kikwete anasifiwa waziri mkuu au tuseme mawaziri wakuu wengine hawajafanya lolote kuwasaidia marais wao ila Lowassa tu.
 
Chuki mbaya sana, eti Lowasa ndiyo katafuta hela za kujenga chuo kikuu Dodoma na kuanzisha shule za kata!
Sina uhakika na kutafuta pesa za kujengea chuo kikuu Dodoma.

LAKINI NI KWELI kuwa sekondari za kata lilikuwa ni wazo la Lowasa, na ujenzi wa shule hizo kwa nchi nzima, ulisimamiwa na yeye mwenyewe akiwa Waziri Mkuu.

Suala pia la kuvuta maji kutoka ziwa Victoria, lilikuwa wazo lake, na hata walipletewa upinzani toka Misri, alitoa maelekezo mradi uendelee.
 
Pitia huu uzi tangu mwanzo kuanzia kwa mleta mada hadi wachangiaji utangundua Magufuli aliwaachia watu mimba nyingi sana, ndio zinawafanya wawe na hasira nae kiasi hiki
Watu wanajadili mambo ya maana wewe unaleta utani wa kijinga. Huko kwenye mambo ya mimba, bila shaka ndiyo akili zako zinakoishia.
 
Back
Top Bottom