Hayati Magufuli aliona mbali kuhusu chanjo, ona sasa huko Ulaya wanavyoanza kupukutika

Kuna kitu huwa hamuelewi kusema mitishamba inatibu haimaanishi uitumie kama ilivyo. Ikipita maabara inakua controlled, mfano unaweza kunywa aloe vera kama ilivyo ikaponya tatizo lako lakini maadam haikuchunjwa chochote inaingia na sumu nyingi zaidi mwishowe unapata shida zingine ila ikipita maabara inakuwa neutralized iwe na level optimum za kutibu binadamu
 
Tungefika tu huko kupitia Magufuli sema ndio hivyo kaondoka mapema, japo hilo la ARV wazungu wenyewe huwa wakali sana.
Magufuli angeacha? Hizo device za kupush damu yake mnajua zimetengenezwa na mabeberu? Ina maana bila wazungu kumsaidia angekua ameshafariki toka 2011!!

Kejeli hazisaidii.....
 

tusi argue sana kwenye hili. Kuhusu kupata chanjo au kutopata linaelekea kuwa ni maoni na kupenda kwa mtu. inavyoelekea kuchanjwa haitakuwa lazima.
 
Hilo haliepukiki maana anataka kurudisha mahusiano mazuri na wazungu kwa hivyo huwezi kuelewana na hao wazungu bila hicho chanjo.
Sababu chanjo zenyewe zimeleta mlipuko zaidi,ikitokea watu wakichanjwa ndo ikaongezeka rais atakuwa na wakati mgumu sana,lolote linalofanyika lisifanyike kuwafurahisha wazungu ila wananchi.Kikwete alijitahidi kuwafurahisha tukaona akina Bush,Obama wakipishana Dar kumbe walikuwa na yao sasa hivyi nchi ni jina tu kuwa ina gesi.
 
Hebu acha uongo wako!!!!! Unajua maana ya neno kupukutika!? Hebu tuambie hiyo idadi ya waliopukutika katika nchi za Ulaya na Afrika ambazo chanjo ya COVID-19 imetolewa. Kuna watu wanajua kuongeza chumvi dah!!!
 
Chanjo ya PFIZER imepunguza sana mzigo wa UVIKO Uingereza.

Utafiti uliohusisha watu 170,000 baada ya kupata chanjo umeonyesha idadi ya wagonjwa kupungua kwa asilimia 75 kwa watu wenye umri kati ya miaka 80 hadi 83 ndani ya siku 35 hadi 41 baada ya kupata dozi ya kwanza.
Kasi ya maambukizi imepungua kwa asilimia 70. Idadi ya waathirika imeshuka kutoka asilimia 15.3 hadi 4.6 kwa watu 100,000 waliopimwa.

CHANZO
telegraph.co.uk April 14 2021
11:27 PM
 
CC Kingwangalah na Mbowe hawa ndo wapiga debe watanzania wapigwe chanjo sasa mtu ambae hana safari za kwenda Ulaya yeye ni Mwanza ,Kigoma ,Dar Chanjo ya nini ? Wapigwe wenye kutaka kwenda kwa Mabeberu

Mkuu, una maana watanzania waliopata covodi-19 na kufa au kupona walisafiri ikawapata huko?? Tanzania hatujaifunga nchi, wageni waruhusiwa kuingia - hudhani hao wanaweza kuambukiza hawa ambao hawajasafiri??

Ama kweli ujinga ni adui mkubwa kuliko anavodhaniwa. Sikuwahi kudhani kuna akili imefungwa kiasi hiki na ikafungika!!
 
Dawa ni kwa ajiri ya wagonjwa ila hapa tunazungumzia chanjo sio dawa, kama kuganda damu ni moja ya side effects za hizo chanjo basi wangetuambia kabisa ili tujue.
Tatizo ni ubishi usiokuwa na maana.... ungesema waliopewa chanjo ni watu kadhaa, kati ya hao kadhaa wamekufa kwa kuganda damu, ili tujue risk factor zake. Hata ARV kuna watu wakitumia side effects zake ni kupata temporary insanity. Kama nilivyosema hakuna medical product inayomkubali kila mtu. Hata dawa za headache kuna watu zinawakataa. Tatizo kwenye hili jambo tumetanguliza politics over science.
 
Tanzania wasio piga chanjo wangapi wamepukutika? tusimseme jirani mwenye akili tukajifananisha na sisi wapumbavu!
 
Yanayotokea huko utakuta mwamba Mr mbowe anawaza usiku na mchana damu isije kuganda akadhalilika.
Kumbe kufa ni kudhalikika?
Hongera sana kwa kutueleza ukweli wa hilo.
 
tusi argue sana kwenye hili. Kuhusu kupata chanjo au kutopata linaelekea kuwa ni maoni na kupenda kwa mtu. inavyoelekea kuchanjwa haitakuwa lazima.
Kama Yellow fever ni compulsory ndio sembuse Covid? By 2025 itakua unanyimwa visa kma huna chanjo yoyote.
 
Idadi waliopata tatizo la kuganda damu walikuwa 4-5 kati ya milioni 1 wastani. Ambayo ni kawaida kwa chanjo. Nadhani wengi wetu wamepata chanjo ya ukambi / measles. Hata baada ya chanjo ya ukambi kuna mshtuko wa mfumo wa kinga (anaphylactic shock) kwa watu 3.5-10 kati ya milioni.
Kama marehemu rais angejipatia chanjo angekuwa hai.
 
Kinachotokea huko kwa wenzetu lakini si unakiona mkuu na hatua wanazochukua kuhusu hizo Astrazeneca? mwanzoni mlikuwa mnakataa kuwa hizi chanjo hazigandishi damu ila sasa hivi hilo suala lipo wazi na tumeona wengine wamesitisha kwa wenye miaka chini ya 60 na sio Astrazeneca tu bali sasa hivi na Johson& Johnson nazo tunasikia zina tatizo hilo.

Sasa hapo hao nao ni wabishi?
 
Magufuli angeacha? Hizo device za kupush damu yake mnajua zimetengenezwa na mabeberu? Ina maana bila wazungu kumsaidia angekua ameshafariki toka 2011!!

Kejeli hazisaidii.....
Kwani alipata kama sadaka kwamba ni msaada?
 
Bila shaka tuzidi kusali hakika Mungu anaponya , nabii wetu katangulia ila tupo swalama.
Acha ujinga kumuita yule mtesaji nabii.

Korona na chanjo zake,na kukataa chanjo si suala la unabii bali ni sayansi.
 
Nakwambia hiyo mitishamba ipo ambayo imefanyiwa tafiti za kisayansi na kubainika kuwa inatibu ugonjwa fulani au ina faida fulani kiafya na ni kwa sababu gani, sasa hili la kutaka kutuambia kwamba kila dawa lazima iwe imetengenezwaa maabara nadhani hata hao wanasayansi wenyewe watashangaa.

Zipo dawa za asili ambazo hazijafanyiwa tafiti za kisayansi labda uongelee hizo lakini sio kutaka kusema kwamba dawa lazima itoke maabara.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…